Lowassa hatojuta akienda UDP ya cheyo

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Tuache uonge, Lowassa, alipokatwa na vikao vya juu vya chama chake (ccm wakati huo) na kuamua kukimbilia Chadema nchi ilitikisika.

Nchi ilitikisika kwa sababu ilikuwa ni Mara ya kwanza Tanzania kushuhudia mtu mzito aliyeshika nafasi ya uwaziri Mkuu kuhama chama tawala na kujiunga na upinzani.

Niseme tena hapa kwamba nakubaliana na wanaoamini kuwa huenda Medeye ametangulia tu UDP na muda mfupi ujao Lowassa anaweza kuingia huko na kuchukua uenyekiti baada ya Medeye kutunukia cheo cha Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kwanini nasema hivyo, nasema hivyo kwa sababu katika siasa hakuna 'mwiko' lolote linaweza linawezekana wakati wowote.

Wengi wanaamini kuhama kwake kunawezakana kutokana na ukweli kwamba thamani yake ndani ya chadema imeshuka.

Ni bora akahama mapema ili kukijenga chama hicho cha UDP ambacho miaka minne ijayo kitakuwa kimeimarika kwa kiwango fulani na yeye kuwa na nafasi ya kutimiza malengo take ya kisiasa.

Kwa kauli ya Mwenyekiti wa UDP cheyo anasema; "UDP ni chama cha wananchi.hatuna ubaguzi wa kabila, rangi au dini. Kama Lowassa anataka kuhamia kwenye chama chetu, anakaribishwa kwa mikono miwili".

Kwa maana hiyo namshauri Lowassa naye kuhamia UDP mapema, kwani hatajutia uamuzi wake, kuliko kuendelea kubaki Chadema ambako hana uhakika wa kufanya siasa kwa fursa anayoitarajia.
 
Back
Top Bottom