Lowassa atembelewa na Madiwani kutoka Halmashauri ya Magu mkoani Mwanza

Lowasa Aache haya mambo ya Kukutana na makundi makundi asije kuanza kujenga mtandao wake upya, kwa sasa Tunatekeleza Ilani. Asitukwamishe
 
hahaha, inafurahisha, nakumbuka kwenye kampeni yule jamaa wa mwanza alitoa shairi lake ati anaharisha atawaletea kipindu pindu, nilihuzunika sana, mtu huwezi ropoka vile kwani hujui kesho yake, ona sasa, hawa hawa wa mwanza ndio waliomtukana sana kwenye kampeni, tena matusi ya dhihaki na dhihaka, daah aisee,
Wasukuma wanaanza kujipendekeza kwa wa Kaskazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kutangaza kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukaa ndani ya upinzani kwa takribani siku 1312 kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiongozi huyo ameanza kupewa fursa.







LOWASSA AAAAAAAA.jpg

Lowassa akiwa a baadhi ya madiwani Halmashauri ya Magu​
Fursa ambayo kiongozi huyo ameipata ni kutembelewa na madiwani kutoka Halmashauri ya Magu mkoani Mwanza ambao walifika ofisini kwake Mikocheni Dar es salaam kwa ajili ya kumuomba kutembelea halmashauri hiyo.
Wakizungumza mbele ya kiongozi huyo, Madiwani walimuomba Lowassa kutembelea Jiji la Mwanza baada ya uamuzi wake wa kurejea chama tawala ikiwa pamoja na kuhamasisha hali ya ukusanyaji wa mapato kwenye jiji hilo.
Wakati akipokelewa na uongozi mkuu wa CCM, Marchi 1, 2019 Lowassa mwenyewe hakubainisha nini sababu ya kurejea CCM, bali aliishia kusema kuwa amerudi nyumbani.
Chai bila maziwa? Hivi vyuma imeshakuwa taaabuu
 
Hivi kuna watu humu hawajui unaweza tu kuwa na ofisi unayoitumia kukutana na watu kuongelea issue mbalimbali za maendeleo na biashara?

Siyo lazima hiyo ofisi iwe na leseni au iwe biashara fulani. Na pia hauhitaji kuwa tajiri au mwanasiasa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom