WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
WAKUU,
Habarini za asubuhi ya Leo?Natumaini hali zenu zimeimarika zaidi kwa siku ya leo.
Nimepata taarifa kutoka huko Mkoani Geita Kwamba Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ameanza kuvamia kanda ya ziwa na harambee zake na anatarajiwa kufanya Harambee kubwa ya kuchangia kanisa la AICT Mjini Geita kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo Juni 16 mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya watu wanaoshughulikia ziara hiyo kwa ukaribu wamenidokeza kwamba pamoja na Harambee hiyo lakini ED anakwenda huko kwa kazi maalum ya kupanga safu yake ya Kanda ya Ziwa katika uchaguzi Mkuu ujao 2015!
Miongoni mwa waandaaji wakubwa wa Harambee hiyo ni Diwani wa kata ya Butobela Leonard Kiganga
Bugomola,ambaye ni Diwani anayedaiwa kukubalika na mwenye ushawishi mkubwa sana katika siasa za mkoa huo ambaye pia anajipanga kugombea ubunge katika moja ya majimbo ya mkoa Huo.
Bugomola anadaiwa kushirikiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Joseph Lwiza Kasheku (Msukuma) ambaye anaelezwa kwamba ni kambi ya ED inayojifua kwa ajili ya Mwaka 2015 naye anaelezwa kwamba atagombea ubunge 2015.
SWALI:KWANZA naomba kama kuna mwingine mwenye taarifa kamili juu ya Harambee hii na madhumuni yake atujuze,
PILI:Hivi bado ED ana nguvu za kuwani Urais mwaka 2015,anaweza?!