Lowassa azungumzia kuanguka kwa Hosni Mubarak | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa azungumzia kuanguka kwa Hosni Mubarak

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Feb 12, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Awasifia wananchi wa Misri.

  Amkosoa Mubarak kwa kukaa madarakani bila kikomo, kutosikiliza wananchi na kujilimbikizia mali.
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  huyo ndio mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, leo amesema kutosikiliza wananchi na kutosoma alama za nyakati ndio sababu ya viongozi kuchokwa na kuondolewa madarakani.
  Lakini pia tofauti kubwa ya kipato kati ya walionacho na wasionacho ametaja kama mojawapo ya sababu.

  TBC1

  My take:
  Siamini kama anayosema yanatoka moyoni.
  Nimeamini Lowasa yuko mbioni kugombea urais, hizi movie anazocheza sijui kama zitamsaidia tusubiri tuone.
   
 3. chokambayaa

  chokambayaa JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 528
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Viongozi wote wa africa ndo tabia yao hiyo
  Kasahau hata hapa bongo mambo ndio hayo hayo
  Iko siku wananchi wataamka
  peopleeeeeeeeeeees poweeeeeeeeeer
   
 4. c

  carefree JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kweli nyani aoni kundule naangalia tbc 1 lowasa anasema viongozi wasikae madarakani mpaka wachokwe , wasijilimbikizie mali wakati wananchi wana matatizo pia washughulikie matatizo yanayowaumiza wananchi akimaanisha hayo ndiyo yalisababisha wananchi w misri kumng'oa rais wao
   
 5. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kukaa madarakani muda mrefu sana sio issue kubwa tatizo ni kujilimbikizia mali... tena kwa kuiba kile kidogo ambacho raia maskini anahitaji ili aishi!! Ila na wewe mheshimiwa EL hivi hizo mali zote ulizonazo ulitoa wapi????
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huyu hata aseme lipi akigombea mimi na familia yangu na marafiki zangu hatutampa kura maana tunamjua ni fisadi.
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ameongea kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje.
  Hii yaweza kuwa mbinu ya kuzuia peoples power isitokee Tanzania.
   
 8. fige

  fige JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulianza kuitwa wananchi wa kawaida leo Lowasa kawaita wananchi wa Misri binadamu wadogowadogo anyway wamasai hawajui kiswahili inawezekana alitaka kusema lilelile neno tulilozoea wananchi wa kawaida.

  My take, kama sisi ni binadamu wa kawaida wao ni binadamu wa aina gani ?
   
 9. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu muheshimiwa angeanza kwanza kutuambia hizo zake alizitoa wapi kama sio kujilimbikizia akiwa mtumishi wa umma???:twitch:
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tangu nisikie kwamba huyu bwana ni miongoni mwa watu wanaotuongezea umasikini nchi kwa makampuni ya kimsukule, kadri ninavyojibidisha kuamini lolote analolisema, hata iwe ni jema kiasi gani, ndivyo ninavyojikuta roho yangu ikojitenga mbaaali kabisa na chochote kutokana naye.

  Mungu nisaidie siku moja niweze kuwasamehe Mafisadi wa nchi hii waliotufanya wengine tufanane tu na misanamu mbele ya 'waungwana' wa aina yao!!
   
 11. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu Fisadi Lowassa anachekesha Hizo mali alizonazo yeye na Mafisadi wenzake wamezitoa wapi? Kwani Wao ndio wanaosikiliza mamtatizo ya wananchi? tangu lini CCM na Serikali yake ikasikiliza matatizo ya wananchi? Mpumbavu Lowassa na hao waliomsikiliza na kumpongeza pia ni wapumbavu kama Lowassa wenyewe, Fisadi Lowassa:twitch:
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Makubwaa!!! Siku zote huwa nadhani ni mimi tuu, kumbe kuna na wengine huko nje wanaokoseshwa amani na hili KUNDI MUIBUKO ndani CCM??
   
 13. k

  kayumba JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi anadhani waTz wote ni mbumbumbu?

  Tunakuangalia kwa makini na hizo nyendo zako!
   
 14. F

  Fahari omarsaid Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Km ni wizi lowasa anaongoza ss anatoa ushauri gani wa kilevi
   
 15. kinja

  kinja Senior Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyo ni walewale na ndiye mubaraki wa tz. Tazama dip, kagoda, tangold, meremetaaaa, richmundi, dowans = mwk mambo ya nje
   
 16. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ambaye pia ni waziri mkuu aliyejiuzulu bwana Edward Lowassa amethibitisha kuwa ni kiongozi mwenye maono na mtazamo(visionary leader).

  Lowassa amezungumzia nguvu ya umma ya wananchi wa Misri katika maeneo yafuatayo:-
  1. Amewasifu na kuwapongeza wanaharakati wa Misri
  2. Ameongelea sualala umuhimu wa kuwepo ukomo wa uongozi
  3. Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusoma alama za nyakati
  4. Amezungumzia ubaya wa viongozi kujilimbikizia mali ambapo amesema
  inasemekana Mubarak ana utajiri unaokaribia kumfikia Bill Gates
  5. Amezungumzia athari za sera za ubepari kama mfumo huo hautachukuliwa kwa
  umakini
  6.Amezungumzia umuhimu wa viongozi kusikiliza na kutatua matatizo ya watu

  Lowassa amenena. Amethibitisha ukomavu wake ktk siasa na utendaji
   
 17. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kujilimbikizia Mali kana kwamba yeye hajilimbikizi mali, Fisadi Lowassa unamali nyingi ambazo umejilimbikiazia mbona hujisemi mweyewe na majambazi wenzake? watanzania sio wajinga kiasi hicho cha kumsema mwenzako kuwa amejilimbikizia mali wakati wewe mwenyewe una mali kibao:twitch:
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  huyo jamaa anaongea hivyo ili yeye aweze kujiweka karibu na wananchi.............2015 aweze kugombea maana siku za hivi karibuni amekua na matamko tofauti sana.......
   
 19. Mwelewa

  Mwelewa JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 2,312
  Likes Received: 2,522
  Trophy Points: 280
  Du, hii kali amepata wapi huo ujasiri kiongozi mwenye shutma za ufisadi kiasi hicho???
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri alitakiwa kuenda mbali zaidi na kusema kuwa si hivyo tu ni pamoja na kutosikiliza wananchi wanataka kina nani wawaongoze. Election model for Egypt was same as the one for Tanzania. Lowassa kugombea urais ni haki yake kama mtanzania ila kuchaguliwa na wananchi asahau hata kama chama chake kitampitisha na wakiiba kura 2015 ajiandae na ya misri.

  Suala la Egypt si kutosikiliza wananchi bali ni kuwadanganya wananchi. Kwa kuwa wananchi walikuwa wanajua hila za Mubarak kuwa ni muongo na mambo yakitulia hakuna kitakachofanyika basi wakaona ni bora wawe mitaani mpaka aondoke. Uongo pia ni utamaduni wa CCM kila uchaguzi wanaahidi mambo mapya wakati yaliyopita hawajatekeleza. CCM 2015 hata wamchague Dr Slaa aliyeshinda 2010 kihalali kuwa mgombea wao hawatashinda maana wananchi wanajua kuwa atakuwa ni kondoo mmoja tu ndani ya kundi la chui. Watu wanataka CCM out of power ili wajaribu kitu kingine na siyo kuachiana vijiti miongoni mwa kundi lilelile la wadanganya wananchi kila uchaguzi.

  Nina hakika kwa sasa watu watakuwa wanajiondoa chama tawala cha Misri wakijua kuwa under free and fair elections they would end up with nothing.
   
Loading...