Lowassa atakupunguzia kura!

Tz Asilia

Member
Oct 30, 2009
45
1
RAIS wangu, siko hapa kumhubiria mtu au watu, bali kuihubiri habari njema ya ukweli, upendo na haki.

Katika watu waliofanikiwa sana kiuongozi kisiasa katika nchi hii kwa nyakati zao ni pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Edward Moringe Sokoine, Augustine Lyatonga Mrema (wa zamani), Edward Ngoyayi Lowassa na John Pombe Magufuli.

Watu hawa walikuwa na hulka inayofanana. Ni watu wakali kweli kweli. Pamoja na kuwaheshimu lakini wengi wetu wema kwa waovu waliwaogopa sana. Kwao hawa hakuna maamuzi magumu.

Katika kutenda ni mahiri, hawangojei wala hawasiti au kutia shaka. Kulia ni kulia kama vile kushoto ilivyo kushoto.

Wakati wao kila mwananchi aliona matairi ya nchi yanazunguka, nchi ikawa inakwenda.

Rais wangu, wewe ni mtu tofauti na hawa kama sisi wengine tulivyo tofauti. Ndiyo kazi ya Mungu, binadamu hawafanani.

Alituumba kila mtu na tabia zake. Wengine wanasema baba ni mpole sana, wakati wengine wanasema u - mvumilivu kupita kiasi. Wako wanaosema subira yako haina ukomo.

Wengi hawakujui unapokemea. Hawaoni unapoamua. Hawasikii ukifokea. Watu wamejaa mashaka kwa kukosa muongozo. Tofauti hizi na kwa haya yaliyotokea hivi karibuni bungeni najawa na wasiwasi, ndugu Edward Lowassa atakupunguzia kura wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.

Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Nitaupiga vita ufisadi wa aina yoyote hata kama ufisadi huo utafanywa na baba yangu au mama yangu mzazi.

Nitaendelea kuitetea kweli bila kujali binadamu wengine wanawaza au watasema nini, kwa kuwa naamini ni katika ukweli tu ndimo kuna upendo, haki na amani ya kweli.

Rais wangu kashfa ya Richmond imeipitisha nchi katika mashaka mazito.

Waziri mkuu na mawaziri wengine wawili walijiuzulu. Baraza la mawaziri likavunjika lenyewe. Rais akabaki peke yake akining'inia. Nchi hii ilikaa kama ziwa lenye maji yaliyotuama kwa miaka miwili!

Hapakuwa na kiongozi wa kuelekeza, wala wa kushauri, wa kukemea au wa kutoa maamuzi Richmond ishughulikiwe vipi. Viongozi wetu walikuwa waoga wa Richmond kutokana na ushiriki wao.

Nchi iliachwa angani ielee na Richmond, itakapoangukia ndipo hapo hapo. Wawanda wanasema, "Pano yaponela iponele!" Imeanguka na sasa tunahesabu na kutafakari athari zake!

Tumewasikia makamanda wa vita dhidi ya ufisadi walivyofanya hitimisho lao kule bungeni. Tumeziona kufuli za Spika Samuel Sitta alizofungia mjadala wa Richmond. Tukamsikia na waziri mkuu akiyasema matarajio yake kwa wahanga wa udhalimu huu.

Kwa haya yaliyokwisha kufunuliwa na yanayoendelea kufunuliwa, Edward Lowassa atakupunguzia kura baba katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Ndugu Rais na Spika Sitta, Edward Lowassa na wapiganaji wa vita dhidi ya ufisadi tuambieni ukweli kuhusu Richmond, nayo kweli itawaweka huru!

Bwana Sitta mjadala wa Richmond hauwezi kufungwa mpaka wanawanchi waambiwe ukweli.

Mmekula zaidi ya milioni 450 fedha za walipa kodi, maelezo yako wapi? Mwana mwema Ananilea Nkya na wanaharakati wenzako tumekusikia.

Tutaenda kaskazini mwa nchi yetu, kusini, katikati na magharibi, kuyaambia makabila zaidi ya 120 ya nchi yetu ukweli kuhusu udhalimu huu uliofanywa na wabunge wao wa Chama Cha Mapinduzi!

Mwenyezi Mungu awatangulie katika hili! Nasi kwa pamoja tupaaze sauti zetu juu ya jukwaa moja tukitaka maelezo kwa nini mkutano wa 18 wa Bunge ulishindwa kuchukua hatua madhubuti juu ya kashfa ya Richmond, mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, ukodishaji wa Bandari kwa TICTS, TRL, na ripoti za Loliondo na mgodi wa dhahabu wa North Mara.

Viongozi wema hata ndani ya CCM bado wapo, watatusikia! Jinsi paa anavyotamani vijito vya maji, ndivyo roho yangu inavyoitamani CCM isiyo na viongozi wa sasa.

Mwaka 1995 ndugu Rais ulijitokeza mbele ya Watanzania kuomba urais. Haukuwa peke yako kama wenzako, kina Benjamin William Mkapa, Cleopa Msuya, John Samwel Malecela na wengine. Kwa kutafuta mtu wa kukupiga ‘tafu' uliwaaminisha Watanzania kuwa wewe mwenyewe uliona kuwa peke yako hautoshi.

Hukumchagua mwingine yeyote ila Edward Ngoyayi Lowassa. Leo hauko na Edward Lowassa unataka tena urais, utatosha vipi? Mwezi wa kumi utakapowarudia Watanzania kuwaomba kura watakuuliza, mwenzio yuko wapi? Watataka kujua hatima ya Richmond. Mara zote mbili ulimhitaji Edward Lowassa, safari hii umempata Edward mwingine? Lowassa atakupunguzia kura!

Kumbuka ndugu rais mliitwa ‘Boys II Men.' Mlisafiri hata kwa helikopta pamoja katika kutafuta neema ya maisha ya baadaye kwa ajili yenu wenyewe na familia zenu.

Baadaye mkapanga mipango mikubwa zaidi ya kuitwaa nchi.

Nchi mkaitwaa. Tukadhani yale maandiko yasemayo ‘Kila mtakapokusanyika wawili au zaidi mimi nitakuwa kati yenu' yanatimia. Hiyo haikuwa.

Badala yake tunaiona kazi ya shetani. Iweje leo kile mlichotafuta pamoja ubaki nacho peke yako! Nguvu ya Lowassa iliyofanikisha urais itakapowekwa hadharani Lowassa atakupunguzia kura.

Nguvu kubwa iliyoanza nayo Serikali ya Awamu ya Nne iliwapa wananchi matumaini makubwa ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Njaa ilipoikumba nchi serikali ilionekana kutenda kwa wakati na hata ugonjwa mpya wa Bonde la Ufa ulipoingia serikali iliukabili kama vile ilikuwa inaungojea.

Shule zilianza kuota kama uyoga kila kata nchi nzima. Ahadi ya zahanati kila kata ilikuwa katika ‘programme'. Dhamira ya serikali kuwapa Watanzania maisha bora ilionekana wazi. Katika kile kipindi kifupi Watanzania walijawa na matumaini.

Lowassa alipoondoka, akaondoka na matumaini yote ya Watanzania kupata maisha bora. Tangu hapo tukaanza kusikia ombwe la uongozi. Tukasikia uongozi wa juu ni dhaifu. Uongozi ukaanza kufundishwa kufanya maamuzi magumu ambayo mpaka leo haujafanya.

Tangu Lowassa aondoke hakuna Mtanzania anayejua tunakwenda wapi! Hakuna anayejua serikali inafanya nini! Hata shule za kata ambazo zingechukuliwa kama kisingizio cha maendeleo nazo zikaathirika na kuondoka kwa Lowassa. Zilizobaki zinajengwa kwa ‘remote'. Kumbe nguvu ya serikali alikuwa Edward Lowassa?

Kumbe heshima ya serikali alikuwa Edward Lowassa? Baba utaonyesha nini kwa wananchi mwezi wa kumi ambacho ni kazi ya mikono yako? Ni kipi ulichokifanya baada ya Lowassa kuondoka? Ndugu Rais, Lowassa atakupunguzia kura!

Rais wangu ulilitangazia taifa kuwa Edward Lowassa ni rafiki yako kikazi na kifamilia. Naye kwa unyenyekevu kabisa akaongezea: "Na urafiki wetu haukuanzia barabarani.'' Watu makini walielewa.

Kilichotokea ndani ya CCM mwaka 2005 yalikuwa ni mapinduzi kama mapinduzi mengine yoyote. Hili nalo neno. Mna deni kubwa kwa wana CCM na kwa Watanzania wote.

Mlitengeneza maadui wengi kwa sababu njia nyingine mlizopitia zilikuwa za hila. Wakati wa kulipa deni hili kwa Watanzania utahimili bei yake bila Edward Lowassa baba?

Safari zako nyingi za nje hazikuwapalia wananchi wakati wa Lowassa kama zinavyowapalia sasa.

Edward alijua kuzifukia kwa kuwapatia wananchi cha kufanya. Wale ambao wako katika mateso kwa sababu ya wawekezaji, wanapokuona kutwa ughaibuni ukidai unatafuta wawekezaji wanakuelewaje? Mwekezaji anayekuja kuwekeza kwa faida yake si mjomba wetu wa kutusaidia!.

Ukiona, una madini mengi na mengine yanapatikana Tanzania peke yake katika ulimwengu mzima na tena una wanyama wa kila aina na mbuga na vivutio tofauti na sehemu nyingine duniani.

Nawe umewekeza wawekezaji wako katika nyanja zote hizo, lakini bado huna uwezo wa kuwasomesha watoto wako, huna uwezo wa kuwatibu watu wako, na huna uwezo wa kutoa huduma za kijamii na za kimaendeleo, jua unafanya kazi ya **** au gulagula. Si busara hata kidogo kuendelea kutafuta waporaji (wawekezaji) wengine.

Angalia sekta ya madini. Ni wapi alipowekeza mwekezaji ambapo wananchi wanaomzunguka hawako katika mateso?

Mara ngapi tulimwona Edward Lowassa akiwaita wawekezaji na kuwaambia matakwa ya serikali nao wakatii? Uwezo wa kutenda, umahiri katika kutenda na ufuatiliaji ndiyo siri kubwa ya kiongozi bora.

Leo kabaki Magufuli peke yake, naye kapewa samaki na ng'ombe huku majambazi wakitamba na kuua wananchi watakavyo. Hatuwezi kumweka Magufuli Mambo ya Ndani, wananchi wakiwa salama atapata mvuto! Nina hakika Edward Lowassa atakupunguzia kura.

Tumewashuhudia mitume au makamanda walivyo mahiri wa kujieleza. Walitumia mizinga, mabomu na bunduki za rashasha. Wakatwambia adui yao na wetu ni mafisadi. Baada ya kiongozi wao Spika Samweli Sitta kusimamisha vita, wananchi wameenda kuangalia athali za mabomu yao na silaha nyingine.

Kwa mshangao wa wengi, hakuna hata fisadi mmoja aliyeuawa. Hata wa kujeruhiwa tu hakuna.

Ufisadi na mafisadi wamebaki vile vile walivyokuwa mwanzo! Wananchi sasa wameamini walichoambiwa siku ile bungeni, kuwa kilichokuwa kinalengwa na kushambuliwa si mafisadi ni uwaziri mkuu.

Makombora yote yalitupiwa kwa uwaziri mkuu ambao walifaulu kuuteketeza kabisa. Tunamshukuru Mungu kutupa mtu mwenye upeo mkubwa wa kufikiri.

Alijiuzulu mara moja. Nina hakika, angegoma kama alivyogoma Edward Hoseah, amani ya nchi ingekomea pale. Yangetokea machafuko makubwa ya kumwaga damu. Edward, kwa hili taifa lina deni kubwa kwako!

Akiwa katikati ya wabunge, Edward Lowassa alilia: "Nimefadhaishwa sana", lakini ni wangapi walimsikia? Wachache sana. Na wachache zaidi walimwelewa. Sikupata bahati ya kumwelewa wakati ule.

Nimekuja kumwelewa pale rais wangu ulipolitangazia taifa kuwa Richmond ni zao la baraza la mawaziri ambalo wewe ndiye mwenyekiti wake.

Nilijua umeukata mzizi wa fitina. Kuanzia pale nikawa nangojea moja kati ya mawili.

Au serikali yote iporomoke au Bunge lifunge mdomo liendelee na serikali isiyo na udhu.

Sikutegemea mtu angemgusa tena Naziri Karamagi, Ibrahim Msambaha, Edward Lowassa, Edward Hoseah na wote waliotajwa na Bunge kuwa wawajibishwe kutokana na kashfa ya Richmond.

Baba ulipokiri kuwa Richmond ni msalaba wako, ulinikumbusha ile hadithi tuliyosimuliwa kuwa, Bwana Yesu alikuwa na wafuasi wake. Watesi wake walipomfuata aliwauliza:

"Mwamtafuta nani?"

Wakamjibu, "Yesu Mnazareti!'

Akawaambia: "Ni mimi hapa, nikamateni. Waacheni hawa waende zao kwa amani".

Uongozi wa kichungaji. Huku ndiko kuwajibika kwa dhamana kubwa uliyopewa. Baba, haukuwa jasiri. Kukiri peke yake haikutosha. Ulipaswa kusema:

"Ni mimi hapa nikamateni. Waacheni hawa kina Edward Lowassa, Nizar Karamagi, Ibrahimu Msabaha, Edward Hoseah, Auther Mwakapugi, Johnson Mwanyika na wengine wote mliowaorodhesha waende zao kwa amani.''

Kama wana madhambi yao mengine wahukumiwe kwa madhambi yao mengine si Richmond.

Urais ni pamoja na machungu, si raha tu. Kwa haya Lowassa atakupunguzia kura katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Rais wangu Kama Spika Samuel Sitta aliikataa ripoti yenye ukweli kamili ya mafisadi iliyotolewa na Dk. Slaa, akaikubali ripoti yenye ukweli nusu iliyotolewa na Dk. Mwakyembe, amebakiwa na udhu gani wa kuendelea kuwa kati ya viongozi wakuu katika nchi hii?

Jina la rais wetu limetumika vibaya. Rais wetu amehusishwa na wapiganaji bandia wa vita hii bandia bila mtu kukanusha kwa miaka miwili. Hata alipozuka fisadi anayetangatanga kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa uko pamoja naye huku akiwafisadi hata watu maskini kabisa na kujidai kuwasaidia maskini wengine baba, hukumkanusha! Tunataka rais ajaye awe mtendaji.

Nchi haiwezi kukaa kimya kama maji katika mtungi miaka miwili halafu mkasema rais yupo! Wanaotuletea habari za mvuto ni wapuuzi.

Mwenye akili timamu havutwi kijingajinga. Hata hivyo mashindano ya mvuto si yapo? Kama mtu ana mtu wake ampeleke huko akashindane.

Profesa mzima analeta upuuzi wa mvuto katika masuala ya nchi! Nao hawa wamekosa mtu wa kuwakemea.

Aje rais mtendaji kwa mambo makubwa ya kitaifa. Kukabidhi gari moja kwa mkurugenzi mmoja haiwezi kuwa kazi muhimu ya rais wetu.

Yakifanyika makosa tunasoma Ikulu yamwangukia mkurugenzi, heshima ya Ikulu iko wapi? Tunaowadhania kuwa ni wana wema tuwataje kwa majina wananchi wawajue ili kati yao hao wamchague wamtakaye.

Wana CCM kama Salim Ahemd Salim, John Pombe Magufuli, Abdulrahaman Kinana na Edward Lowassa wasipochukua fomu kuomba kugombea urais mwaka huu, wakae wakijua, iko siku wataulizwa namna walivyovitumia vipawa walivyopewa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake.

Rais wangu, wengine waliona ni unafiki lakini uelewa mdogo ulichangia.

Edward Lowassa alipoiita serikali yote na familia zao pale Karimjee kumuaga binti yake, hukutokea.

Machungu anayoyapitia leo Lowassa ni kwa sababu ya kukubali kwake kubeba msalaba wa bosi wake, kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ni kwa sababu ya fitina, chuki na uovu uliotendwa na kamati ya Bunge ya kuficha ukweli.

Kukutana na rafiki yako faragha na kumkacha mbele ya hadhira, jamii ya kistaarabu inaweza kuona ni kitendo cha kizandiki vilevile. Kinaweza tu kuwafurahisha toto tundu.

Kama wanakamati wa kamati ya Bunge chini ya uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe, wangemwogopa Mwenyezi Mungu wasingeuficha ukweli mwingine. Akitumia ripoti batili, Spika Samueli Sitta na Bunge lake waliwafukuzisha kazi, waziri mkuu na mawaziri wengine wawili.

Baada ya mambo sasa kufunuliwa, Spika, Samuel Sitta na Bunge lake wangekuwa wanamwogopa Mwenyezi Mungu wangemwomba radhi ndugu Edward Lowassa na mawaziri wawili waliojiuzulu pamoja naye.

Rais wangu, katika kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere tuliambiwa kuwa 1995 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hakumkataa mtu, bali aliwauliza baadhi yao akisema: "Ninyi ni wahuni? Hivi ndivyo tunavyomchagua rais wa nchi?" Yaonekana walikuwapo wagombea wahuni.

Kwakuwa sakata la Richmond limeendeshwa kihuni na kumalizwa kihuni na viongozi wetu, basi ni dhahiri kuwa baadhi ya viongozi wetu ni wahuni tu! 2005.

Mwalimu Nyerere angekuwa hai asingewakubali wahuni kuwa miongoni mwa viongozi wetu.

Wananchi wasiwarudishe madarakani wahuni katika uchaguzi ujao. Ni jukumu lako Rais wangu kulisimamia hili, vinginevyo Edward Ngoyayi Lowassa atakupunguzia kura!.


Source: Gazeti la Tanzania Daima la Leo.

Swali kwetu Wanajamiiforum, Je yaliyoandikwa yanaukweli?
 
Hii makala inavutia kuisoma!

Ila bado sijafunguka vizuri kwanini anasema Lowasa agombee Urais!?

Kwanini alikubali kuwa mbuzi wa kafara kama sio yeye aliyehusika na Richmond, ndo kusema hana ujasiri wa kukataa kufanya mambo maovu anayoamuriwa na boss wake?!

"Ila kuna sehemu imenigusa na kunifanya nijiulize mara mbili mbili, ntanukuu;

Mwaka 1995 ndugu Rais ulijitokeza mbele ya Watanzania kuomba urais. Haukuwa peke yako kama wenzako, kina Benjamin William Mkapa, Cleopa Msuya, John Samwel Malecela na wengine. Kwa kutafuta mtu wa kukupiga ‘tafu' uliwaaminisha Watanzania kuwa wewe mwenyewe uliona kuwa peke yako hautoshi. Mwezi wa kumi utakapowarudia Watanzania kuwaomba kura watakuuliza, mwenzio yuko wapi? Mara zote mbili ulimhitaji Edward Lowassa, safari hii umempata Edward mwingine?

Kumbuka ndugu rais mliitwa ‘Boys II Men.'"

nadhani hiyo phrase hapo juu ndo imebeba ujumbe wa msingi ambao bado nautafakari sipati jibu!
 
Huyu mtu anaelekea kuwa na busara na akili nyingi. Lakini akili na busara za watanzania wengi huathiriwa na RUSHWA.

Huyu mzee nadhani yuko katika payroll ya Lowassa na hivyo akili na busara yake imeathiriwa kama walivyo wa TZ wengine.

Nimekuwa nikilalamikia gazeti la Tanzania Daima kwa jinsi wanavyomtetea lowassa kwa nguvu kubwa.ninachokiona na kukishuhudia,kinanifanya niseme ''politics is too serious a matter to be left to politicians''
 
Huyu mtu anaelekea kuwa na busara na akili nyingi. Lakini akili na busara za watanzania wengi huathiriwa na RUSHWA.

Huyu mzee nadhani yuko katika payroll ya Lowassa na hivyo akili na busara yake imeathiriwa kama walivyo wa TZ wengine.

Nimekuwa nikilalamikia gazeti la Tanzania Daima kwa jinsi wanavyomtetea lowassa kwa nguvu kubwa.ninachokiona na kukishuhudia,kinanifanya niseme ''politics is too serious a matter to be left to politicians''
nina wasiwasi na akili yako ambayo badala ya kujibu hoja umejikita kutukana watu kwa kujuifanya wewe ni mstaarabu.....sema ni nini ambacho jk amekifanya toka lowasa ametoka madarakani ambacho ni cha kukumbukwa
 
Huyu mtu anaelekea kuwa na busara na akili nyingi. Lakini akili na busara za watanzania wengi huathiriwa na RUSHWA.

Huyu mzee nadhani yuko katika payroll ya Lowassa na hivyo akili na busara yake imeathiriwa kama walivyo wa TZ wengine.

Nimekuwa nikilalamikia gazeti la Tanzania Daima kwa jinsi wanavyomtetea lowassa kwa nguvu kubwa.ninachokiona na kukishuhudia,kinanifanya niseme ''politics is too serious a matter to be left to politicians''
Kama dhamira, utashi na busara za huyu bw. makofia zinashindwa kumwezesha kubaini kuwa ilikuwa ni kosa kubwa kuiingiza nchi ktk biashara na kampuni hewa ya kufua umeme wakati wa dharura kama ile na tena kwa bei ya kuruka...kilichobakia ni kumwomba mungu amuepushe na ukengeufu na mtindio wa kufikiri.
 
Huyu mtu anaelekea kuwa na busara na akili nyingi. Lakini akili na busara za watanzania wengi huathiriwa na RUSHWA.

Huyu mzee nadhani yuko katika payroll ya Lowassa na hivyo akili na busara yake imeathiriwa kama walivyo wa TZ wengine.

Nimekuwa nikilalamikia gazeti la Tanzania Daima kwa jinsi wanavyomtetea lowassa kwa nguvu kubwa.ninachokiona na kukishuhudia,kinanifanya niseme ''politics is too serious a matter to be left to politicians''

my signature mtu wangu you can say that again...

Tanzania daima, wanahalisi wana mission moja! wahariri wao ni marafiki.

mwanahalisi lilimponda sana Lowassa, na Tz daima lina mfagilia sana Lowassa!

Mwanahalisi la JK, Tz daima la Chadema!

Ukiweza kutegua kitendawili kigumu hiki basi utapata jibu la mswali mengi sana.

I am still connecting dots........................................................................
 
my signature mtu wangu you can say that again...

Tanzania daima, wanahalisi wana mission moja! wahariri wao ni marafiki.

mwanahalisi lilimponda sana Lowassa, na Tz daima lina mfagilia sana Lowassa!

Mwanahalisi la JK, Tz daima la Chadema!

Ukiweza kutegua kitendawili kigumu hiki basi utapata jibu la mswali mengi sana.

I am still connecting dots........................................................................

Pamoja wote si wasafi
Lakini mimi namini demokrasia ya tanzania itakuwa ya kuchangamusha na kuchukuwa mwelekeo tofauti kabisa kama Lowasa akiwa mpinzani wa Kikwete.

Lowasa anaweza akabadilika na aka perform vizuri sana kama tu akigombea na jk na kumubwaga.
 
Back
Top Bottom