Lowassa atawatesa CCM milele

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,104
2,000


KATIKA uchaguzi wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, watu wengi walishtushwa ilipotangazwa kwamba kada maarufu, Edward Lowassa, aliyekuwa anakonga nyoyo za Watanzania, hakupitishwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kamati Kuu ya CCM haikutoa maelezo ya kutosha kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), kwa nini wanachama walioomba nafasi ya kuteuliwa kugombea urais hawakuitwa kujieleza. Wana CCM 42 walijaza fomu ya kuomba uteuzi, hawakuitwa kutoa maelezo, badala yake Kamati Kuu ikaja na majina matano na kuyaweka mbele ya NEC.

Kwa kuwa habari za uteuzi huo zilikuwa zimevuja, wajumbe watatu wa CC, Sofia Simba, Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa, waliitisha mkutano na kuwaambia waandishi wa habari kwamba hawakukubaliana jinsi uteuzi ulivyoendeshwa.

Kamati Kuu ikapeleka majina matano kwenye NEC na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipoingia ukumbini, wajumbe wote walisimama na kuimba: “Tuna imani na Lowassa” ilhali wakijua kwamba jina lake lilikwisha katwa!

Kilichotokea ni historia. Lowassa, yumo katika kumbukumbu akisema hataondoka CCM, lakini baadaye, alifuatwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na akakubali kuungana nao kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo alikubali kupeperusha bendera ya Chadema kugombea nafasi ya urais.

Katika kampeni za chama tawala, jina la Lowassa lilichafuliwa sana—huku wakimtwisha kila aina ya lawama na kumpaka kila aina ya uchafu. Hakuna kiongozi wa CCM ambaye alipanda jukwaani alikosa kutamka kwamba Lowassa ni mchafu, fisadi, ni mwizi, mgonjwa na hatamudu nafasi ya Ikulu. Waliendelea kuwaaminisha wapiga kura kwa maneno hayo, lakini hakuna hata mmoja wao aliyetoa vielelezo vya tuhuma dhidi yake, ukiondoa ule wimbo walioupenda wa ‘Kashfa ya Richmond.’ Wakaahidi kuunda mahakama ya kuwahukumu mafisadi—kana kwamba ndiyo ilikuwa kipaumbele cha wananchi—wakisahau kwamba waliofanya hayo ni viongozi wa CCM!

Sasa Lowassa, ambaye aliwaasa wana Ukawa kuendesha siasa za kistaarabu, wasijibu mapigo kwa matusi na kashfa, waeleze sera na nini watakifanya wakipewa dhamana na kuingia Ikulu, juzi hapa amefunguka na kusema:

Lowassa aliwahi kusema: “Dhamira yangu wakati natangaza kuwania urais ndani ya CCM, ilijulikana wazi kuwa ni kwenda kuifumua mikataba ile, ndiyo maana wakubwa wale wakasimama kidete kuhakikisha sipenyi.”

Akampongeza Rais John Magufuli kwa kuisoma Ilani ya Ukawa—ambao ndio walitamka kwamba wataifumua mikataba yote mibovu na hasa mikataba ya madini. Hili halikuwamo katika Ilani na wala haikuwa sera ya CCM. Sasa Rais Magufuli amechukua hatua ya kuiangalia upya mikataba hiyo, na amemwagiza Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, apitie upya Sheria ya Madini na kuipeleka bungeni ama kubadilisha baadhi ya vifungu, au kuifuta kabisa sheria hiyo.

Wakubwa wa CCM walipokuwa wanaulizwa ni nini alichofanya Lowassa, walisema kichinichini kuwa ni mtu wa kisasi—kumbe walijua kuwa alikuwa hapendelei jinsi mambo yalivyokuwa yanaendeshwa.

Sishangai kwamba Umoja wa Vijana wa CCM wanadai kwamba Lowassa ameyasema hayo ili kujitafutia ‘umaarufu’. Lowassa ni mtu maarufu sana, ndiyo maana hata akikohoa kuna watu wanatetemeka.

Hata vijana wa chama tawala bado wanaendelea na wimbo wa Richmond na ufisadi bila kutoa ushahidi.

Tatizo la vijana wa chama tawala inaelekea hata historia hawasomi wakajua tulikotoka, tulipo na tuendako. Niwakumbushe kwa uchache tu. Lowassa akiwa Waziri wa Maji, ndiye alivunja mwiko wa Tanzania kutotumia maji ya Ziwa Victoria. Lowassa akiwa Waziri wa Ardhi, alimpokonya tajiri mmoja kiwanja cha Mnazi Mmoja (pale Mnara wa Azimio), alichokuwa amepewa na Meya wa Dar es Salaam kupitia CCM. Waliovunja uzio na kuchukua mabati wanalijua hilo.

Akiwa Waziri Mkuu, Lowassa ndiye aliyeanzisha kampeni ya madawati shuleni, lakini alipoondoka aliyefuata hakulitilia maanani. Lowassa, hata kama hamumpendi, ndiye aliyetoa agizo kwamba kila kata iwe na shule ya sekondari na Kituo cha Afya. Someni background kabla hamjaropoka neno na kumzulia mtu tuhuma ambazo hamuwezi kuzisimamia.

Wanahabari pia wanapaswa kuacha kuandika kila lisemwalo na wanasiasa. Kabla ya kulifikisha kwa wananchi, wachambue maneno yao na kauli zao. Mmoja wa viongozi wa UWT aliwahi kusema, tena bungeni, kwamba Lowassa ni mwanamume.

Vijana, si wa CCM pekee—vijana wote wajifunze kuheshimu watu—hasa waliolitumikia Taifa hili, kama si kwa kazi walizofanya, waheshimuni basi kwa umri wao. Tunamuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, si kwamba katika utawala wake wa miaka 23 hakuwahi kufanya makosa. Mwalimu alisema hakuwa Mungu na kwa hiyo lazima kuna makosa aliyofanya. Lakini alituachia wosia pia: Ikulu ni Mahali Patakatifu.


Acheni kutoa misifa kuwapamba viongozi, wao ni binadamu pia, wana mapungufu yao. Hatuwezi kuyaanika, ila tunayajua. Hii vita ya uchumi haikuanza leo. Misingi yake ni Azimio la Arusha ambalo CCM waliamua kulitosa baharini pale Kisiwa cha Chumbi (Zanzibar), wakaifuta miiko ya uongozi iliyokuwa inawabana kutotumia nafasi zao za uongozi kwa manufaa yao binafsi. Uozo wote wa kuingia mikataba mibovu, ulianzia hapo.

Kelele za Loliondo na hujuma za rasilimali za Taifa hazikuanza juzi. Hadi twiga walibebwa kwa ndege pale Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kupelekwa ughaibuni. Yote haya yanatokana na ubinafsi wa viongozi wa juu wa chama tawala. Ni serikali ya CCM iliyoua viwanda, ni Serikali ya CCM iliwapa Makaburu Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) sawa na bure. Ni Serikali ya CCM juzi kati, imeuza hisa zote katika viwanda vya bia na sigara, licha ya kwamba vilikuwa vinatoa gawio kubwa kwa Serikali!

Ukitaka kumnyooshea mtu kidole, jiangalie kwanza mwenyewe kama uko vipi. Kutoa kauli za kuudhi ili kumdhalilisha fulani, ni siasa za maji taka. Kama hujui jambo, lifanyie utafiti au waulize watangulizi wako.

Tafakari kwanza kabla ya kutamka maneno ya chuki dhidi ya Lowassa.
 

jembe afrika

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,336
2,000
Hivi@lizabon yuko wapi au buku 7 zimefika kikomo. Maana huyo huwa akimuona lowasa huwa anajinyea
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,668
2,000
Haya maandiko anatakiwa Shaka wa uvccm ayasome ili ajiongeze maana anakoelekea ataokota makopo!!!
 

Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,946
2,000
Lowassa ni mwanasiasa aliyekomaa kisiasa kwa hiyo lazima atuumize ndo maana mikutano tumezuia kwani huyu mtu siasa anazijua namna ya kuzichanganya karata zake. Anayesema hatuumizi sawa tumruhusu aende mikoani kuwashukuru wapigakura waliopigia japo hakushinda ndo tutajua anavyotutesa.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,318
2,000
Hili linahusianaje na namna Lowassa anavyowatesa CCM?
Mtu mpaka anaenda kuomba kura za kidini halafu unasema anawatesa CCM?

Nnaona yeye ndiye mwenye kuteseka.

Kama kuna mtu Dunia hii ana hamu na Urais basi wa kwanza ni Lowassa. Amefanya kila njia, katumia kila maarifa, pesa, honga makanisa na misikiti, honga mpaka kwenye sherehe za harusi. Mitandao ya ku brainwash watu nchi nzima, kampeni yupo taabani mpaka anakosea kupanda masteji, mpaka yaliyomkuta Chato, lakini wapiiiii?

Na bado anaendelea kuteseka kwa uchu wake wa madaraka.

Nnakushangaa unaposema anaitesa CCM, CCM ilishamuona hafai toka alipopigwa chini Uwaziri Mkuu.

Kumbuka huyo ni Waziri Mkuu wa kwanza Tanzania kung'olewa madarakani kwa kashfa. Mateso madogo hayo?
 

PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
367
250
nilijualo; hakuna kuteswa kubaya kama kwenye uchaguzi mkuu!
nawachia wenyewe lkn km mfuatiliaji wa siasa naamini ndugu yangu umepagawa kbs....kujifariji huko sidhani km kutakutolea maumivu. lete hoja 'magreat thinkers' tujadili bwana!!!!!
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,104
2,000
Mtu mpaka anaenda kuomba kura za kidini halafu unasema anawatesa CCM?

Nnaona yeye ndiye mwenye kuteseka.

Kama kuna mtu Dunia hii ana hamu na Urais basi wa kwanza ni Lowassa. Amefanya kila njia, katumia kila maarifa, pesa, honga makanisa na misikiti, honga mpaka kwenye sherehe za harusi. Mitandao ya ku brainwash watu nchi nzima, kampeni yupo taabani mpaka anakosea kupanda masteji, mpaka yaliyomkuta Chato, lakini wapiiiii?

Na bado anaendelea kuteseka kwa uchu wake wa madaraka.

Nnakushangaa unaposema anaitesa CCM, CCM ilishamuona hafai toka alipopigwa chini Uwaziri Mkuu.

Kumbuka huyo ni Waziri Mkuu wa kwanza Tanzania kung'olewa madarakani kwa kashfa. Mateso madogo hayo?
kwa hiyo watu wa msikitini na makanisanai sio wapiga kura?
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,104
2,000
Umemsikia anavyoziomba hizo kura?

Sasa huyo ndiye wa kuitesa CCM au CCM imemtesa yeye?

Ukisoma huelewi, ukitazama video huelewi.

Hivi kuna mateso zaidi ya kung'olewa uwaziri mkuu kwa kashfa?
Hivi hizo kashfa uchwara mlizomtungia mbona hamjawahi kumfikisha mahakamani?
 

Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,946
2,000
Pole mwanaccm mwenzangu ktk dini ni majibu ni hayo. Itikadi ni imani inayoishi Moyoni kama zilivyo imani za dini kwa hiyo hizi zote ni imani zingine .Kwa hiyo huko makanisani ndo zilikozaliwa ndo maana tunaambiwa imani ndo mfumo au mwongozo hapa duniani .Bila imani ya kitu chochote huyo mtu ni shida. Kwa ufupi tena siasa na dini hizi zote ni ndugu kwa wanafanya shughuli zao kwa kushirikiana kimawazo na kimtazamo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom