Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Hivi Mods hii post mmeunganisha na ya Mwanakijiji kwa sababu zipi wakati ni vitu viwili tofauti. ya mwanakijiji inatoa sababu za kutofaa wakati hii inatoa siri ya watu kumchafua
 
Lowasa yeye mwenyewe ni mchafu hakuna anayemchafua hata mmoja bali yeye ndiye mchafu.

ndugu Simiyu tatizo linalonipa changamoto ni kwanini watu wachafu hamuwachukulii hatua za kisheria amabzo zipo mpaka wanafanikiwa kuchukuwa fomu za kuwania uraisi? Je tulitunga sheria kwa ajili ya wengi na wachache adhabu zao ni chamani?
 
Nani anafaa?

mambucha komaa na jamaa hadi akujibu swali hili,tofauti na hapo atakuwa anapenda kupiga storiiiiii tu na maneno matamu,watu hawapendi tena maneno wanataka vitendo mwambie mwanakijiji aseme kwa kutaja jina kama alivyotaja hapo na makala zake zingine huwa anasema fulani hafai ila hasemi nani anafaa...
cc:Mzee Mwanakijiji
 
kwahiyo tumchague nani?
Mkuu komaa nae mpaka atutajie tumchague nani....
siyo atupe sifa hapa,mbona majina anataja hata makala zake zingine kataja majina flani hafai,flani hafai nani anatufaaa
mkuu komaa kumuuliza hata mara 10,M Quote halafu muulize tena na tena huyu Mzee Mwanakijiji,asituache njia panda haswa sisi ambae hatuelewi...
 


Hoja hii ameirudia tena juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ambao bila ya shaka wengi wamekuwa 'charmed' na wingu la umaarufu wa Lowassa kiasi kwamba hakuna ambaye ameweza kumbana vizuri kwenye maswali. Anasema endapo atachaguliwa basi ataelekeza nchi kwenye "elimu kwanza"; kwamba hiki ndicho kipaumbele chake.

Ugonjwa huu wa kutokuuliza maswali ya magumu yasiyokuwa na Majibu mepesi umeanza mbali uko kwenye vyombo vyote vya habari na Waandishi wake.

Pamoja na hilo la hapo chini ya Tido juzi tarehe 27/5/2015 Mhariri wa Raia Mwema naye alifanya kama Tido alivyofanya.
Nimetafuta Mahojiano husika lakini naona Gazeti kwenye web page yake hawakuweka-ukiyapitia mahojianao yenyewe utagundua tatizo unalolizungumza hapo juu.

Ni kweli kazi ya uandishi wa habari ni ya hatari maana inagusa masilahi ya watu/mtu lakini pale ambapo chombo/Mhariri au Mwandishi anafahamu wazi kuwa hata fanya kazi yake kwa uhuru na kwa manufaa ya Umma/jamii hasa hili la nafasi ya Kiuongozi basi ni bora kutokushiriki kwa namna ambayo ikowazi kuwa Chombo au mwandishi ni sehemu ya njama na wahusika kuhujumu Ukweli.




[h=3]Lowassa: Bado nahitaji utajiri (''Nachukia Umaskini'' by Lowassa Raia Mwema toleo na.407 Mei 27-June 22015 pg 12-13.[/h]
[h=3]Raia Mwema - Maswali ambayo Tido alishindwa kumuuliza ...[/h]





Lowassa inaonekana ameshindwa kuelewa au hataki kukubali kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni la aina tatu:
1. Ufisadi
2. Ufisadi
3. Ufisadi

Wanaomtaka Lowassa - wapenzi, mashabiki na waumini wake - watuambie vita dhidi ya ufisadi ina umuhimu na uzito gani katika agenda za Lowassa. Wakituambia kuwa "ni mojawapo" ya mambo atakayoyashughulikia tuendelee kumkataa kwa sababu bado atakuwa hajaelewa tatizo letu hasa ni nini kama taifa.

Nitandelea...

Sehemu ya Maswali ya Mahojiano ya Lowasa na Mhariri wa Raia Mwema.Na.407 Mei 27-June 2 2015 na ambayo hoja hii ya Ufisadi Ufisadi hadi 70x70 ilikuwa imepata nafasi.

Swali.
Raia Mwema:Umekuwa mwanasiasa kwa sehemu kubwa ya umri wako wa utu uzima,Ni wanasiasa gani unaweza kuwaita roles Model kwako?

Jibu:
Lowassa: Wanasiasa wawili walinivutia zaidi. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Kwame Nkrumah wa Ghana. Hawa ndio role models wangu kwenye siasa.

Swali.
Raia Mwema: Ina maana kwamba kama utafanikiwa kuwa Raisi wa JMT tutarajie uongozi wa aina ya Nyerere au Nkrumah kutoka kwako?

Lowassa: Hapana.Kuwapenda wanasiasa ni tofauti na kutawala kwa staili yao.Fahamu kwamba nyakati zimebadilika sana. Leo ni zaidi ya miaka 50 tangu tupate uhuru na watu ambao mwalimu alikuwa akiwa tawala na changamoto zao si sawa na watu waliopo leo na changamoto zao. Nitakupata mfano. Wakati Mwalimu akiwa Rais,kwa sehemu kybwa ,hakukuwa na tatizo la ajira kwa vijana kama ilivyo leo.Utatuzi wa hilo ni lazima uendane na mazingira yaliyopo.

Nina uhakika,kuna baadhi ya mambo ambayo wakati Mwalimu yangeweza kuvumilika lakini leo mwanasiasa mwingine akifanya hivyo anaweza kujikuta akipigwa mawe.

La muhimu hapa ni kwamba mimi ni Edward Ngoyai Lowassa na si Julius Nyerere au Kwame Nkrumah. Nina njia zangu za kufanya kazi. Ninawajua watu wangu na ninajua nini kinahitajika kufika kule Watanzania wanakotaka.

Nyerere na Nkrumah nitaendelea kuwapenda na kuwaheshimu lakini nitafanya kazi zangu kwa mujibu wa karama nilizopewa na Mungu na mahitaji ya Changamoto na mazingira yaliyopo.
 
Naziona mbio za mtia nia Lowata zikienda kuishia ukingoni bila mafanikio. Waswahili husema ngoma ikilia sana mwishowe hupasuka.
 
Ukitaka kujua kuwa Lowasa ni fisadi huhitaji kuumiza kichwa, wewe angalia tu marafiki zake: Chenge, Karamagi, Rostam Azizi na fisadi wa ubungo Bus terminal Kingunge Ngombale Mwiru
 
Lowassa ndie Rais... Mwanakijiji umechuja sana siku hizi... uzee mbaya hasa wa kudumaa akili..!!!
 
Lowassa ndie Rais... Mwanakijiji umechuja sana siku hizi... uzee mbaya hasa wa kudumaa akili..!!!

Mchakato ndani ya CCM bado, kampeni usiseme, bado ww unabwabwaja.. kweli ushabiki mbaya. Haya. Kaa na upofu wako, muda si mrefu tutaziona pumba na chuya.
 
Mwanakijiji sisi hatuaminishwi.Tunamfahamu Lowassa vema kuliko wewe na tunawafahamu wataka urais wote tz.Pamoja na mnavomdhihaki,mnavomtusi,mnavo mpaka kinyesi mh.Lowassa ndivyo mnavotufanya tumwelewe zaidi,tumwamini zaidi,tumpende zaidi,tumkubali zaidi,kumpigania zaidi na kumbeba juujuu kuelekea Ikulu.Hakatwi MTU.
 
Mwanakijiji sisi hatuaminishwi.Tunamfahamu Lowassa vema kuliko wewe na tunawafahamu wataka urais wote tz.Pamoja na mnavomdhihaki,mnavomtusi,mnavo mpaka kinyesi mh.Lowassa ndivyo mnavotufanya tumwelewe zaidi,tumwamini zaidi,tumpende zaidi,tumkubali zaidi,kumpigania zaidi na kumbeba juujuu kuelekea Ikulu.Hakatwi MTU.

Hafai full stop
 
kwa historia ya nchi yetu imedhihirika pasipo na shaka kuwa kiongozi aliyetoka jamii ya kimasai ni watu shupavu na wameonyesha kwa vitendo utendaji kazi wengine ni maneno matamu utafikiri wanatongoza binti wa kike. wa kwanza alikuwa ni Edward Sokoine na wa pili alikuwa ni Edward Lowassa.

siri kubwa ya kupingwa kwa lowassa ni Ukaskazini wake na Uthibitisho ni kauli iliyowahi kutolewa na Mmoja wa makada wa CCM kutoka Bagamoyo kuwa raisi hatatoka kaskazini.

Hili suala la kuchafua watu wa Kaskazini limekuwa pia likishikiwa bango na baadhi ya makada wa CCM dhidi ya CDM.


hivi nyie wanasiasa mnaohubiri ukanda mnayo akili kweli? nani kawamilikisha Tanzania?

Nani kakwambia Lowasa mmasai?
 
Back
Top Bottom