Lowassa azungumzia kuanguka kwa Hosni Mubarak

:car::Lowasa shetani::(maneno matamu but unafiki) hungry::popcorn:......................................... mbio za ....................................................Ikulu 2015.

I am frusty::A S thumbs_down::

Kama kweli waTZ watadanganyika kirahisi kumwamini hawa mafisadi kuchukua nchi 2015. Basi nchi hii wanaimalizia tu kuiuza.

Katiba mpya inawezekana kabla ya 2015? La sivyo wataiba kura kama kawaida. Nguvu ya umma inahitajika wakati huu kwa TZ. it is more than too late.
 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ambaye pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowassa amethibitisha kuwa ni kiongozi mwenye maono na mtazamo(visionary leader).

Lowassa amezungumzia nguvu ya umma ya wananchi wa Misri katika maeneo yafuatayo:-
1. Amewasifu na kuwapongeza wanaharakati wa Misri
2. Ameongelea sualala umuhimu wa kuwepo ukomo wa uongozi
3. Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati
4. Amezungumzia ubaya wa viongozi kujilimbikizia mali ambapo amesema
inasemekana Mubarak ana utajiri unaokaribia kumfikia Bill Gates
5. Amezungumzia athari za sera za ubepari kama mfumo huo hautachukuliwa kwa
umakini
6.Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusikiliza na kutatua matatizo ya watu

Lowassa amenena. Amethibitisha ukomavu wake ktk siasa na utendaji



Mchongoma hauzai zabibu!h
 
Viongozi wote wa africa ndo tabia yao hiyo
Kasahau hata hapa bongo mambo ndio hayo hayo
Iko siku wananchi wataamka
peopleeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeer

Mkuu maandamano ya nchi nzima kumwondoa Kikwete na mafisadi wake ni tarehe 19/02/2011
 
Awasifia wananchi wa misri.
Amkosoa mubarak kwa kukaa madarakani bila kikomo,kutosikiliza wananchi na kujilimbikizia mali.
Mwambieni Lowasa aache unafiki hana tofauti na Mubarak huenda tofauti yao ni kuwa mmoja ni mweusi na mwingine ni mweusi,awambie wananchi nao wapinge Dowans na CCM na pia arudishe mali. Alizolimbikiza na hazina maelezo ya jinsi alivyopata
 
Awasifia wananchi wa misri.
Amkosoa mubarak kwa kukaa madarakani bila kikomo,kutosikiliza wananchi na kujilimbikizia mali.

Huyu ndiyo wale wale anataka kujitakasa wakati yeye mwenyewe ni fisadi. Hakuwa na mali huyu miaka ya nyuma kawafisadi Watanzania na sasa ni bilionea. Akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete wako madarakani miaka 26 sasa ambayo inakaribiana na miaka 30 ambayo fisadi Mubarak alikuwa madarakani lakini wote hawa hawakuleta manufaa yoyote kwa Watanzania bali kuongezeka ugumu wa maisha na kero chungu nzima kama vile umeme wa shida, maji ya shida, umaskini wa kutisha n.k.

 
Aibu tupu Bunge la Spika Lowasa....maana Rais RA Spika Lowassa na si JK na Makinda
 
Lowasa na "U-turn" ya ghafla baada ya uchaguzi 2010. Anafuata msemo wa "JANJA YA NYANI KULA HINDI BICHI". Kuna mwanakijiji mmoja katika mazungumzo alimhurumia Mheshimiwa huyu kuwa mgongoni ana mhuri umeandikwa FISADI ambao itakuwa vigumu sana kuufuta hata kwa kutumia maji makali a betri.
 
hapo ndipo utakapo amini kuwa siasa ni mchezo mchafu, hv naota au lowasa ndo anatamka hayo? ;
mmmh kuna kitu
 
Awasifia wananchi wa misri.
Amkosoa mubarak kwa kukaa madarakani bila kikomo,kutosikiliza wananchi na kujilimbikizia mali.

Mbona anachekesha huyu mtu.. yeye anafanya nini?? kweli nyani haoni kun***&&^%
 
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ambaye pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowassa amethibitisha kuwa ni kiongozi mwenye maono na mtazamo(visionary leader).

Lowassa amezungumzia nguvu ya umma ya wananchi wa Misri katika maeneo yafuatayo:-
1. Amewasifu na kuwapongeza wanaharakati wa Misri
2. Ameongelea sualala umuhimu wa kuwepo ukomo wa uongozi
3. Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati
4. Amezungumzia ubaya wa viongozi kujilimbikizia mali ambapo amesema
inasemekana Mubarak ana utajiri unaokaribia kumfikia Bill Gates
5. Amezungumzia athari za sera za ubepari kama mfumo huo hautachukuliwa kwa
umakini
6.Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusikiliza na kutatua matatizo ya watu

Lowassa amenena. Amethibitisha ukomavu wake ktk siasa na utendaji


Mkuu ukomavu gani unazungumzia?

Yeye mali alizonazo zinaelezeka? Tofauti yake na ya Mubarak katika kujilimbikizia mali unaionaje???

Maneno mazuri bila kutoka moyoni ni upotezaji wa muda wetu. Tutasikia hata mafisadi papa wakitoka hadharani na kusema "unajua ufisadi ni mbaya" na bila aibu wengine watajitokeza kuwasifu na kuwapongeza.

 
Lowasa aache kabisa kumkosoa Mubarak hana haki hiyo.Wao si ndio kina Mubarak amekaa muda gani ktk ubunge kwa nini asiachie wengine nao waongoze jimbo lake.CCM imekaa miaka mingapi madarakani bila kutuletea mafanikio? Mbona haiambii iachie nchi? Lowasa Mubarak na wewe ni wamoja ila nchi tofauti. Kaa kimya
 
Lowasa aache kabisa kumkosoa Mubarak hana haki hiyo.Wao si ndio kina Mubarak amekaa muda gani ktk ubunge kwa nini asiachie wengine nao waongoze jimbo lake.CCM imekaa miaka mingapi madarakani bila kutuletea mafanikio? Mbona haiambii iachie nchi? Lowasa Mubarak na wewe ni wamoja ila nchi tofauti. Kaa kimya

nadhani hajatambua ni watanzania wa aina ipi anaongea nao leo hii.bado anahisi watanzania wote ni mbumbumbu.
 
Awasifia wananchi wa misri.
Amkosoa mubarak kwa kukaa madarakani bila kikomo,kutosikiliza wananchi na kujilimbikizia mali.

Sikutegemea maneno hayo kutoka kwa Lowasa because he is in the same boat.Ila ninahakika hajui analo ongea.Mubarak alisema haondoki na akaondoka.Wanafanana hao.Wamefundishwa na baba yao shetani kuwa waongo.Wasubiri their turn.
 
Kwako MH Lowassa.

Nirahisi kwako kumlaumu Rais wa Zamani wa Egypty Hussein Mubarak kwamba ame ng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu hadi wananchi walipochoka na kuamua kumtimua.
Si rahisi kwako kuelekeza lawama za namna hiyo hiyo kwa kundi la Wahuni ndani ya CCM, wewe ukiwemo, ambao kwa miaka mingi sasa wanaendelea kupindisha sheria na taratibu, wanaendelea kutumia madaraka vibaya na kujiweka juu ya sheria ili kujineemesha wao na familia zao pia kujenga mazingira ya kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza nchi hata pale ikosapo ridhaa ya wananchi.

MH Lowassa si rahisi kwako kuelekeza lawama kwa CCM kwa kuruhusu Wizi mkubwa wa mabilioni ya serikali, kuingia mikataba kihuni, kuingia mikataba na kampuni za mifukoni, kuwalinda majizi wakubwa ndani ya serikali ya CCM na wewe mwenyewe kushiriki wizi na Uharamia wa KIMAFIA. Vyote kwa pamoja vikiwa vimesaidia kuhujumu uchumi na kuyongeza gap kati ya matajiri na masikini.

MH Lowasaa si rahisi kwako kuilamu CCM kwa kuilea Rushwa na kuikomaza na kuendeleza unyanyasaji kwa wananchi. Kuzibia masikio vilio vya watanzania kuhusu Rushwa. Pia si rahisi kwako kujijazia Lawama kwamba umeshiriki kikamilifu katika kupokea RUSHWA na kuilinda RUSHWA kwa kutumia madaraka yako.
Pia si rahisi kujijazia Lawama Mabegani mwako kwamba Utajiri wako umetokana na Kiburi chako cha Fedha ya wizi,Wizi wa haki,Uongo na upotoshaji katika utendaji wako na Vitisho na hata kuua wananchi.

MH Lowassa wewe binafsi una HOJA nyingi sana unazotakiwa kujibu kutoka kwetu wananchi, na ninaamini siku moja utakuja kuzijibu kwa Amri yetu wananchi, ambazo umekuwa ukipiga chenga na hata kujificha nyuma ya kinga uliyo nayo ya kisiasa na mashoga zako ndani ya CCM kukukingia kifua.

MH Lowassa bado kuna maswali mengi kuhusiana na Richmond na Dowans ambayo unatakiwa kuyajibu ili kuweka mambo sawa. Richmond iliingia nchini wewe ukiwa Waziri mkuu lakini hata siku moja hujawahi kueleza wazi wazi au kwa hiari yako au kwa kubanwa ili kutoa kiwingu kwa nini serikali yako ilishindwa/ haikuweza kutambua dosari za Richmond na hatimaye Dowans??
Kwa nini serikali yako ilidai haimjui mmiliki wa Richmond wakati serikali ilikuwa na nyaraka zote na hata kama haikuwa nazo tuna idara ya usalama wa taifa ambayo ingeweza kuchunguza.

MH Lowassa kuna swali kuhusu kujua kwako kwa undani kwamba Richmond na baadaye Dowans ni kampuni za MH Rostam Aziz na haina wamiriki wowote nje ya Tanzania.

MH Lowassa kuna swali kuhusu wewe kama Waziri mkuu kuingilia utendaji wa kila siku wa TANESCO.

MH Lowassa unamlaumu Rais wa Zamani wa Egypty kwa kushindwa kusoma alama za nyakati??

Hivi nikikuuliza wewe na Chama chako CCM mna soma alama za nyakati hapa Tanzania??
MH Lowassa ni rahisi kwako kusoma alama za nyakati??
MH Lowassa undhani tumesahau mambo maovu ambayo wewe na kundi lote la Mafisadi ndani ya CCM mmetufanyia??
MH Lowassa unadhani maneno yako ya kujifanya mzalendo yanaweza kufuta uovu wako na uovu wa CCM kwetu sisi wananchi??
MH Lowassa unadhani tunasahau kwamba wewe na CCM yako mnawakumbati wageni na kuwalamba miguu na kuwapa ardhi yetu kinyang'anyi na kutufukuza kama mbwa katika maeneo yaliyo asili yetu??
MH Lowassa unadhani njama zako na za viongozi wenzako wa CCM za kuendelea KUHUJUMU,KUDHURUMU NA KUDHARIRISHA UTU WETU KISIASA NA KIUCHUMI zitafanikiwa??
MH Lowassa unadhani udhaifu wetu na unyonge wetu kiuchumi ndiyo kamba ya kutushona midomo ili kuziba vilio vyetu??

MH Unaongelea kuhusu viongozi kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi, wewe ukiwa waziri mkuu wa Tanzania ulipopewa kilio chetu cha Nishati ya umeme ulitatua??
Ukiwa Waziri mkuu wa Tanzania kwa makusudi ulituingiza katika mgogoro mkuwa wa nishati ya umeme mgogolo unaendelea hadi leo. Je MH Lowassa huko ndiko kusiliza na kutatua matatizo ya wananchi??

MH Lowassa kuna uongo umeuongeza hapa kwenye maelezo yako. Utajiri wa Mubarak hauzidi ule wa Bill gate wala si nusu wala si robo.
Mubarak anashukiwa kuwa na kiasi cha $1-5 Billions wakati Bill gate ana karibi mara 7 ya kiasi hicho umeongeza chumvi kwa makusudi ili kuonyesha kwamba Wewe na Viongozi wenzio wa CCM hamjatuibia fedha nyingi. Pia umesahau kusema Account zote za Muabarak Zimekuwa Freezed.
Kama ilivyo CCM Mubarak aliruhusu kundi kubwa la Wahuni wenzie ndani ya Chama kujichumia kimabavu na kuwanyonya wa egypty kwa nguvu na kiuuaji.

MH Lowassa hivi karibuni kijana wako alikutwa na Burungutu nene la Fedha $ 400,000.00 huko UK unaweza kuchukua nafasi hii kutueleza Fedha hizo alipata wapi?? Je fedha hizo ni halali na zilihamishwa kihalali kutoka Tanzania??
Na kwa nini alishitukiwa na Makachero wa UK??

Kumbuka Siku kama ya Mubarak ina kuja kwako na kwa mafisadi wenzio wote ndani ya CCM!!!!
Sehemu za kukimbilia zinazidi kuwa finyu kila siku.


Ukiacha Mwalimu Nyerere ni kweli hakuna Rais mwingine aliyekaa madarakni kwa muda mrefu. Lakini vipi mizengwe iliyojaa ndani ya chama cha CCM??
Bilal alishinda kura za maoni ya urais Zanzibar kwa makusudi mkamchagua Kijana wake Karume kama kifuta machozi je huko si kung'ang'ania madaraka kitimu?? MH Lowassa CCM inatumia Polisi Usalama wa Taifa na Dola nzima kuhakikisha Inapata Wabunge wengi na Rais anatoka kwake Je huko si kung'ang'ania madaraka kichama??
CUF wameshinda uchaguzi wa Zanzibar mara 4 lakini wakati wote wanaishia kupigwa virungu mpaka safari hii walipokubali kuolewa na CCM.
Je kuwaibia CUF ushindi wao ndiyo kusoma alama za nyakati na kusikiliza kilio cha wananchi??

Serikali ya CCM imekiuka amri ya Mahakama kuruhusu wagombea binafsi. Je huo si uvunjaji wa sheria?? Je huko si kuhodhi madaraka kichama?

MH Lowassa najua mwaka 2015 una nia hamu na kusudio la kuchukua Fomu ya kugombea Urais wa JMT ili once and For all kuhalalisha uovu wako wote na ule wa shoga yako Rostam na Viongozi wote wa CCM.

Je unajua wewe ni mmoja kati ya Viongozi walijilimbikizia Fedha nyinngi kwa njia ya Wizi Rushwa Magendo na Kupindisha sheria kwa kutumia madaraka yako??
MH Lowassa unajua kwamba wewe ni mmoja wa watu wenye kiburi na wasio kuwa tayari kujifunza? Na kamwe hawtakuwa tayari kusoma alama za nyakati??

MH Lowassa Unajua kuwasifu na kuwapongeza wananchi wa EGYPTY kupigania haki zao na wewe hapa Tanzania kuwa ni mmoja wa Viongozi wanaotumia nguvu za dola kuzima sauti ya umma ni undumila kuwili na ni janja yako ya Kucapitalize mchakacho wako kifashisti?? Na zaidi ni matusi kwetu Watanzania tuishio kwa taabu zote chini ya Himaya ya uonevu na uharamia ya CCM na Mafisadi wake??

MH Lowassa unajua kwamba huwezi kuendelea kudanganya watu siku zote??

MH Lowassa unajua kwamba kuna wimbi liitwalo"WORLDWIDE HIGH AWARENESS" ambalo kuanza kwake hakutoi nafasi za alama za nyakati?????



Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ambaye pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowassa amethibitisha kuwa ni kiongozi mwenye maono na mtazamo(visionary leader).

Lowassa amezungumzia nguvu ya umma ya wananchi wa Misri katika maeneo yafuatayo:-
1. Amewasifu na kuwapongeza wanaharakati wa Misri
2. Ameongelea sualala umuhimu wa kuwepo ukomo wa uongozi
3. Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati
4. Amezungumzia ubaya wa viongozi kujilimbikizia mali ambapo amesema
inasemekana Mubarak ana utajiri unaokaribia kumfikia Bill Gates
5. Amezungumzia athari za sera za ubepari kama mfumo huo hautachukuliwa kwa
umakini
6.Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusikiliza na kutatua matatizo ya watu

Lowassa amenena. Amethibitisha ukomavu wake ktk siasa na utendaji
 
Ndugu Zangu,



NDANI ya saa 24 baada ya tukio la Mapinduzi ya Umma kule Egypt, Edward Lowassa ,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ameonekana kwenye runinga akitoa tafsiri ya kilichotokea Egypt , nini cha kujifunza na kipi cha kufanya.


Lowassa alianza kwa kuwapongeza wanaharakati wa Misri. Akazungungumzia madhara ya viongozi kujilimbikizia mali, umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati, athari za ubepari, umuhimu wa viongozi kusikiliza matatizo ya watu wao na mengineyo. Kimsingi, Edward Lowassa alizungumzia masuala yanayowahusu ‘ People On The Streets’- Watu wa mitaani, na kwa lugha inayoeleweka na watu wa mitaani.


Na kwa hakika, yanayotokea sasa ni Mapinduzi ya Umma wa Kijamaa barani Afrika. Kilio cha mamilioni ya Waafrika ni kilio cha kutaka uwepo wa Haki za Kijamii- Social Justice. Sera za Kibepari hazijali haki za kijamii. Ndio maana, Wajamaa wa Afrika tumeyapokea yalitokea Tunisia na Misri kwa mikono miwili. Ni fundisho kwa watawala wetu. Tusingependa vurugu za Tunisia na Egypt zifike kwetu, maana zina madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi.


Hata hivyo, tunataka watawala wetu wasome sasa alama za nyakati. Waongoze mabadiliko ya amani ikiwamo mabadiliko makubwa ya Katiba ili tuepushe watu wetu kupoteza maisha na mali zao mara vurugu za kisiasa zitakapotokea. Na tusijidanganye, kuwa tuna amani, yetu ni amani ya vurumai.

Edward Lowassa ameonyesha ujasiri wa kujitokeza hadharani na kukiri , kuwa kuna mapungufu ya kimfumo, kwamba ubepari huu ndio umewafanya WaMisri waingie mitaani. Utajiri wa Mubarak unasemwa unaweza kuvuka utajiri wa Bill Gates. Wakati huo huo watu wa kawaida wa Misri wamekuwa wakiishi katika maisha magumu sana. Na Lowassa alionyesha hatari inayoweza kutokea kwetu . Amefikiri juu ya kipi kifanyike.

Mwanafalsafa Benjamin Disraeli anasema; “A good leader knows himself and the times”- Ndio maana pia ya kiongozi kuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati. Na kiongozi mzuri, hata katika nyakati ngumu, mara zote hujiweka katika nafasi ya ushindi.


Kwenye ulingo wa myeleka, hubaki katikati ya duara, atapigwa, ataanguka, atasimama. Atapigwa tena, ataanguka, atasimama. Hutokea kwa adui kuingiwa na mashaka na woga kutokana na ustahimilivu wa anayepigwa. Kwenye mchezo wa myeleka jitupe katikati upambane, kamwe usisimame kando ya duara, utaharakisha kazi ya adui kukutupa nje ya ulingo.


Na sifa moja ya mwanasiasa ni kuwa na uwezo wa kufanya yale ya kuwashangaza wengine, inahusu timing, inahusu wakati. Hata kabla ya Waziri wetu wa Mambo ya Nje hajaongea na wanahabari, Edward Lowassa , kwa nafasi yake ya uenyekiti wa kamati husika na mambo ya Ulinzi, Usalama na Nje ameongea na wanahabari.


Na hakuongea kwa kukurupuka, Lowassa alionekana kuifanyia kazi taarifa yake. Si ndio, wanaomjua Edward Lowassa wanasema, kuwa jamaa ni workalcoholik, ana ulevi wa kuchapa kazi. Anafanya kazi kwa saa nyingi. Na kuna ujumbe aliutuma jana, kuwa Edward Lowassa amerudi. Baada ya kimya kirefu.


Lowassa huyu anaonekana kuwa bado ana nguvu na ushawishi ndani ya Bunge na Serikalini. Si tumeona, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati nyeti bungeni bila kupingwa. Na kama ana dhamira ya kusimama, kugombea Urais 2015, basi, Edward Lowassa ana kazi moja kubwa inayomkabili ; kurudisha image yake ya zamani kwa umma, in principio, ya kama mwanzoni. Huu ni mtihani mgumu kwa Lowassa, akifaulu, 2015 hakamatiki.


Maana ni ukweli, kuwa Edward Lowassa wa sasa ni ’ libero’ uwanjani, hana wizara, lakini anaongoza Kamati nyeti na yenye nguvu kuliko zote bungeni. Lowassa huyu ni hatari kwa wapinzani wake katika kuelekea 2015 kuliko Edward Lowassa aliye Waziri Serikalini. Naam. Kuna burudani ya kisiasa inakuja.


Na kuna watakaoshika tama na kusema, kumbe, Edward Lowassa hajamalizwa kisiasa! Je, akina Mwakyembe hawakufahamu, kuwa simba humwui kwa risasi ya kumpapasa masikioni. Kama ni mchezo wa ngumi, basi, kwa mpinzani wa Lowassa, akubali, kuwa kummaliza Lowassa , awe tayari kucheza raundi zote 12.


Ndio, siasa inahusu pia sanaa ya mawasiliano, kwa mwanasiasa, kama huiwezi sanaa ya kuwasiliana na wananchi, basi, ni sawa na mtu anayejiita fundi mekanika , lakini hawezi kushika spana.


Tunayasema mabaya mengi ya Edward Lowassa, lakini, ni ukweli, kuwa Lowassa anaijua siasa na sanaa ya mawasiliano katika siasa. Katika mahojiano yale ya jana kwenye TBC, Lowassa aliwavuta anaowasiliana nao kwa kuanzia na mada husika na mahali alipochagua kufanyia mahojiano, palionekana kuwa ni nyumbani kwake, kule Dodoma.


Kwa muonekano, Lowassa alionekana yuko simple. Alikaa kwenye kochi karibu kabisa na mwandishi anayemhoji. Na mwandishi naye alikaa kulia kwa Lowassa kwenye kochi linalofanana na la Lowassa.


Tulimwona Lowassa akiongea kwa utulivu na kwa mpangilio, Edward Lowassa ni mahiri wa rhetorik, sanaa ya kuongea. Katika dakika chache zile, Lowassa aliweza kuunganisha yaliyotokea Egypt na ya ’binadamu wadogo’ wa hapa kwetu na mahitaji yao, akiwa na maana ya mahitaji ya watu wadogo. Lowassa ni Mmasai, labda Umasaini kuna ng’ombe na binadamu tu!


Na hapa mtaona tofauti, miezi kadhaa iliyopita tuliona kupitia TBC, mahojiano ya Ben Mkapa na mwandishi Edson Sanga. Mkapa alikuwa akitoa maelezo kuhusu kazi yake kule Sudan, mahojiano yale hayakuwa na mvuto, ni kuanzia kwenye upangaji wa scene ya mahojiano. Mkapa alikaa kwenye kochi akiongea huku akiangalia chini na huku anayemhoji akiwa kushoto kwake amekaa kwenye kito tofauti na Mkapa na umbali wa mita kadhaa. Ni heri mwandishi angemhoji Mkapa kwa njia ya simu.


Naam, siasa ni burudani pia, tusubiri ya usiku wa leo, kwenye TBC1. ITV na kwingineko!
Maggid
Iringa,
Jumapili, Februari 13, 2011
mjengwa
 
ngoja tutawajibu sasa nadhani hili wengine tumeliacha kwa muda hadi linaanza kuwa ni ukweli. Lowassa hana nafasi ya uongozi wa taifa la Tanzania. NONE. Not while he doesn't want to apologize to Tanzanians and own up his failures as a leader. Not a chance.
 
Back
Top Bottom