Kuna kila dalili kuwa uanzishaji wa mahakama ya mafisadi aliyoahidi Dr Magufuli utakwama.
Sababu kubwa inayotajwa wachambuzi wa mambo Serkalini ni LOWASSA.
Kwa mujibu wa maoni hayo, Magufuli alikuja na wazo hilo, au tuseme ndoto hiyo, kutokana na hofu na chuki ya kisasi, aliyoijenga juu ya mshindani wake huyo katika uchaguzi uliopita, ambapo Aliapa "KULALA NAYE MBELE".
Hata hivyo baada ya kuingia Ikulu na kujua uhalisia wa mambo, Kwamba tuhuma za Mheshimiwa Lowassa ni ngumu Sana kuzithibitisha, ari na morali ya kusukuma uanzishwaji wa mahakama hiyo imeshuka Sana kama si kufa kabisa.
Lakini pia, maoni yanaendelea zaidi, imethibitika upo ugumu wa kumshtaki Lowassa bila ya kumuunganisha aliyekuwa Mkuu wa Nchi Mheshimiwa Kikwete na maafisa wengi waandamizi wa serikali yake. Na kama hilo likitokea na kwa jinsi, mchakato wenyewe ulivyokwenda, toka hatua za kisekta hadi Baraza la Mawaziri, madhara yake yatakuwa makubwa kwa uongozi huo wa awamu ya nne na kwa chama tawala.
Yetu ni macho na masikio, Lakini tunaisubiri mahakama hii kwa hamu!.