Lowassa: Gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa kama alivyosema Waziri Mkuu, Majaliwa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtumia ‘salamu’ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwamba gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa ukilinganisha na mahitaji ya Watanzania.

“Wananchi wamesema Rais Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya, lakini waziri mkuu wake amesema ni gharama sana mimi nasema gharama hizo ukilinganisha na idadi ya watu wanaohitaji jambo hili ni kubwa sana atukubalie tujadili Katiba Mpya,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.

Lowassa, awali aliwauliza wananchi: “Tunahitaji Katiba Mpya hatuhitaji?” na wananchi walijibu: “Tunahitaji.”

“Mimi pendekezo langu ni kwamba mheshimiwa Rais kwa heshima zote akubali mjadala wa Katiba Mpya,” alisisitiza Lowassa.
 
Mwacheni Mheshimiwa Rais Magufuli asafishe nchi kwanza hayo mambo ya katiba yatakuja baadaye
 
Hivi MZEE wetu Lowasa ile mvua ya mabomu iliishia wapi; nayo inahitajika katika mjadala wa katiba mpya. Nauliza tu kupata uelewa
 
Kama gharama si kubwa agharamie yeye. Pesa alizoibia wananchi akiwa na nyadhifa za juu serikalini atumie hizo
 
EL Alishiriki kikamilifu kutunyima katiba nzuri, atuombe kwanza msamaha kwa kuipinga rasimu ya Warioba kipindi kile
 
Back
Top Bottom