1.Naunga mkono moyo wa huruma na imani wa waziri mkuu katika kuchangia shughuli za maendeleo.
2.Milioni 60 ni fedha nyingi sana haiyumkini kwa mwanasiasa wa Tanzania kuwa na kiasi hicho cha fedha.
3.Lowassa ametoa wapi fedha hizo?
habari hii hapa chini imetolewa na magazeti ya ipp:
2.Milioni 60 ni fedha nyingi sana haiyumkini kwa mwanasiasa wa Tanzania kuwa na kiasi hicho cha fedha.
3.Lowassa ametoa wapi fedha hizo?
habari hii hapa chini imetolewa na magazeti ya ipp:
Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, Mufti Mkuu Sheikh Simba alisema alipokea taarifa kutoka kwa Waziri Mkuu kwamba hatoweza kufika kutokana na udhuru.
Alisema kuwa hatoweza kufika lakini kwa kuwa alifahamu lengo la hafla hiyo, aliahidi kuchangia Sh. milioni 60 kwa ajili ya ujenzi huo kwa vile shule hiyo ni muhimu katika kuwaendeleza vijana kimichezo.
Nimetoa Sh. milioni 60 kuonyesha kuwa nipo nanyi katika hafla hii na ninaahidi kuhudhuria inafuatia, alimnukuu Waziri Mkuu.
Aidha, Mufti Simba alisema kuwa Bw. Lowassa alisema mchango huo ni mwanzo tu na kwamba ataendelea kuchangia maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo. Aidha Bw. Lowassa aliwataka watu wengine kuchangia kwa hali na mali ujenzi huo.