Lowassa katika maandalizi ya Urais wa Tanzania 2015?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
543
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Ngoyai Lowassa yuko kwenye maandalizi ya kuukwaa Urais wa Tanzania 2015.

Hii inadhihirishwa na nguvu kubwa aliyotumia kuhakikisha CCM inshinda udiwani Makuyuni_Monduli kwa mbinu yoyote ile ili kumhakikishia JK umaarufu wake kama alivyoahidi kwenye vikao vya CCM. Kule Makuyuni kumetokea vurugu zilizosababisha Mbunge wa Chadema Joshua Nasari kujeruhiwa.

Monduli si kwamba hakuna upinzani ila Lowassa amekuwa akiandaa magenge ya kihuni na kuwapa fedha ili kudhibiti wapinzani wa CCM na hata wapinzani wake ndani ya CCM. Sasa huyu ndiye Mtu anayetegemewa kugombea Urais kupitia CCM. Huyu Mtu hafai kabisa ni Mtu wa visasi na hapendi kukosolewa.

Ushahidi ni wapinzani wake ndani ya CCM-Monduli amewahujumu hadi basi, kwa kifupi Mtu kama huyu akichukua nchi ni afadhali ya Iddi Amini wa Uganda.

Angalia alipokuwa Waziri Mkuu alivyokuwa anatumia madaraka vibaya na kupelekea hata kukiuka sheria an hatimae dhambi ikamfikisha kwenye arobaini kwenye sakata la Richmond (Richard Monduli).

Anajifanya anapenda elimu lakini ni unafiki kwani huku Monduli hataki wasomi maana hataki kukosolewa wengi wa washabiki wake wanaelimu ndogo na wachache wenye elimu ni wale wa ndio-mzee.

Nawasilisha kwa uchambuzi zaidi. Mungu atuepushe na watu wanaojivika ngozi ya kondoo wakati ni chui.
 
Hata kama tapitishwa ili mradi ni miongoni mwa watu ambao Nyererealitoa wosia na mashaka yake katika kuwapa uongozinadhani anatutafutia laana ya kwenda kinyume cha wosia wa Muasisi wa taifa. Ebu angalia majanga ambayo pacha wake anatuletea kwa vipindi hivi viwili, Ufisadi wa kupindukia, Udini wa dhahiri, Mauaji ya viongozi wa dini, utekwaji wa watua maarufu, mauaji kwenye mikutano ya siasa na hasa CHADEMA,Wizi wa raslimali za taifa mpaka Twiga alama ya Taifa vinapelekwa Uarabuni, Gesi ya Mtwara na mauaji ya raia wasio hatia yoyote, Madini kuchukuliwa na bila kuchangia hata kwenye bajeti ya serikali, Madawa ya kulenya na wengine kukamatiwa uchina, biashara ya meno ya tembo. Fedha za EPA, Meremeta, Deep Green nk.

Haya tumwachie Mungu, Ninachojuafimbo ya Munguitawachapa hapa hapa na muda si mrefu

Ni kwenye CCM tu ndo mtu najitokeza mwenyewe na kujipigia debe kwamba atafaa. Lakini pote Ulimwenguni Kiongozi anatafutwa kwa njia za kidemokrasia na anaombwa kuwa yeye anaweza kuongoza chma fulani. Tunamshukuru Mungu J.K alithibitishia UMMA kwamba harakati zake alizianza kwa karibu miaka kumi na kuunda kile kilichoitwa mtandao. Wote mmeshuhudia ufisadi, matumizi mabovu ya raslimali za taifa, wizi wa fedha za UMMA kwa mujibu wa CAG, kuuzwa na kugawiwa wageni ardhi na raslimali za asili wote mnajua kinachoendelea Mtwara, Uranium Namtumbo, Makaa ya Mawe kwenye kijiji cha Mtunduwalowananchi hata hawajapewa fidia lakini mwekezaji anapiga kazi kama kawa. Lowasa atulie tu, fimbo ya Mungu ikiamua kupiga hakuna atakayestahimili.
 
Hata kama tapitishwa ili mradi ni miongoni mwa watu ambao Nyererealitoa wosia na mashaka yake katika kuwapa uongozinadhani anatutafutia laana ya kwenda kinyume cha wosia wa Muasisi wa taifa. Ebu angalia majanga ambayo pacha wake anatuletea kwa vipindi hivi viwili, Ufisadi wa kupindukia, Udini wa dhahiri, Mauaji ya viongozi wa dini, utekwaji wa watua maarufu, mauaji kwenye mikutano ya siasa na hasa CHADEMA,Wizi wa raslimali za taifa mpaka Twiga alama ya Taifa vinapelekwa Uarabuni, Gesi ya Mtwara na mauaji ya raia wasio hatia yoyote, Madini kuchukuliwa na bila kuchangia hata kwenye bajeti ya serikali, Madawa ya kulenya na wengine kukamatiwa uchina, biashara ya meno ya tembo. Fedha za EPA, Meremeta, Deep Green nk.

Haya tumwachie Mungu, Ninachojuafimbo ya Munguitawachapa hapa hapa na muda si mrefu

mbona serikali tatu mnazishangilia japo Mwl Nyerere alizipinga mara zote na kwa nguvu zake zote,alimvua Mzee Jumbe madaraka kwa kutaka serikal tatu 1983, Mzee Malecela alivuliwa u PM kwa kuunga mkono G55 juu ya Azimio la kuirejesha Tanganyika1993!
 
yah kuna maali anakosea sana kipindi hiki cha uchaguzi amemwamuru DED kuwasimamisha watumishi 6 wa serikali ambao wapo kata husika na wengine kata za jirani akihofia hawamuungi mkono na DED bila kutafakari akawapa barua za kuwasimamisha hadi uchaguzi upite its not fear kwa kweli, hana washauri wengi ni wapambe na waganga njaa hasa madiwani wawili vijana na katibu tarafa mmoja ndo wanamwaribu kabisa na elimu zao ndo zilee yaani hamna kitu.
 
Kamanda nakubaliana na wewe, ebu waliokaribu wafuatilie elimu ya hao vihiyo anaowatumia. Ila kwa ujumla Lowassa anawahadaa tuu wasiomfahamu lakini kwa ukweli hafai kuwa Kiongozi bora. Ukifuatilia matamko yake yote anaongelea vitu ambavyo angeweza kuvifanya alipokuwa waziri mkuu lakini wakati alikuwa bize na dili la Richmond eti sasa ndio anatuhadaa kwamba ana ndoto hii na ile ni unafiki mtu wala haoni aibu Mungu na Baba wa Taifa letu waendelee kumlaani asiwadanganye Watanzania.
 
Back
Top Bottom