Lowassa kuendesha harambee kubwa kuwezesha kila kijana Dar kumiliki bodaboda!

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
kupitia ukurasa wake wa facebook amesema alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya bodaboda amegundua asilimia 50 si zao.

hivo tarehe 15 mwezi wa kwanza atakutana na viongozi wa bodaboda kisha ataandaa harambee kubwa sana ili hiyo asilimia 50 itapewa bodaboda bure ili kujiajiri wenyewe
 

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,237
1,500
kupitia ukurasa wake wa facebook amesema alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya bodaboda amegundua asilimia 50 si zao.

hivo tarehe 15 mwezi wa kwanza atakutana na viongozi wa bodaboda kisha ataandaa harambee kubwa sana ili hiyo asilimia 50 itapewa bodaboda bure ili kujiajiri wenyewe
Mbona kama title inapotosha vile, umeandika kuwa ataendesha harambee ili KILA KIJANA DAR AMILIKI BODABODA YAKE na habari yenyewe inasema ni kwa ajili ya 50% ya waendesha bodaboda wasio zimiliki! ina maana vijana wote Dar ni waendesha bodaboda!
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Si ndio ahadi yake hiyo, tusijali akiwa raisi wetu wakulima wataombewa harambe, kila shule yenye matatizo itaombewa harambee. Maana kwa huyu billionea kila kitu solution yake ni harambee (ndio mazoea ya kutoa hongo za pesa kwenye kila kitu, hata huko NEC, bungeni, kwenye kura na kwengineko kwenye mikono yake). Me too i need harambee.
 

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Hakuna cha bule kutoka kwa EL. Si wenye dini au wakuu wadini, kila aliyepokea cha bule will have to pay back in 2015. Wakati huo kutakuwa na liba yakutosha.
 

2pad

JF-Expert Member
May 10, 2013
328
195
Sasa nikuhadaa watu tu ila CCM sela hakuna eti Raisi mtalajiwa kuamini ajila kwa vijana kupitia Bodaboda ujinga mtupu ajira Niviwanda tu.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
kupitia ukurasa wake wa facebook amesema alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya bodaboda amegundua asilimia 50 si zao.

hivo tarehe 15 mwezi wa kwanza atakutana na viongozi wa bodaboda kisha ataandaa harambee kubwa sana ili hiyo asilimia 50 itapewa bodaboda bure ili kujiajiri wenyewe

I;i kuwaua hao VIJANA wasio na AJIRA ila BODA BODA???
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
36,467
2,000
Noma Sana alisema bodaboda zimeajiri vijana laki 4 so 50% means atawanunulia bodaboda vijana laki 2 piga mahesabu boda boda 1 sh 1.7m,Du 340B hatazitoa wapi huyu mzee?

Cc: Pasco wa JF.
 
Last edited by a moderator:

acha matata

Senior Member
Jan 5, 2011
165
225
Mwambie mimi ni kiongozi wa wenye mapagare (mijumba ambayo haijaisha kujengwa ) Dar. Kama anataka kura zetu basi tuwasiliane hapahapa tuoange harambee.
 

bmalale

Senior Member
Mar 30, 2011
467
0
kupitia ukurasa wake wa facebook amesema alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya bodaboda amegundua asilimia 50 si zao.

hivo tarehe 15 mwezi wa kwanza atakutana na viongozi wa bodaboda kisha ataandaa harambee kubwa sana ili hiyo asilimia 50 itapewa bodaboda bure ili kujiajiri wenyewe

Tupe link ya huo ukursa...coz zipo kurasa nyingi sana za Edward lowassa ........
 

shalet

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,355
2,000
bado kuna watu wanamwita fisadi kama matokeo ya ufisadi ndo haya wacha aendelee
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,622
2,000
Tatizo watanzania wanapenda vya bure sana, na wanasiasa wetu wanajua hilo. Kwa hiyo utashangaa mwanasiasa anavyoahidi kutoa vya bure, nakumbuka mwaka 2010 kulikuwa na ahadai nyingi sana za kutoa vya bure.
 

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,234
2,000
Na haowaliwapa hao ajira hao vijana na hizo boda boda ambao si zao? Atawafanyaje? Akili zingine bana?
 

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
Noma Sana alisema bodaboda zimeajiri vijana laki 4 so 50% means atawanunulia bodaboda vijana laki 2 piga mahesabu boda boda 1 sh 1.7m,Du 340B hatazitoa wapi huyu mzee?

Cc: Pasco wa JF.

hizo ni pesa ndogo sana kwake na marafik zake
 
Last edited by a moderator:

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Kwa vile mimi hata ukurasa wake wa fb, sijawahi kuutembelea, ila kama ni kweli amesema kweli, huu utakuwa ni uongo mtakatifu!.
  1. Kwanza sio kweli kuwa kati waendesha boda boda, eti 50% ndio boda boda zao!. Kati ya waendesha boda boda, 10% ndia zitakuwa boda boda zao, na 90% ni boda boda za matajiri wa boda boda!.
  2. Atakachoweza kufanya ni kupitia umoja wa wenye boda boda, kuwafanyia harambee ili kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki boda boda zao kuliko hali ilivyo sasa kwa boda boda nyingi zaidi kumilikiwa na matajiri wa boda boda!.
  3. Hata kama ingekuwa ni kweli kuwa asilimia 50% ya waendesha boda boda, wanaendesha boda boda za matajiri wa boda boda, hata akiwaendeshea harambee ya kumuliki hizo boda boda, bado wale matajiri watawaajiri vijana wengine kuendesha hizo boda boda zao, hivyo there will never be a time kila mwendesha boda boda ataendesha boda boda yake!.
  4. Boda boda zikiwa nyingi, kutotokea problem ya the economics of scales, the law of demand and supply vs infrastructures ya njia ya hizo bodaboda, hivyo sio tuu kuigeuza vurugu mabarabarani, bali itakuwa ni biashara kichaa isiyo na faida kwa kila familia yenye kijana asiye na kazi, kazi yake itakuwa ni kuendesha boda boda, mwisho hata wale wadada wa ile biashara nao watageukia boda, mchana watachoka, usiku hawatoa zile huduma, itakuwaje kwa sisi wateja wao?!.
  5. Hata hivyo namuunga mkono EL kwa asilimia 100% mass mobilization ndicho kipaji chake!, anakitumia vizuri ku mobilize harambee!, wahangiaji wanaitikia vizuri!.Kila longozi ana kipaji chake!. Nyerere alikuwa na kipaji cha uadilifu na iaminifu na kujenga umoja na mshikamamo. Mwinyi alikuwa na kipaji cha kutoa ruhusa ya kufanyika kila kitu. Mkapa alikuwa Mr. Clean. JK, Mr. Smilling and trips!. Waliopo kuelekea 2015, Membe Mr. Kuchekacheka, Magufuli Mr. Kumbukumbu za urefu wa mabarabara. Sitta Mr. Speed and Standards, Mwakyembe Mr. Misifa, EL ni Mass Mobilizer for economic develpment, etc etc, kutegemeana tunataka nini, tunachagua tunachotaka!.
  6. 2014 atakitumia vizuri kumobilize vijana wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura jambo ambalo ni very crucial kwa mustakabali wa taifa letu!.
  7. 2015 atamobilize watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura kumchagua mgombea wa chama chake!, with politics you may never know atakuwa chama gani, hivyo he could be the only hope kwa kupatikana kwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania na kutimia kwa lile neno la rais wa 2015, lazima atoke Kaskazini!.
  8. Rais wa Kweli wa Tanzania kwa mwaka 2015, sio mwingine yoyote bali ni yule tuu Mungu aliyempangia na aliye muandikia, lililopangwa na Mungu, bunadamu hawezi kulipangua hata watu mseme vipi, Mungu ni Mungu na tuache Mungu aitwe Mungu!.
  9. Uzuri wa Mungu kuna vitu anaviona binadamu hatuvioni, ndia maana aliwahi kumwambia mtu fulani "Wewe ni Mwamba!, Juu ya Mwamba Huu, nitalijenga Kanisa Langu!. Tayari maneno hayo kuna mtu ameisha ambiwa, ila ameambia "Wewe ni Mwamba na Juu ya Mwamba huu, Nitalijenga Taifa Langu!.
  10. Na mwisho, alilolipanga Mungu ndilo liwalo, na huweza kuyafanya yale ambayo kwa binadamu hayawezekani kama alipowaambia makutano "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!". Subirieni 2015 kutimia kwa maneno ya unabii huu, 2015 TB Joshua atautangaza rasmi!.
Merry X-Mass
Pasco.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom