LOWASSA avamia Kanda ya Ziwa?!

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
WAKUU,

Habarini za asubuhi ya Leo?Natumaini hali zenu zimeimarika zaidi kwa siku ya leo.

Nimepata taarifa kutoka huko Mkoani Geita Kwamba Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ameanza kuvamia kanda ya ziwa na harambee zake na anatarajiwa kufanya Harambee kubwa ya kuchangia kanisa la AICT Mjini Geita kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo Juni 16 mwaka huu.

Hata hivyo baadhi ya watu wanaoshughulikia ziara hiyo kwa ukaribu wamenidokeza kwamba pamoja na Harambee hiyo lakini ED anakwenda huko kwa kazi maalum ya kupanga safu yake ya Kanda ya Ziwa katika uchaguzi Mkuu ujao 2015!

Miongoni mwa waandaaji wakubwa wa Harambee hiyo ni Diwani wa kata ya Butobela Leonard Kiganga
Bugomola,ambaye ni Diwani anayedaiwa kukubalika na mwenye ushawishi mkubwa sana katika siasa za mkoa huo ambaye pia anajipanga kugombea ubunge katika moja ya majimbo ya mkoa Huo.

Bugomola anadaiwa kushirikiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Joseph Lwiza Kasheku (Msukuma) ambaye anaelezwa kwamba ni kambi ya ED inayojifua kwa ajili ya Mwaka 2015 naye anaelezwa kwamba atagombea ubunge 2015.

SWALI:KWANZA naomba kama kuna mwingine mwenye taarifa kamili juu ya Harambee hii na madhumuni yake atujuze,

PILI:Hivi bado ED ana nguvu za kuwani Urais mwaka 2015,anaweza?!
 
Atawaambia wamchague yeye kwasababu anachangia kanisa. Bongo bwana akishinda uchaguzi kwa mfano, kanisa lina haki ya kusema lilimsaidia!
 
ana angaika sana huyu mzee na rasimu ya katiba mpya bado ana matumaini ya kupambana na hawa chipukizi ni hatari sana yeye na makanisa tu kwa nn asiende misikitini sasa? Amekosa cha kuzungumzia kwenye majukwaa ya siasa au siaende arusha mjini akafanye kampeni za udiwani
 
WAKUU,

Nimepata taarifa kutoka huko Mkoani Geita Kwamba Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ameanza kuvamia kanda ya ziwa na harambee zake na anatarajiwa kufanya Harambee kubwa ya kuchangia kanisa la AICT Mjini Geita kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo Juni 16 mwaka huu.

Hata hivyo baadhi ya watu wanaoshughulikia ziara hiyo kwa ukaribu wamenidokeza kwamba pamoja na Harambee hiyo lakini ED anakwenda huko kwa kazi maalum ya kupanga safu yake ya Kanda ya Ziwa katika uchaguzi Mkuu ujao 2015!
Siasa zinazochochea udini ni hatari na tutaendelea kuzikemea Accordingly.Hivi kuna haja gani ya kuhusisha kampeni, mitandao ya kampeni za urais/ubunge/udiwani na nyumba za ibada bila kujali dini? wakuu hili jambo ni double trafficking tuweni makini.Naona dalili mbaya mbele ya safari.Siwataji kwamba ni viongozi gani ambao washaanza kukatumia haka kamchezo kuelekea 2015 ila kwa kuwa wanajijua nawasihi waache.Watazua mgogoro usio wa lazma.
 
Huku hatumtaki, na anajua hilo
Unless kalipa watu wachache wamvalishe sijui nini nini kama kawaida yake

Akavamie Korea kusini
 
Ninavomjua Lowasa, ni mtendaji mzuri sana.huwezi kumlinganisha na pinda the "shock absorber" wa serikali ya sasa, wala kikwete, au Wasira, Lukuvi na wengineo. nilitamani siku moja lowasa awe rais lkn alichafuliwa na ccm hiyohiyo
 
Tuwe na Mtemi wa Kimeru???

Yeye awanunue hao wanaofanya naye maigizo mbele ya TV ili akarushwe kwenye TBC yake

Ndg,wanaweza kumpa...si juzi walimpa Pindaa..huyu kidogo mizimu ya kisukuma itamsaidia kupunguza kulia lia kwake...kuna mwingine baada ya kuiba na kuliingizia taifa hasara kubwa(chenge) wasukuma wakamtunuku UTEMI kwa kazi Nzuri na nzito ya uizi....

Lakini kiboko yao ni yule aliyewaambia pale Bujora kuwa"wanafunzi wanaopata mimba ni vihere hele" baada ya kazi hiyo nzito wakamtunuku UTEMI na kumuita MASANJA huku kabla ya hapo akiwa amepewa kiti kama hicho sehemu tofauti tofauti na kubeba mizimu ya makabila tofauti matokeo yake mizimu inapambana kweli kweli na kusababisha kila akaapo anaishia kujiinamia na kusinzia.....mizimu ya kimasai,kikurya,kiha,kihaya,kihehe,kisukuma,kinyakyusa,kifipa ikibebwa na mtu mmoja anaweza kuishia kuwa zezeta.. Kosa jingine jina la Masanja,hili jina si la kupewa mtu hovyo hovyo,wasukama wametuharibia rais wetu kiasi kwamba kichwani mwake anawaza kuwa MASANJA kweli kwa kutumia mda mwingi kuizunguka Dunia.
 
Acheni Mawazo ya kijinga.

“Watanzania ni
watu wapole na
wakarimu ila mna
tatizo moja la
kuhofia kila jambo.
Kila kitu
mnachofanyiwa
mnaona kuna baya
linakuja. Sisi tuna
nia njema ya
kuwasaidia
kuendelea.
 
Utemi wa kulipa hela hata 'masanva' hayakutambui

Unadhani anaweza sogelea hata 'kaduku' wa hivyo? Hata kwenye 'mita' lazima mumtoe

Ndg,wanaweza kumpa...si juzi walimpa Pindaa..huyu kidogo mizimu ya kisukuma itamsaidia kupunguza kulia lia kwake...kuna mwingine baada ya kuiba na kuliingizia taifa hasara kubwa(chenge) wasukuma wakamtunuku UTEMI kwa kazi Nzuri na nzito ya uizi....

Lakini kiboko yao ni yule aliyewaambia pale Bujora kuwa"wanafunzi wanaopata mimba ni vihere hele" baada ya kazi hiyo nzito wakamtunuku UTEMI na kumuita MASANJA huku kabla ya hapo akiwa amepewa kiti kama hicho sehemu tofauti tofauti na kubeba mizimu ya makabila tofauti matokeo yake mizimu inapambana kweli kweli na kusababisha kila akaapo anaishia kujiinamia na kusinzia.....mizimu ya kimasai,kikurya,kiha,kihaya,kihehe,kisukuma,kinyakyusa,kifipa ikibebwa na mtu mmoja anaweza kuishia kuwa zezeta.. Kosa jingine jina la Masanja,hili jina si la kupewa mtu hovyo hovyo,wasukama wametuharibia rais wetu kiasi kwamba kichwani mwake anawaza kuwa MASANJA kweli kwa kutumia mda mwingi kuizunguka Dunia.
 
Lowasa is the next president kama hamuamini subirini TIME WILL TELL.tunahtaji watu watendaji na wenye kujiamini na si waigizaji.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom