Lowassa katoa wapi milioni 60?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,442
54,993
1.Naunga mkono moyo wa huruma na imani wa waziri mkuu katika kuchangia shughuli za maendeleo.

2.Milioni 60 ni fedha nyingi sana haiyumkini kwa mwanasiasa wa Tanzania kuwa na kiasi hicho cha fedha.

3.Lowassa ametoa wapi fedha hizo?

habari hii hapa chini imetolewa na magazeti ya ipp:

Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, Mufti Mkuu Sheikh Simba alisema alipokea taarifa kutoka kwa Waziri Mkuu kwamba hatoweza kufika kutokana na udhuru.

Alisema kuwa hatoweza kufika lakini kwa kuwa alifahamu lengo la hafla hiyo, aliahidi kuchangia Sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi huo kwa vile shule hiyo ni muhimu katika kuwaendeleza vijana kimichezo.

”Nimetoa Sh. milioni 60 kuonyesha kuwa nipo nanyi katika hafla hii na ninaahidi kuhudhuria inafuatia,” alimnukuu Waziri Mkuu.

Aidha, Mufti Simba alisema kuwa Bw. Lowassa alisema mchango huo ni mwanzo tu na kwamba ataendelea kuchangia maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo. Aidha Bw. Lowassa aliwataka watu wengine kuchangia kwa hali na mali ujenzi huo.
 
PM wa sasa alianza wizi mapema hata marehemu JKN alisema kwamba ni mchafu mno lakini sasa ndiye PM wetu na yuko na Mzee wa kasi . hapo kuna mengi sana mbali na msaada wa pesa ambayo hatuji EL kaipata wapi .Inawezekana ni pesa toka serikalini .Maana kuna hoja ya kuwa na Mahakama najua hii ni ndoto na sasa Mkristo anaweza kutumiwa kwa njia kwamba hapingi lakini Watanzania hawataki ila watachangia maendeleo ya namna hiyo .mahela haya ni mengi kama kweli katoa mfukoni mwake basi sioni haja ya kwenda kuomba pesa nje wakati wako watu kama yeye they can do more kuliendeleza Taifa . Iko kazi sana na Siasa za uchwara .
 
Lakini je Lowasa hana hizo milioni 60?
maana kwa standards za kiafrica jamaa pesa anazo na najua credit rating yake sio mbaya kupata mikopo

labda kuna jingine tusilolijua
 
Msanga acha hizo masihara.
Tony blair hajawahi kutoa pesa kama hizo.
kumbuka Sokoine kafa na suti pea nne tu. sasa ilikuwaje kwenye kampeni kusema tutayaenzi ya awamu ya kwanza,?
kwani MWL hakuwa na sera ya kujilimbikizia mali.
pia ina maana uongozi hivi sasa ni umilionea? imagine ametoa pesa hizo bila yeye kuhudhuria na wala hajui huo mradi una ukweli kiasi gani?
tizama akina mzee kawawa wanavyoishi kwa taabu. mtizame Jumbe Abood Mwinyi, fuatilia maisha ya familia ya marehemu DR. Omari ALI JUMA jinsi wanavyoishi kwa dhiki hawa hawakuwa wajinga walifuata miiko ya uongozi.
kwa mtaji huu hata akina sisi nasi itabidi tukagombee ili tuwe mabilionea.
 
Mzee Es
kuna maswali ya Lowasa katoa wapi mapesa ya kuhonga na kufanya kampeni mapema kabla a muda .je unaweza kusema anazitoa ama alisha iba siku nyinngi na sasa anaanza kuzigawa ili apate kura na waislam maana alisha anza na kanisa lake si mara moja sasa anahamia huko il kublance maneno ama vipi ? Hebu tupe mwanga kazipata wapi kwa tetesi tu na nini malengo yake ?
 
Kanisani kwao huko Monduli alitoa milioni 35. Akasema marafiki zake wamechanga kama sikosei!

Ila sidhani kama anafanya kampni za urais mwaka 2010 bali ni za 2015. Lakini ninadhani wakati huo hatapata wajue si wao tu!!?


Ziara zake pia ni nzuri kuwaamusha wakurugenzi na wakuu wa wilaya ila tu mimi niliona AMAEZIDISHA ZA ARUSHA NA HUYO NI UKWELI.


ILA HATA MIMI NINAMUUNGA MKONO KUZUNGUKA MIKOANI NA WILAYANI MAANA HAO WAKUU WA MIKIO NA WILYA WAMEKUA MIUNGU WATU KWA MUDA MREFU.iLA IWE KWA SPEED YA MAENDELEO NA MENGINE ATAPEWA TU BAADAYE BAADA YA MATOKEO MAZURI YA KAZI!

CHA AJABU KUNA TAABU NYINGI SANA HAKUNA MADAWATI ETC, SASA HIZI HELA ZA MAKANISANI NA MISIKITINI NI ZA NINI?

60+35=95 HIZO KAMA ZINGETUMIKA KUNUNUA MADAWATI INGEKUWA SUPERB!
 
Hapa Michigan tuna watu wanagombea Ugavana wa Jimbo.. mmojawapo wa wagombea wa Republican Dick Devos, yeye kasema akichaguliwa yuko tayari kufanya kazi bure (bila kulipwa) kwani jamaa ni bilionea... then nikajiuliza je Tanzania kuna kiongozi yoyote anayeweza kusema kitu kama hicho...!! Labda Lowassa?!! ama?
 
MwanaK,

Hiyo itakuwa ndoto, maana waTz huwa tunajisahau na wealth accumulation as if tutakwenda nazo kaburini. Unajua concept ya philanthropist sio lazima uwe milionea but its more of making a difference to other people's lives. For our leaders I don't see that in the near future!
 
Mzee Mwanakijiji said:
Hapa Michigan tuna watu wanagombea Ugavana wa Jimbo.. mmojawapo wa wagombea wa Republican Dick Devos, yeye kasema akichaguliwa yuko tayari kufanya kazi bure (bila kulipwa) kwani jamaa ni bilionea... then nikajiuliza je Tanzania kuna kiongozi yoyote anayeweza kusema kitu kama hicho...!! Labda Lowassa?!! ama?

Kwa Tanzania mmmh, I doubt it.

Ilinigusa tu pale IGP Mwema alipotolea nje marupurupu na nyongeza ya mshahara wake hadi hapo jeshi zima la Polisi kuanzia ngazi ya chini litakapojumuishwa katika zoezi hilo!
Ref: http://darhotwire.com/dar/Habari/2006/05/11/19040.html
 
Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat?

Wazee bado niko nje ya nchi, lakini hii inapaswa kuwa a "CONCERN", maana hata ma-billionnea Mkapa na Sumaye hawajawahi kutoa kititta kizito hivyo,

lakini nilisema huko nyuma kuwa huyu mzee anamtuma tuma agent wake kukusanya hisa na mapesa kwa wahindi, lakini hili kwangu jipya, lakini kama kawaida nikirejea na kuzipata nitaziweka hapa hapa, ingawaje siku hizi hapa pamejaa manjago ile mbaya, majuzi nulikutana na "Kigogo" mmoja wa nchi akiwa na print-out kibao za hii forum!
 
Halafu waambie tuna mpango wa kuweka summary kisha tunapeleka kwenye magazeti yoote TZ, gazeti litakalotaka lichunguze lichapishe lisilotaka liweke kapuni.

Hapo ndio watakoma!

FD
 
Ninavyoelewa mimi ni kuwa hawa viongozi wote wa kubwa hizi pesa sio zao binafsi bali huwa wana kasma yao wanayopewa na serikali na huwa ni juu yao hizo pesa kuzitoa wapi,sio kwenye harusi au misiba,lakini kwenye issue za maendeleo kama hivyo.Hata kwenye makampuni makubwa kuna kitu kama hicho,nakumbuka zamani siku moja nilikwenda Tanzania Breweries,na pale kuna mkurugenzi mmoja nilimkuta akitoa msaada wa pesa kwa vijana flani hivi,nikamuuliza mbona ametoa pesa nyingi kiurahisi hivyo,akaniambia zinatoka kwenye kasma yake.
Hata rais anayo,huko nyuma tumesikia sana vitu kama hivi lakini not in this magnitude,sasa yawezekana kasma ya uongozi huu ni kubwa zaidi.Hata juzi hapa tulisikia rais akitoa pesa kuwapa Taifa Stars,ni utaratibu huohuo.
 
sasa kama hilo ni kweli mbona balozi zetu hazina fungu la kutoa misaada kama hiyo kwa Watanzania wanaopata matatizo nje ya nchi? Fedha wanazotoa viongozi kama rambirambi kwenye misiba huwa zinatoka fungu gani?
 
Shaloom wanabodi,

Mie sipati tabu saaana kusikia EL atoa kiasi hicho cha fedha kama mchango wake kwa shughuli za maendeleo ya jamii.

Ikiwa yeye alishakuwa bilionea toka enzi za uhai wa JKN, hadi wakakodi lidege pamoja na swahiba wake JK, kuzungusha fomu mikoani, sembuse enzi za BWM alivuna hasa, je sasa si ndo hana pakuzipeleka? zaidi ya kutafuta umaarufu?

Nikifanya tathmini ya kwamba serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, na kwakuwa wanakomba ruzuku ya mamilioni just for a month, achilia mbali michango inayotumwa na wafanyabiashara kwa kujipendekeza! sorry. Hivi mwajua JK ametaifisha mali/hela za baadhi ya vigogo waliobanwa wakati wa kampeni ya kupambana na ujambazi? Hizo hela zipo wapi? Hii inamaanisha kwamba EL anapewa kasma na serikali na ndivyo protocol zilivyo, yes sometimes anatoa mfukoni mwake.

.......................................
:U Can't Change The Nature:
 
basi ielezwe kwamba fedha hizo zimetolewa na ofisi ya waziri mkuu kutokana na kasma iliyopewa na bunge/hazina/serikali.
 
Huyu mbona kaanza kampeni mapema sana,hata Sumaye alikua hivyo hivyo,kuchangia makanisani na misikitini,kufanya ziara kibao mikoani,kuwalubuni wakuu wa wilaya,ila alifilisika kisiasa mara moja.Kwa hiyo hata huyu mmaasai acheni apitishe muda wake,tutakuja kumbwaga vibaya sana,EL ni dikteta kasro bunduki.
 
Kwa Tanzania mmmh, I doubt it.

Ilinigusa tu pale IGP Mwema alipotolea nje marupurupu na nyongeza ya mshahara wake hadi hapo jeshi zima la Polisi kuanzia ngazi ya chini litakapojumuishwa katika zoezi hilo!
Ref: http://darhotwire.com/dar/Habari/2006/05/11/19040.html

Kwakweli kuna watu wanahuruma kiasi kwamba kama tungepata watu wa jinsi hii kama kumi hivi ilikuwa tosha wakaunda hata baraza la mawaziri tukaweza kupata maendeleo kuliko kundi hili la wasiokuwa waaminifu. Hata hivyo kama wazalendo halisi lengo letu liwe ni kuhakikisha 2010 hawapati nafasi kirahisi namna hiyo.
 
Hizo pesa zimetolewa na ofisi ya waziri mkuu na ninavyojua mimi zinakuwa zimo kwenye budget ya ofisi yake kwa ajili ya mipango ya maendeleo.

Hizo sio pesa za Lowassa kutoka mfukoni mwake. Inatakiwa waseme ofisi ya rais au ofisi ya waziri mkuu, lakini bahati mbaya wao wanasema Lowassa katoa, au JK katoa.
 
Back
Top Bottom