Quote toka Gazeti la Tanzania Daima
Lowassa achimbwa
na Mwandishi Wetu
SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.
Katika kile kinachoonyesha kuwa ni jitihada za kundi la mahasimu wake kisiasa kuanza kudodosa mambo yanayomhusu Lowassa, baadhi ya siri zilizokuwa hazijawekwa bayana kwa miaka kadhaa tangu akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, sasa zimeanza kuvujishwa kwa vyombo vya habari.
Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili hivi karibuni, zinaeleza kuwa, Lowassa alitumia nafasi yake ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, ya uwaziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo kununua eneo kubwa la Ranchi ya Taifa ya Mifugo ya Mzeri, iliyoko wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Zinaeleza kuwa Lowassa anamiliki kitalu namba 645/5, huku majina ya watu wanaoonekana kuwa wamiliki halali wakiwa ni wengine, jambo linalotia shaka.
Taarifa zinaeleza kuwa maelezo ya wamiliki wa kampuni hiyo yaliyoko kwa Msajili wa Makampuni (BRELA) na yaliyo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), yanaonyesha kuwa Kampuni ya Olospa, ndiyo mmiliki wa ranchi hiyo.
Baadhi ya viongozi wa NARCO waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, wakati ranchi hiyo ikiuzwa kwa Kampuni ya Olospa, kitalu namba 645/5, hawakujua kama ilikuwa na uhusiano wowote na Lowassa.
Kwamba baada ya kuanza kuibuka kwa tetesi kuwa ranchi hiyo ni mali ya Lowassa, walianza kuwa na wasiwasi kuwa inawezekana hakuweka wazi uhusiano aliokuwa nao na kampuni hiyo kutokana na wadhifa aliokuwa nao wakati huo.
Ni kweli imebainika kuwa Lowassa anamiliki block namba 645/5, na amekuwa akionekana huko mara kwa mara, lakini sisi hatukujua lolote wakati wa zoezi la kumilikisha maeneo hayo, alisema Mshauri Mkuu wa NARCO, Fabian Shempemba, ambaye wakati wa uuzaji wa ranchi hizo alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo.
Alisema taratibu zilizokuwepo za kumilikisha ranchi ndogo za kibiashara kwa wafugaji wadogo, ziliipa madaraka ya kufanya maamuzi ya mwisho iliyokuwa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakati huo ikiwa chini ya Lowassa.
Baada ya kukubaliwa na serikali mwaka 2002, kwamba ranchi za taifa zigawanywe vipande vidogo vidogo vya kibiashara na kumilikishwa Watanzania, NARCO tulipewa jukumu la kutangaza na kupokea maombi.
Baadaye Bodi ya NARCO iliwasilisha mapendekezo yake wizarani kuhusu nani anafaa na nani hafai kumilikishwa ranchi hizo ndogo ndogo, halafu wizara ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuamua wamiliki, alisema Shempemba.
Shaka inayoelezwa hapa ni uwezekano wa Lowassa kuamua kununua ranchi hiyo kupitia Kampuni ya Olospa kwa sababu hakutaka kwa wadhifa aliokuwa nao kuhusika kwa namna yoyote na ununuzi wa ranchi.
Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua.
Kwani kuna makosa yoyote mimi kununua hiyo ranchi? Sikiliza wee , wewe si ndiye uliyekwenda kwanza Wizara ya Mifugo kuhoji habari hizi wiki iliyopita?
Sasa si vizuri kuzungumza haya mambo kwenye simu, nisubiri Dar es Salaam, nitarudi baada ya wiki moja, kwa sasa nipo safarini Monduli.
Lakini njoo ukijua kuwa hiyo ilikuwa ni sera ya taifa ya kuzigawanya ranchi za taifa na mashamba makubwa ya mifugo ya umma, katika vipande vidogo vidogo na kuwamilikisha Watanzania wenye uwezo wa kufuga kisasa na kibiashara, alisema Lowassa.
Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kama alivyoahidi ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo na lilipompata kupitia simu yake ya kiganjaini alieleza kuwa atatoa ufafanuzi huo wiki ijayo.
Nipo njiani narudi Dar es Salaam, nakuomba unipigie Jumatatu nitakuambia tukutane wapi ili tuongee kwa kina suala hilo, na ningependa uje na mhariri wako, alisema Lowassa.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa, Kampuni ya Olospa ilisajiliwa Julai 31, 1992, chini ya wakurugenzi wanawake watatu.
Taarifa zilizoko BRELA zinaonyesha kuwa wakurugenzi hao ni Ruth Mollel, Nengai Kingori Mollel na Olomutai Mollel.
Jina kamili la biashara la kampuni hiyo lililosajiliwa BRELA ni Olosipa Printers and Stationers Limited, ambayo ni kampuni inayofanya biashara za uchapishaji na uuzaji wa vifaa vya ofisini.
Shughuli za kampuni hiyo zinapingana na shughuli za biashara ya ranchi (kufuga na kuuza mazao ya mifugo), jambo ambalo linatia wingu zaidi la mashaka kuhusu kampuni hiyo kuuziwa ranchi hiyo.
Uamuzi wa kuzigawa ranchi za taifa katika vipande vidogo vya kibiashara na kuzimilikisha kwa Watanzania wazalendo, ulifikiwa na serikali mwaka 2002, na utekelezaji ulianzia kwa Ranchi ya Mkata (Morogoro), na kufuatiwa na ranchi ya Mzeri iliyogawanywa vipande 9, ambapo kipande kimoja (Block 645/5) ndicho kinachomilikiwa na Olosipa.