Lowassa- Hii sio conflict of Interest tu-ni Ufisadi!

Mnyoofu

Senior Member
Feb 24, 2008
153
49
Quote toka Gazeti la Tanzania Daima

Lowassa achimbwa

na Mwandishi Wetu

SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.

Katika kile kinachoonyesha kuwa ni jitihada za kundi la mahasimu wake kisiasa kuanza kudodosa mambo yanayomhusu Lowassa, baadhi ya siri zilizokuwa hazijawekwa bayana kwa miaka kadhaa tangu akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, sasa zimeanza kuvujishwa kwa vyombo vya habari.

Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili hivi karibuni, zinaeleza kuwa, Lowassa alitumia nafasi yake ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, ya uwaziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo kununua eneo kubwa la Ranchi ya Taifa ya Mifugo ya Mzeri, iliyoko wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Zinaeleza kuwa Lowassa anamiliki kitalu namba 645/5, huku majina ya watu wanaoonekana kuwa wamiliki halali wakiwa ni wengine, jambo linalotia shaka.

Taarifa zinaeleza kuwa maelezo ya wamiliki wa kampuni hiyo yaliyoko kwa Msajili wa Makampuni (BRELA) na yaliyo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), yanaonyesha kuwa Kampuni ya Olospa, ndiyo mmiliki wa ranchi hiyo.

Baadhi ya viongozi wa NARCO waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, wakati ranchi hiyo ikiuzwa kwa Kampuni ya Olospa, kitalu namba 645/5, hawakujua kama ilikuwa na uhusiano wowote na Lowassa.

Kwamba baada ya kuanza kuibuka kwa tetesi kuwa ranchi hiyo ni mali ya Lowassa, walianza kuwa na wasiwasi kuwa inawezekana hakuweka wazi uhusiano aliokuwa nao na kampuni hiyo kutokana na wadhifa aliokuwa nao wakati huo.

“Ni kweli imebainika kuwa Lowassa anamiliki block namba 645/5, na amekuwa akionekana huko mara kwa mara, lakini sisi hatukujua lolote wakati wa zoezi la kumilikisha maeneo hayo,” alisema Mshauri Mkuu wa NARCO, Fabian Shempemba, ambaye wakati wa uuzaji wa ranchi hizo alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo.

Alisema taratibu zilizokuwepo za kumilikisha ranchi ndogo za kibiashara kwa wafugaji wadogo, ziliipa madaraka ya kufanya maamuzi ya mwisho iliyokuwa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakati huo ikiwa chini ya Lowassa.

“Baada ya kukubaliwa na serikali mwaka 2002, kwamba ranchi za taifa zigawanywe vipande vidogo vidogo vya kibiashara na kumilikishwa Watanzania, NARCO tulipewa jukumu la kutangaza na kupokea maombi.

“Baadaye Bodi ya NARCO iliwasilisha mapendekezo yake wizarani kuhusu nani anafaa na nani hafai kumilikishwa ranchi hizo ndogo ndogo, halafu wizara ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuamua wamiliki,” alisema Shempemba.

Shaka inayoelezwa hapa ni uwezekano wa Lowassa kuamua kununua ranchi hiyo kupitia Kampuni ya Olospa kwa sababu hakutaka kwa wadhifa aliokuwa nao kuhusika kwa namna yoyote na ununuzi wa ranchi.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua.

“Kwani kuna makosa yoyote mimi kununua hiyo ranchi? Sikiliza wee ……, wewe si ndiye uliyekwenda kwanza Wizara ya Mifugo kuhoji habari hizi wiki iliyopita?

“Sasa si vizuri kuzungumza haya mambo kwenye simu, nisubiri Dar es Salaam, nitarudi baada ya wiki moja, kwa sasa nipo safarini Monduli.

“Lakini njoo ukijua kuwa hiyo ilikuwa ni sera ya taifa ya kuzigawanya ranchi za taifa na mashamba makubwa ya mifugo ya umma, katika vipande vidogo vidogo na kuwamilikisha Watanzania wenye uwezo wa kufuga kisasa na kibiashara,” alisema Lowassa.

Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kama alivyoahidi ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo na lilipompata kupitia simu yake ya kiganjaini alieleza kuwa atatoa ufafanuzi huo wiki ijayo.

“Nipo njiani narudi Dar es Salaam, nakuomba unipigie Jumatatu nitakuambia tukutane wapi ili tuongee kwa kina suala hilo, na ningependa uje na mhariri wako,” alisema Lowassa.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa, Kampuni ya Olospa ilisajiliwa Julai 31, 1992, chini ya wakurugenzi wanawake watatu.

Taarifa zilizoko BRELA zinaonyesha kuwa wakurugenzi hao ni Ruth Mollel, Nengai King’ori Mollel na Olomutai Mollel.

Jina kamili la biashara la kampuni hiyo lililosajiliwa BRELA ni Olosipa Printers and Stationers Limited, ambayo ni kampuni inayofanya biashara za uchapishaji na uuzaji wa vifaa vya ofisini.

Shughuli za kampuni hiyo zinapingana na shughuli za biashara ya ranchi (kufuga na kuuza mazao ya mifugo), jambo ambalo linatia wingu zaidi la mashaka kuhusu kampuni hiyo kuuziwa ranchi hiyo.

Uamuzi wa kuzigawa ranchi za taifa katika vipande vidogo vya kibiashara na kuzimilikisha kwa Watanzania wazalendo, ulifikiwa na serikali mwaka 2002, na utekelezaji ulianzia kwa Ranchi ya Mkata (Morogoro), na kufuatiwa na ranchi ya Mzeri iliyogawanywa vipande 9, ambapo kipande kimoja (Block 645/5) ndicho kinachomilikiwa na Olosipa.
 
MASWALI ZAIDI:

1. Tunapenda kujua Kampuni ya Olosipa imefanya kazi yoyote na serikali kuu au za mikoa au na shirika lolote la umma?

2. Kama ni ndio mikataba yake ni ya ukubwa gani na nani alihusika katika mikataba hiyo?

3. Je Lowassa alitoa idhini yeye mwenyewe kuipatia ranchi hii kampuni au afisa gani alipewa idhini hiyo na Bwana Mkubwa?

4. Huyo ofisa pia yeye aligawiwa nini baada ya "kufacilitate" deal hii?
 
Mnyoofu.

Karibu sana JF. maneno haya kaandika Membe soma thread ya Membe aanza makombora kwa Lowassa hapo juu. hauko peke yako kwenye kibarua hiki yuko Masatu atakusaidia.

gazeti la leo lina makala 16 za lowassa jee ni uandishi huo au makombora ya Joti au bwana kimbelembele, kabla ya kukutuma wewe kimbelembele alikuwa aikiingia mwenyewe humu kwa jina la Mbopo. akala mawe akakimbia.
 
BABA H.
ukitaka kujua kuwa Membe hana akili huyu kijana wake MNYOOFU kajiunga leo hii kwenye JF na gazeti limetoka leo na habari za lowassa. Membe tumia akili acha ujinga.
 
Mtalii,

Umeisoma heading ya thread? au wadandia treni kwa mbele tu? kuna mahala katajwa Membe kwenye hiyo newspaper article?
 
BABA H.
ukitaka kujua kuwa Membe hana akili huyu kijana wake MNYOOFU kajiunga leo hii kwenye JF na gazeti limetoka leo na habari za lowassa. Membe tumia akili acha ujinga.

BABA H na MTALII

Acheni Hegemony! msitake kuua fikira za watu wanaotaka kutoa madukuduku yao na michango yao ya kupambana na ufisadi. Sijitetei, bali sijasoma threads mnazozitaja, na situmiki na mtu, na wala sijaingia leo! soma posting zangu za last week!

Sio busara kuanza kutwangana sisi kwa sisi, lets focus on issues. Labda kama ninyi mnatumika then mtanichoka!

Ndio kwanza ninaamka!

Aluta continua!
 
Wape wape vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao!
 
KAMA WEWE UNA UCHUNGU NA MAFISADI mbona hujachangia chochote juuu ya JEETUL-PATEL? au kwanini usiseme au kuanzisha move ili mkapa Benjamin tumpeleke mahakamani kama Chiluba? tuambie habari ya kiwira huko MKAPA ana hisa asilimia 85 au unajua habari za Lowassa tu?

Nadhani una ajenda yako na Membe. mie napiga mawe kwa Membe na Lowassa kama hunijui pitia michango yangu kwenye mada ya vitambulisho-Membe na Lowassa.

Mtumwa mwenzio anaitwa Masatu kama hamjuani.
 
Utamaliza kashfa zote lakini mwisho wa siku hoja ndio ina count...
 
Mnyoofu.

Gazeti la Tanzania Daima hili hapa chini lina vichwa vya habari 16 vinavyomuhusu Lowasa jee huo ni uandishi wa gazeti? hakuna current issues? kama wewe una fuatilia ufisadi wa Lowassa ungesema mkataba wa memorandum of understand wa mwaka 1992 Ambao una ubaguzi wa hali juu kwa Taifa letu.lakini makala yako na ya Gazeti la Tanzania DAIMA yamekaa katika kujipanga zaidi kuliko maslahi ya Taifa.
soma gazeti zima hapa.
http://www.freemedia.co.tz/daima/
 
...and what has it to do with Minister Membe?
 
kama mtu ana kashfa kwanini madhambi yake yasiwekwe hadharani?wee unayemtetea LOWASSA ina maana hujui UFISADI wake?sisi hatujali kama MEMBE ndio source ya hazo habari,tena kama MEMBE atakuwa ndiye source itakuwa safi sana maana atakuwa anatufungua macho kwa kuuanika UCHAFU wa LOWASSA,hivyo wewe MTALII na vibaraka wenzako kama ninyi ndio mliopenyezwa na LOWASSA ili mumsafishe basi mwambie kuwa 'MAJI YAMEKATIKA',na MAFISADI WOTE WATASHUGHULIKIWA KWA HATUA,AACHWI MTU...MPAKA KIELEWEKE!
 
Mnyoofu na Mtimti.

Sijasema kuwa Lowassa ni smart ila imekuwa too much kama nyinyi mnania ya ukweli na Mafisadi waleteni na kina MKAPA. wewe hujui mama Mkapa kachukua nyumba zote za posta, hujui kama MKAPA rafiki yake ni Jeetul Patel? WAMEKOMBA BENKI KUU.wewe humjui Mramba kama anahusika B.O.T mbona uko kimya? hujui precision Air mali ya Mramba unasemaje? Tulipokuwa tunamtaja Diallo sikuona michango yenu.

naomba tumia dakika chache usome posts zangu humu na ujue unabishana na nani. sisi hapa JF ni nyumbani kwetu sio nyinyi wageni wa thread moja tu. akitajwa MEMBE AU DODO ndio mnakuja kuchangia,hamna uchungu na nchi yetu mafisadi kama MEMBE ambaye hata dada zetu wa kiafrika aliwaona hawana maana akaoa mzungu huu ni ushahidi si mzalendo ni anko Tom tu.

Nakuletea ufisadi wa lowassa soma kitabu hiki kama wewe mkweli na una mapenzi ya nchi yako halafu lete mchango wako.ukiona noma badili jina tena.
http://www.igs.net/~kassim/mwembechai/index.html
 
Mtalii
Hapa watu wana nia ya ukweli kabisa na Mafisa, Sio Lowassa, Mramba,Balalli, Mkapa, Diallo, wote watu wana Hasira nao, Tatizo ni kwamba tunachangia ila uwezo wa kuamua kutekeleza imeachiwa serikali ya Mafisadi kaka, Hivyo hata tukalia na kulia vipi kama mafisadi hawajaamua itakuwa ngumu, na sisi watanzania tunachukulia sawa tu.

Maneno hayo waambie kina Mnyoofu na Mtimti. mimi Lowassa kuna sehemu nyingi nimemuweka wazi.lakini hapa MEMBE analeta ujanja wake.
Membe hajawahi kuandikwa vibaya na Tanzania DAIMA.
 
Quote toka Gazeti la Tanzania Daima

Lowassa achimbwa

na Mwandishi Wetu

SIRI zinazohusu utajiri na mipango ya baadaye ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tisa wa Tanzania, Edward Lowassa, baada ya kuachia wadhifa wake kwa kutajwa katika kashfa ya Kampuni ya Richmond, zimeanza kufichuliwa.

Katika kile kinachoonyesha kuwa ni jitihada za kundi la mahasimu wake kisiasa kuanza kudodosa mambo yanayomhusu Lowassa, baadhi ya siri zilizokuwa hazijawekwa bayana kwa miaka kadhaa tangu akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, sasa zimeanza kuvujishwa kwa vyombo vya habari.

Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima Jumapili hivi karibuni, zinaeleza kuwa, Lowassa alitumia nafasi yake ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, ya uwaziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo kununua eneo kubwa la Ranchi ya Taifa ya Mifugo ya Mzeri, iliyoko wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Zinaeleza kuwa Lowassa anamiliki kitalu namba 645/5, huku majina ya watu wanaoonekana kuwa wamiliki halali wakiwa ni wengine, jambo linalotia shaka.

Taarifa zinaeleza kuwa maelezo ya wamiliki wa kampuni hiyo yaliyoko kwa Msajili wa Makampuni (BRELA) na yaliyo katika Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), yanaonyesha kuwa Kampuni ya Olospa, ndiyo mmiliki wa ranchi hiyo.

Baadhi ya viongozi wa NARCO waliozungumza na gazeti hili walieleza kuwa, wakati ranchi hiyo ikiuzwa kwa Kampuni ya Olospa, kitalu namba 645/5, hawakujua kama ilikuwa na uhusiano wowote na Lowassa.

Kwamba baada ya kuanza kuibuka kwa tetesi kuwa ranchi hiyo ni mali ya Lowassa, walianza kuwa na wasiwasi kuwa inawezekana hakuweka wazi uhusiano aliokuwa nao na kampuni hiyo kutokana na wadhifa aliokuwa nao wakati huo.

“Ni kweli imebainika kuwa Lowassa anamiliki block namba 645/5, na amekuwa akionekana huko mara kwa mara, lakini sisi hatukujua lolote wakati wa zoezi la kumilikisha maeneo hayo,” alisema Mshauri Mkuu wa NARCO, Fabian Shempemba, ambaye wakati wa uuzaji wa ranchi hizo alikuwa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo.

Alisema taratibu zilizokuwepo za kumilikisha ranchi ndogo za kibiashara kwa wafugaji wadogo, ziliipa madaraka ya kufanya maamuzi ya mwisho iliyokuwa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, wakati huo ikiwa chini ya Lowassa.

“Baada ya kukubaliwa na serikali mwaka 2002, kwamba ranchi za taifa zigawanywe vipande vidogo vidogo vya kibiashara na kumilikishwa Watanzania, NARCO tulipewa jukumu la kutangaza na kupokea maombi.

“Baadaye Bodi ya NARCO iliwasilisha mapendekezo yake wizarani kuhusu nani anafaa na nani hafai kumilikishwa ranchi hizo ndogo ndogo, halafu wizara ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kuamua wamiliki,” alisema Shempemba.

Shaka inayoelezwa hapa ni uwezekano wa Lowassa kuamua kununua ranchi hiyo kupitia Kampuni ya Olospa kwa sababu hakutaka kwa wadhifa aliokuwa nao kuhusika kwa namna yoyote na ununuzi wa ranchi.

Aidha, shaka nyingine inayojitokeza ni usiri uliopo kati ya Lowassa na Kampuni ya Olospa inayodaiwa kuwa licha ya kutambuliwa kama mmiliki wa ranchi hiyo na NARCO, jina la Lowassa halimo katika orodha ya wakurugenzi wa kampuni hiyo.

Kwamba katika misingi ya uadilifu wa uongozi, Lowassa alipaswa kutangaza mapema masilahi yake katika Kampuni ya Olospa ili asishirikishwe katika kujadili na kufanya maamuzi juu ya maombi ya kampuni hiyo ya kutaka kumilikishwa ranchi hiyo.

Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita kupitia simu yake ya kiganjani, Lowassa alikiri kumiliki ranchi hiyo na kueleza kwamba haoni kosa lolote kuwa mmiliki wa ranchi hiyo kwa sababu hapakuwa na sheria ya kumzuia kuinunua.

“Kwani kuna makosa yoyote mimi kununua hiyo ranchi? Sikiliza wee ……, wewe si ndiye uliyekwenda kwanza Wizara ya Mifugo kuhoji habari hizi wiki iliyopita?

“Sasa si vizuri kuzungumza haya mambo kwenye simu, nisubiri Dar es Salaam, nitarudi baada ya wiki moja, kwa sasa nipo safarini Monduli.

“Lakini njoo ukijua kuwa hiyo ilikuwa ni sera ya taifa ya kuzigawanya ranchi za taifa na mashamba makubwa ya mifugo ya umma, katika vipande vidogo vidogo na kuwamilikisha Watanzania wenye uwezo wa kufuga kisasa na kibiashara,” alisema Lowassa.

Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kama alivyoahidi ili kutoa ufafanuzi wa madai hayo na lilipompata kupitia simu yake ya kiganjaini alieleza kuwa atatoa ufafanuzi huo wiki ijayo.

“Nipo njiani narudi Dar es Salaam, nakuomba unipigie Jumatatu nitakuambia tukutane wapi ili tuongee kwa kina suala hilo, na ningependa uje na mhariri wako,” alisema Lowassa.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa, Kampuni ya Olospa ilisajiliwa Julai 31, 1992, chini ya wakurugenzi wanawake watatu.

Taarifa zilizoko BRELA zinaonyesha kuwa wakurugenzi hao ni Ruth Mollel, Nengai King’ori Mollel na Olomutai Mollel.

Jina kamili la biashara la kampuni hiyo lililosajiliwa BRELA ni Olosipa Printers and Stationers Limited, ambayo ni kampuni inayofanya biashara za uchapishaji na uuzaji wa vifaa vya ofisini.

Shughuli za kampuni hiyo zinapingana na shughuli za biashara ya ranchi (kufuga na kuuza mazao ya mifugo), jambo ambalo linatia wingu zaidi la mashaka kuhusu kampuni hiyo kuuziwa ranchi hiyo.

Uamuzi wa kuzigawa ranchi za taifa katika vipande vidogo vya kibiashara na kuzimilikisha kwa Watanzania wazalendo, ulifikiwa na serikali mwaka 2002, na utekelezaji ulianzia kwa Ranchi ya Mkata (Morogoro), na kufuatiwa na ranchi ya Mzeri iliyogawanywa vipande 9, ambapo kipande kimoja (Block 645/5) ndicho kinachomilikiwa na Olosipa.

Aliyeandika hii mada leo ni shabiki wa Lowassa kindakindaki!!!!!!!
 
Back
Top Bottom