Lowassa atuma shushushu CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa atuma shushushu CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 18 April 2012

  [​IMG][​IMG]
  HATUA ya mfuasi mkuu wa Edward Lowassa kuhama CCM na kujiunga CHADEMA, imetafsiriwa kuwa njia ya Lowassa "kutuma shushushu" katika chama cha mageuzi.

  Lakini Millya amejitetea akisema, "Sijatumwa kuchunguza wala kuua CHADEMA. Ndugu yangu nia yangu ni njema na ili kuthibitisha hilo ni kwamba kuona ni kuamini," anasema Millya; "CHADEMA ni chama chenye matumaini mapya kwa maisha ya Watanzania."

  Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigella alisema kujiondoa kwa Millya ni hatua ya utekelezwaji wa maazimio ya NEC iliyoagiza baadhi ya wanachama wake kujipima na kama wakijiona kuwa ni mizigo wajiondoe mapema.


  Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Dar es Salaam amesema, "Si bure. Nani asiyemfahamu James ole Millya, kuwa ni kidole na pete na Lowassa? Kuna kitu wanatafuta."


  Millya amekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha. Alitangaza kujiunga na CHADEMA juzi Jumatatu.


  Lowassa ni waziri mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya mkataba wa kufua umeme wa kampuni ya Richmond.


  "Imenishtua, imeniudhi na itakiweka chama chetu mahali pabaya. Ni hatua ya tata," amesema ofisa mmoja wa ngazi za juu wa CHADEMA.


  Amesema Millya amekuwa mfuasi mkubwa wa Lowassa; na Lowassa hivi sasa yumo katika mbio za "kusafisha jina lake" tayari kwa kugombea urais mwaka 2015.


  "Jambo hili halina heri. Huu ni mtego na mpango mkakati wa kutudhoofisha. Wanajua CHADEMA ina nguvu na imejipanga kutwaa madaraka mwaka 2015," ameongeza ofisa huyo ambaye ameomba asitajwe jina.


  Hata hivyo, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wanamkaribisha Millya wakiamini kwamba ni mpambanaji katika kutaka kuleta mageuzi ya kiuongozi nchini.


  Hofu ya wanachama wengi wa CHADEMA waliopiga simu kwenye chumba cha habari MwanaHALISI, kuhusu suala hilo ni kwamba Millya ametumwa kama shushushu kwa ajili ya kujua mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.


  Katika kipindi chote ambacho viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA wamekuwa wakishutumu mikataba ya kifisadi iliyoliingizia hasara taifa, ukiwemo mkataba wa kampuni ya kufua umeme wa Richmond, Millya siyo tu amekuwa kimya; amemganda Lowassa kama luba.


  Aidha, Millya amekuwa mtiifu kwa Lowassa ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kuhusika kuipa zabuni ya kufua umeme kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na uwezo wala vifaa.


  Hata Lowassa aliposhutumiwa pia kuhusika kuhamisha mkataba huo kwa kampuni ya Dowans, Millya alikaa kimya.


  Tathmini iliyofanywa na wanachama wengi wa CCM juu ya kushindwa kwa chama hicho kung'ara katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ilionyesha kulitokana na kuwepo kwa watuhumiwa ufisadi ndani yake.


  Watuhumiwa wa ufisadi ambao hata Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) iliazimia kuwang'oa kwenye chama ni waliohusika na mikataba ya Richmond na Dowans na ununuzi wa rada ya Jeshi la Wananchi.


  Wanachama wa CCM waliokuwa wanatuhumiwa na kwamba lazima waondolewe kama magamba ni aliyekuwa mwanasheria mkuu na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge; mfanyabiashara maarufu Rostam Aziz ambaye alikuwa mbunge wa Igunga, na Lowassa.


  Tofauti na mawazo ya wana-CCM, Millya amesema, "Chama hiki kinavurugwa na Samuel Sitta na Dk. Harrison Mwakyembe kwa kueneza vitu vya uwongo dhidi ya Lowassa."

  Millya alikuwa akimshutumu Sitta aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa kwa kuunda Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la mkataba wa Richmond.

  Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Dk. Mwakyembe ndiyo iliweka wazi "ujasiri wa kifisadi" katika mradi huo na hatimaye Lowassa akajiuzulu pamoja na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.


  Baada ya NEC kuazimia watuhumiwa wote wa ufisadi wajiondoe, Rostam Aziz alijiuzulu nyadhifa zake zote lakini si kwa ufisadi bali kwa kile alichoita siasa uchwara ndani ya CCM. Lakini Chenge aliwaambia wapigakura wake wasiwe na hofu kwani lile gamba "limeishia kiunoni."


  Millya alikaririwa akisema kuhusu kashfa ya Richmond na kujiuzulu kwa Lowassa kuwa, "Kama kuwajibika katika kashfa hiyo, aliyepaswa kuwajibika ni rais mwenyewe aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri."


  Historia ya Millya ndiyo inawafanya wanachama na wafuasi wa CHADEMA waamini huenda kijana huyo ametangulizwa kwa malengo maalum ambayo baadaye yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa chama.


  Akitangaza uamuzi wa kuvua fulana za njano, kofia za njano na kuvaa magandwa ya CHADEMA juzi, Millya alisema kuminywa kwa demokrasia ni sababu ya msingi ya yeye kujiondoa CCM.


  "Mwenyekiti (Rais Jakaya Kikwete) ameendelea kupuuza mawazo ambayo sisi wengine tumeona kwamba yangeweza kuimarisha chama, lakini CCM imekuwa ni ya wachache," alisema.


  "Mwenyekiti ameshindwa kazi kwa sababu Kamati Kuu (CC) inayoongozwa na Rais Kikwete imeshindwa kusimamia serikali na kuleta matumaini mapya ndani CCM na kwa Watanzania."


  Pia alimtaja mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Ridhiwani Kikwete kwa "kushiriki" tamko la kibaguzi kwamba "Rais ajaye 2015 hatatoka Kaskazini."
   
 2. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  CDM chama makini, na lowasa keshachelewa.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kama kweli ni shushushu, Chadema wasikubali mpango huo, Lowassa mikono yake ina damu ya ufisadi; aje kwanza atangaze alifisani nini kwa wananchi wa Tanganyika kwanza, he has to come out clean, na Chadema itafikiria kumpokea
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Huku ni kumpa Lowassa sifa zisizo zake ...

  1.Ni mwanasiasa

  2. ni shushushu


  3. ni waziri mkuu wa zamani,

  4. ni mbunge

  5. ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge


  Heeeeeeeeeeeeeeeeeeee bado kidogo tutasikia katuma shushushu JF
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Not a news! Out dated!
   
 6. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Duh:glasses-nerdy:!napita tu
   
 7. M

  Malova JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hata kama ametumwa, kwa chadema hatapata chapa.
   
 8. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  They want to confuse us.
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nilitaadhalisha siku ya kwanza tu Millya alipotangaza kuhama CCM. Chadema wanapaswa kuwa makini sana na huyu jamaa vinginevyo mambo yataharibika. Wanapaswa wasimpe ujumbe wa kamati kuu na asiudhulie vikao vikuu vya chama.
   
 10. Mtanga Tc

  Mtanga Tc JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hata kama ni shushushu,kwa uweza wa Mungu atarudi na kutoa taarifa njema za kuinua CDM and not contrariwise!
  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
   
 11. k

  kaudagaa Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hakuna ukweli wowote kuhusu hilo, taarifa nilizonazo kutoka kwa watu wa karibu na lowassa zinasema kuwa lowassa mwenyewe alipigiwa simu na millya majira ya saa nne asubuhi 15th 04 2012 akimtaarifu juu ya kukihama chama chake.

  my take; lowassa alikuwa hajui linalo endelea. mpeni nafasi but msimwingize mpaka chumbani kabisa, mtoto wa nyoka ni nyoka although nabii Musa alikulia nyumbani kwa farao akaja kuwa mkombozi wa wana israel.:smile:
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mbona tunarudi nyuma waungwana? Milya/lowassa tuliwajadili sana, na hakuna asiyejua uhusiano wao nje ya siasa. Anyway, kama kweli katumwa mwacheni kijana akazitumbue za mjinga, mwishowe anapeleka feedback kuwa chadema hakuingiliki
   
 13. m

  majogajo JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  tena ni chama makini sana, kumbuka Shibuda alitumwa naye awe shushushu ila ameonekana kashindwa. nathibitisha kwani nae ni 1 ya waliosaini kwenye karatasi ya zitto.
   
 14. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Wakuu kama Millya anawaona Sitta na Mwakyembe ni wazushi kwa kumsingizia Lowassa then naweza kuamini kuwa huyu huenda akawa shushushu kweli asiyewatakia mema Watanzania na si mzalendo. Sitta hakufanya kosa lolote kuunda tume ya kuchunguza Richmond kutokana na tuhuma zilizokuwepo. Ina maana Millya anataka kutuambia kuwa Sitta alitakiwa kuupuza tuhuma dhidi ya Richmond? Mwakyembe na kamati yake walichunguza na kujiridhisha pasipo shaka kuwa Lowassa alihusika kulazimisha kuwapa richmond tenda na ni rafiki wa Rostam kwa sana. Kwa maneno haya ya Millya naona hafai kuendelea kuwa CDM si mpiganaji halisi. Huenda amekimbia tu CCM baada ya kuona ananyimwa nafasi za ulaji mfano kugombea Ubunge wa Afrika mashariki, pia walimbana kutokana na urafiki wake na fisadi Lowassa.

  Ushauri wangu: CHADEMA mfukuzeni huyu mapema kabla hajakiharibu chama na tayari kwa maneno yake haya ameshaanza kukitia doa chama.
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Tahadhari kwa CDM.
  Kujiunga kwa ghafla kwa milya na ukimya wa Lowassa kuhusiana na move ya Mlilya vina usiri mkubwa sana chadema inabidi wawe makini sana na huyu jamaa kwani hajakata mawasliano yake na Lowassa na hisia zangu ni kwa chadema kufanya haraka na kumsimamishisha kwy jimbo fulani halafu ajitoe amuache mtu wa ccm anapeta at last minute. CDM wawe makini na hawa wanachama wa ghafla sijui kwanini hawajifunza kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.
   
 16. I

  Ilongailunga JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,132
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Sasa naanza kuamini kuwa gazeti la Mwanahalisi lina agenda ya siri dhidi ya Lowassa, haiwezekani kila toleo liwe na mada dhidi ya EL , ni vema kujadili hoja za millya kwanini kahama CCM kuliko kuanza negative speculations, ndio hili gazeti liliandika habari mbaya dhidi ya Sitta alipolikemea halijarudia mpaka leo. Si sahihi kwa watu makini kumuweka LOWASSA above every thing, event event, and above TZ politics!
   
 17. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,448
  Trophy Points: 280
  Kuna mstari mwembamba sana umetenganisha kati ya kushinda na kushindwa. Ni vizuri kuwa na confidence lakini ni hatari kuwa na over-confidence.

  Sina haja ya kusema lakini naomba viongozi & wanachama wa CDM msibweteke na ....'kusema tuko imara' na/au 'CDM ni chama makini'. Complacent is the worst form of enemy
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  biased journalist
   
 19. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,789
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  kitu cha maana Milya abakie kama mwanachama wa kawaida na cdm wasikurupuke kumpa uongozi wowote au kumshirikisha katika mikakati au mipango ya siri ya chama na pia cdm waendelee kumchukulia kwa taahadhari na kufuatilia mwenendo wake hadi kujiridhisha ni kamanda wa ukweli!!
   
 20. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi naona Millya alikaa CCM kwa matumaini ya kuona mabadiliko lakini hatimaye ameona anaweza kusubiri kitu ambacho hakipo. Hata kama ni kipenzi cha Lowassa, bado ni mapema mno kumhukumu kwamba ametumwa kufanya ushushushu. Millya kuhamia CDM kusimfanye akose urafiki na watu aliokuwa nao muda mrefu. Isitoshe ameona kipenzi chake Lowassa hayuko salama ndani ya CCM. Ndoto ya Lowassa kuteuliwa na CCM kugombea urais 2015 inazidi kufifia. Hapa cha msingi viongozi wa CDM wawe makini kuhakikisha kuwa Millya anakaa chini ya uangalizi kwanza bila kupewa cheo chochote ndani ya CDM hadi baada ya uchaguzi wa 2015. Kama nia yake ni kuharibu chama basi ajihesabu ameingia choo cha kike maana viongozi wa CDM wako makini kuliko sisi tunavyodhani. Kama Millya anafanya uchunguzi na CDM itafanya uchunguzi mara 100 yake. unaweza kukaa CCM kwa matumaini kama Nape kungojea kisichokuwepo hadi ukaishia kuchanganyikiwa. Ni ukweli ulio wazi kuwa ndani ya CCM kuna watu wanachukia maovu ila tatizo lao ni waoga wa kujinyea. Nadhani wamerogwa na Prof Maji Marefu wasihame. Maana hawasikii wala hawaoni hata kama masikio na macho wanavyo. Hawa wachache akina Millya ndo watakuwa wamenusurika kupigwa na vibuyu vya mchawi wao Maji Marefu. Kwanza huyu mtoa mada hii ninamtilia shaka kuwa yeye amehumizwa na kitendo cha ujasiri wa Millya wa kuhamia CDM. Sasa anatafuta agenda ya kutaka Millya afukuzwe ili aaibike amcheke na kupata sababu ya wengine waliomfuata Millya wasitulie. Millya aachwe, atapewa mafunzo maalumu na kusubiria wakati wake muafaka. Kama amekuja kwa ajili ya kupata cheo haraka, bila shaka atatimka. Kama kweli ni mpambanaji basi atasubiria.
   
Loading...