Lowassa hajaalikwa kwenye harambee yetu ~ Kanisa Katoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa hajaalikwa kwenye harambee yetu ~ Kanisa Katoliki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Mar 10, 2012.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kanisa katoliki limekanusha kuwa limemwalika waziri mkuu aliyejiuzulu na mbunge wa monduli, Bwana Lowasa katika harambee ya kuchangia kuundwa kwa dayosisi mpya ya ifakara na kumsimika rasmi Mhashamu Askofu salutaris Libena kuwa askofu wa kwanza wa Dayosisi hiyo mpya. akiongea na waandishi wa habari askofu msaidizi wa jimbo kuu la dsm, askofu Nzigilwa alishangaa ni nani alivumisha hizo habari.(HAPA KWENYE JAMVI KULIKUWEPO NA HIZO HABARI)

  Askofu Nzigilwa alitumia muda huu kuelezea kuwa kanisa katoliki haliwaaliki au kuwatumia wanasiasa katika shughuli rasmi za kanisa hilo kwa kuogopa kupakwa matope na wanasiasa wanaoweza kutumia muda huo vibaya. aidha aliwaonya viongozi walei wahakikishe kuwa kabla ya kuwaalika wanasisa makanisani kuwasiliana na uongozi wa juu wa jimbo kuepuka migongano inayoweza kulichafua kanisa.

  mara nyingi viongozi wakisiasa wanaalikwa katika kuchangia shughuli za kikanisa kama vile mashule na hospitali, lakini si kwa shughuli zinzohusu uendeshaji wa moja kwa moja wa kanisa.

  source-TUMAINI LETU, WEEKLY NEWSPAPER OWNED BY CATHOLIC CHURCH IN TANZANIA
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  LOWASSA NA KANISA KATOLIKI

  Nani anamchafua huyu na kumtakasa yule?

  Na Kondo Tutindaga

  SASA imeripotiwa rasmi kuwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa atakuwa mgeni "maalum" katika harambee ya kuchagisha fedha kwa ajili ya Jimbo jipya la Katoliki la Ifakara. Harambee hiyo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

  Imeripotiwa pia kuwa harambee hiyo itahudhuriwa na maaskofu kadhaa wa kanisa hilo kubwa nchini. Hii yaonyesha umuhimu wa tukio hilo.

  Kimsingi, umuhimu wa tukio huonekana kwa waliohudhuria. Mgeni rasmi ni kikolezo muhimu katika hafla yoyote.

  Edward Lowasa ni jina kubwa na kwa hiyo kila likitajwa, lazima mijadala ianze. Mimi ni mmoja wa waathirika wa mijadala hiyo. Nimejiuliza, kati ya Lowassa na kanisa Katoliki, nani anamchafua mwingine na nani anamtakasa mwingine?

  Taifa hili limo katika mgogoro mkubwa wa uongozi. Wanaojadili kama mimi wanaliita ombwe la uongozi. Kwa kuonyesha heshima kwa mkuu wa nchi, watu wengi wanajificha nyuma ya neno ombwe kueleza udhaifu wa kiongozi wetu wa nchi.

  Wengine kwa kumstahi wanajilazimisha kuwalaumu wasaidizi na washauri wake, lakini kimsingi tuna rais mdhaifu kiuongozi na ambaye ameifanya taasisi ya urais iwe dhaifu na kupoteza heshima yake.

  Rais huyu na udhaifu wake kwa sehemu kubwa alijengwa na kanisa Katoliki pale lilipomtangaza kuwa ni "chaguo la Mungu."

  Alikuwa ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Dk. Methodius Kilaini aliyetamka kuwa "Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu."
  Wakati huo Lowasa ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mtandao uliomwingiza Kikwete madarakani mwaka 2005.

  Kwa hiyo, Lowassa si mgeni sana katika siasa za ndani na nje ya kanisa Katoliki. Ninaamini ndiyo maana hakai mbali nalo kwa sababu anajua tamko la kanisa hilo linaweza kumfikisha mbali katika harakati zake za kuwa rais ajaye wa taifa hili.

  Ni Lowasa aliyeonekana hivi karibuni katika harambee ya Kanisa Katoliki jijini Mwanza.

  Maneno mengi yalisemwa baada ya harambee hiyo na watu wengi walidhani baada ya maneno yale, ama Lowasa angekuwa mwangalifu kutumia makanisa, au makanisa yangekuwa na uangalifu kumtumia Lowasa. Yote mawili hayajatokea, labda ujumbe haujafika sawa sawa.
  Sehemu zote mbili zinahitajiana. Lowassa ana fedha – chafu na safi. Kanisa Katoliki lina ushawishi – mzuri na mbaya. Magwiji hawa wawili yaonekana wameamua kwa mara nyingine kutumiana ili kujinufaisha kwanza bila kujali maslahi mapana ya taifa letu.

  Nina maana kuwa, Kanisa katoliki lipate fedha na kujenga majengo na Lowassa asafishwe na apate madaraka ya urais anaoulilia sana. Ebu turudie tena kuangalia sehemu zote mbili.

  Lowasa ni "fisadi" pasipo shaka. Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanamwita fisadi, wapinzani wanamwita fisadi, bungeni anaitwa fisadi, yeye mwenyewe hajajiita fisadi lakini pia hajakana kama si fisadi.

  Rais Kikwete hajamwita fisadi hadharani na pengine hawezi, lakini walio karibu naye wanasema anakosa usingizi kwa sababu ya Lowassa. Alimruhusu ajiuzuru kwa ahadi ya kumsafisha. Aliposhindwa kumsafisha, Lowassa akaamua kujisafisha na kutafuta namna ya kutimiza ndoto zake. Katika hili, hakuna anayemlaumu Lowasa kwa sababu ana haki ya kujisafisha kwa njia yoyote.

  Rekodi ya Kanisa Katoliki katika vita dhidi ya ufisadi ina utata, sawa tu na rekodi za makanisa mengine. Ni kanisa lenye viongozi wanaokemea ufisadi hadharani bila woga.

  Tumemshuhudia Mwadhama Kardinali Pengo akifikia hatua ya kusema yuko tayari kufa kwa kutetea ukweli. Amepokea vitisho kadha wa kadha na kwa hakika tumeshuhudia akisifiwa hata na viongozi wa serikali.

  Rais Kikwete katika hafla ya kumpongeza Mwadhama Kardinali Pengo kutimiza miaka 25 ya uaskofu alimsifia sana kuwa ni mtu "asiyekurupuka" na anayejua kitu gani cha kusema kabla ya kukisema. Ni vigumu kuamini kuwa kualikwa kwa Lowasa katika harambee hii hakuna baraka za Mwadhama Pengo.

  Tumeshuhudia pia baadhi ya mapadre wa kanisa Katoliki wakiwafungia sakramenti baadhi ya waumini wake kwa kuwaalika viongozi wa kisiasa katika matukio kadhaa kwenye parokia zao.

  Viongozi wa kisiasa hasa wasiotoka katika chama tawala hawaruhusiwi kualikwa kama wageni rasmi katika halfa za kanisa katoliki. Sababu zinazotolewa na mapadre wanaowaadhibu waumini wao ni kuwa "wasichanganye dini na siasa." Kwa hili la kumwalika Lowasa ni vigumu kuamini kuwa si kuchanganya dini na siasa.

  Labda tufikiri zaidi. Kuna ubia gani kati ya CCM na kanisa Katoliki katika vita dhidi ya ufisadi nchini?

  Kanisa Katoliki linajua wazi kuwa utajiri wa watu wanaowakaribisha kuongoza harambee umejaa damu na jasho la watu maskini. Utetezi ambao kanisa hilo limekuwa likiutoa kuwa mafisadi kama waumini wana haki ya kuja kanisani na kuwa haliwezi kuwatenga hauna mantiki.

  Mbona kanisa linawatenga wazinzi, vibaka na hata waumini safi kwa kosa la kuwakaribisha parokiani baadhi ya wanasiasa wasio na hela nyingi?

  Mradi huu kati ya Lowasa na makanisa una maana moja kuu tu. Ni mradi wa kusafishana. Kanisa linamsafisha Lowasa au watuhumiwa wa ufisadi wengine ili lipate fedha; na mafisadi wenye madaraka wanalisafisha kanisa hilo lenye historia na matendo mengine mengi ya aibu.

  Vinginevyo haingii akilini, kanisa hilo hilo kupitia maandiko yake na mafundisho lipige vita ufisadi na hapo hapo liwakumbatie mafisadi na kutamani fedha zao.

  Kama ingekuwa kuwa fedha ya mafisadi inaingia kanisani kwa njia ya zaka, tungesitisha malalamiko yetu, lakini sasa kanisa limeamua mchana kweupe kuwaibia Watanzania kupitia fedha za harambee za mafisadi. Mafisadi wanajaribu kutakasa fedha zao chafu kupitia makanisa.

  Niliwahi kusema huko nyuma kuwa CCM inawachukia mafisadi lakini inapenda fedha zao; sasa kanisa katoliki linajitangaza kuwachukia mafisadi na ufisadi, lakini linatamani matunda ya ufisadi.

  Inawezekana fedha za Lowasa ni zile zile za Richmond, Dowans, EPA na nyinginezo ambazo zimekosesha huduma za jamii kama vile madawa hospitalini.

  Kuibwa kwa fedha hizo ndiko kulikosababisha migomo vyuoni, ndiko kulikosababisha mahakama kukosa fedha za kutosha za kutoa haki kwa wanyonge; kumepandisha bei ya umeme, kumewanyima maji safi mamilioni ya wananchi na kupandisha gharama za maisha kwa walalahoi.

  Fedha za Lowasa atakazotoa katika harambee ni hizo hizo zinazokosekana katika hazina ya taifa; yaani ni kama Edward Lowasa kaiba hazina kupeleka katika harambee ya kanisa Katoliki na kanisa linapokea na kutakasa uovu huo.

  Yawezekana hukumu yangu hii ikawa na makosa, lakini kanisa Katoliki likumbuke kwa makini kuwa siku za karibuni limelazimika kulipa mabilioni ya fedha kufidia maamuzi yake ya zamani ya kukumbatia uovu wa kashfa za ngono.

  Kukumbatia uovu kwa kujua ni dhambi inayoweza kulitafuna kanisa hili kwa muda mrefu.

  Kwanza, kitendo hicho kinalinyima kanisa nguvu ya ujasiri ya kukemea uovu, na pili kunalifanya kanisa kuwa mtumwa wa uovu huo.
  Madhara yanayosababishwa na ufisadi hapa nchini hayana tofauti na madhara ya kashfa za ngono zilizofanywa na mapadre huko nyuma na kuligharimu kanisa fedha nyingi.

  Kuna siku wahanga wa ufisadi hapa nchini, wajukuu na vitukuu, watasimama na kudai fidia si kutoka kwa serikali tu, bali hata mashirika na madhehebu yanayokumbatia vitendo hivyo.

  Kwa kumtakasa Lowasa, kanisa linajichafua kwa gharama ndogo ya harambee kupitia chakula cha hisani.

  tutikondo@yahoo.com

  MwanaHALISI - Toleo Na. 283
   
 3. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Tumeijadili jana hii kitu ulikuwa wapi mkuu??? Hebu achana nayo njoo tuzindue kampeni Arumeru mida hii kamanda Mbowe yuko Live unachelewaa
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Kanisa katoliki jimbo kuu la dsm lime-black list watu wa kuwaalika katika kukusanya pesa za maendeleo na miradi yake, ni wale ambao mienendo yao inatia wasiwasi.

  Ni kwa bahati mbaya sana Lowassa alikanyaga madhabahu ya bwana kule nyakato mwanza, tunaambiwa kuwa kanisa limehuzunishwa sana na mwaliko ule uliofanywa wakati askofu mkuu akiwaa nje ya nchi. Kanisa katoliki ni taasisi inayojitegemea kijimbo, pamoja na kuwa pengo ni kardinali hana mamlaka ya kuingilia askofu mkuu wa jimbo kama la mwanza ambalo ni archdiocese kama ilivyo dsm, wote mbele ya vatican ni maaskofu
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Shame on the roman catholic church. Shame on Senorine Libena, the new bishop of Ifakara.
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Aalikwa sio haalikwa
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  What's wrong with that?
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hatumtaki aende hukohuko wanakoruhusu kamgeni makanisani
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sahihisho: Kardinali Pengo ana mamlaka ya kum-discipline askofu aliye chini yake. Mbona anawahamisha hamisha i.e Kilaini?:
   
 10. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  usipipotoshe, kardinali hana hayo mamlaka, papa ndiye anayeteua, hamisha, simamisha au kufukuza maa-askofu. ni vatican peke yake yenye mamlaka juu ya askofu. pengo anaweza kuhamisha mapadre wake ndani ya dayosisi yake ya dsm, hawezi kamwe kumpa padre uhamisho hata kwenda hapo bagamoyo ambayo ni dayosisi ya Morogoro, soma taratibu za kanisa katoliki ni tofauti sana na tawala za kisiasa
   
 11. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mod, naomba niandike tena thread hii kwa kuwa humu ndani kuna mtu ameandika kuwa lowasa ataenda arumeru east baada ya kuhudhuria sherehe za kumsimika askofu salutaris libena wa dayosisi mpya ya katoliki ifakara.kanisa katoliki kupitia kwa askofu msaidizi wake eusebius ngigilwa lilishatamka wazi kuwa lowasa haajalikwa wala kwenye harambee zake, au kama mgeni rasmi katika sherehe hizo. Kanisa limeweka wazi kwenye magazeti linaloyamiliki kupitia tumaini media kama tumaini letu, tv tumaini etc, pia kanisa lilieza waziwazi kuwa huwa halina utamaduni wa kualika viongozi wa siasa kuchangia moja kwa moja shughuli za kanisa hasa wale ambao hupenda kutumia kanisa kujisafisha. Hivyo hata kama lowasa atahudhuria shereehe izo ataenda kama mtu binafsi au kumsindikiza mkewe regina, ambaye ni mkatoliki. Tafadhali someni taarrifa ya kanisa kwenye catholic web, na nyie wapambe wake please acheni kumsogeza mtuhumiwa wenu kwenye madhabahu takatifu ya bwana!!!!!!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mkapa atakuwepo!
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi Mungu yupo kwa ajili ya kubagua watu?.La hasha ni KUOKOA.
   
 14. M

  Mwanisawa New Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani lowasa yeye ni nani mpaka aalikwe, kwani wengine walio alikwa kwenye hyo sherehe hawatoshi, bila lowasa, acheni upumbavu wenu wa kuchanganya siasa na dini.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
   
 16. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  "usihukumu usije ukahukumiwa"
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kumbuka Mungu si mwanadamu hata awe na chuki kwa watu wake.
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Lowassa ni Freemason.
  Freemason huwa hawasubiri kualikwa, wanajipeleka wenyewe kadiri shetani anavyowaongoza!
   
 19. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Reference please?
   
 20. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Acha kuwa na akili kama za Kimalima Malima wewe.
   
Loading...