Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Lowassa atumia muda mfupi kuumaliza upinzani ndio maneno mafupi unayoweza kuyatumia. Ni kama vile mbwa anavyomfuata chatu huku akilalamika kujiandaa kumezwa ndicho kinachoendelea kwa sasa. Kwani 'wanaomezwa' hawamjui adui yao, wao wanazidi kujipeleka huku wakichukiana wenyewe kwa wenyewe.
Katika kipindi cha mwaka mmoja alichokaa upinzani amefanikiwa kusambaratisha kitu kilichoitwa ukawa bila kujulikana kama yeye ndiye chanzo. Anatengeneza kitanzi anampa Mbowe amtundike Seif yeye anakaa mbali akishuhudia maangamizi bila ya kutambulika,sasa CUF taabani hawajui wanalosimamia, walitangaza kutoshiriki chaguzi zozote huku Chadema wakitumia mwanya huo kusimamisha wagombea kwa mwamvuli wa ukawa japo Prof.Lipumba kashitukia uhuni huo.
Huku akiunda safu yake ndani ya chadema anahakikisha akina Mbowe hawakai ofisini, anawapa safari za ughaibuni huku akijipanga kwenye chaguzi za uongozi wa majimbo chadema. Ni wazi wanazi wa chadema hawazungumzi lolote wametengwa huku wasijue la kufanya na mengi yataonekana kuelekea uchaguzi wa chama. Licha ya Ben Saanane kutuliwa msaidizi binafsi wa Mbowe amejikuta hana kazi ya kufanya zaidi ya kununua magazeti,kutengeneza chai na kukaribisha wageni kwani mambo yote ya kimkakati hufanywa ofisi za mikocheni. Hii tunaita kifo cha kimya kimya,Hakuna kelele.Tutashuhudia mengi sana.