Uchaguzi 2020 Lowassa: Huko kina Lissu wameanza kujipambanua kwa sera, fujofujo mpaka matv mengine yanatisha. Rais wetu usitishike

CCMkuelekeaUchaguzi

Senior Member
Aug 18, 2015
179
77
Waziri mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwa Monduli kwenye kikao cha chama cha mapinduzi ambapo mwanae Fred Lowassa anawania jimbo hilo, alipata fursa ya kuongea na kumuelezea Dkt. Magufuli aliyoyafanya katika vita dhidi ya Korona. Pia kwenye kikao hicho alikuwepo Mizengo Pinda.

Lowassa: Mimi sina mashaka juu ya kushinda, mashaka yangu atapita kwa kura ngapi. Huko kwa kina Lissu wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo zile, wanaonekana kwenye mamitaa, matv, matv mengine yanatisha tisha lakini tulimwambia Rais wetu usitishike hata kidogo.

Umma wa watanzania uko nyuma yako na dunia inajua kwamba kuna mwanaume Tanzania. Nasema hivyo kwa sababu, Australia kama ulisikiliza BBC leo, Rais anajiuzulu, kule Bolivia Rais anajiuzulu yote kwa sababu ya hii kitu, Corona si mchezo.

Nyinyi mtu wenu tena mtu mweusi hana nguvu za kimitume anakwenda anawaambia Taifa lake, jamani tumuendee mwenyezi, tumuombe atusaidie tuondokane na hili janga. Watu wa ajabu, wakasema huyu anababaisha tu. Anababaisha? Imepita wiki mbili, tatu hamna korona.

 
Huo umma anao uzungumzia ni upi, labda hao hao walio kwenye mzunguko wao wa kuneemeka na Madaraka ya uwepo wa CCM Mamlakani.Wananchi wa kawaida tunaisomba Namba vilivyo.

Mwishoni sija muelewa ,mifano aliyo itoa ni kama amechanganya mafaili.
 
Huo umma anao uzungumzia ni upi ,labda hao hao walio kwenye mzunguko wao wa kuneemeka na Madaraka ya uwepo wa CCM Mamlakani.Wananchi wa kawaida tunaisomba Namba vilivyo.

Mwishoni sija muelewa ,mifano aliyo itoa ni kama amechanganya mafaili.
Ameshakuwa mzee akili imerudi utotoni, anachozungumza hata hakieleweki
 
Back
Top Bottom