Lowassa Ataka Majina Ya Wadaiwa Sugu

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
885
Nileteeni majina ya wadaiwa sugu wa maji- Lowassa

15 Sep 2006
By Beatrice Bandawe, Kigoma

Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, ameziagiza Mamlaka za maji nchini, kumpelekea orodha ya wadaiwa wote sugu wa maji ifikapo mwisho wa mwezi huu, ili aweze kuwashughulikia na kuhakikisha wanalipa bili zao.

Alitoa agizo hilo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mamlaka za Majisafi na Majitaka Mijini, unaofanyika mjini hapa.

Alizitaka Mamlaka kuhakikisha wateja binafsi na taasisi mbalimbali, hususan taasisi za serikali ambazo zinadaiwa malimbikizo ya madeni ya ankara za maji zinalipa kwa wakati.

“Nileteeni orodha ya watu wote wanaodaiwa, mwisho wa mwezi huu nipatiwe, nitahakikisha madeni yote yanalipwa,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Alisema kila Mamlaka iorodheshe Wizara, Idara, Mikoa na Taasisi zote za Serikali zenye madeni sugu ya huduma za maji ili kila Ofisa Mhasibu aweze kuwajibika kwa kueleza sababu za kutolipa madeni hayo.

Bw. Lowassa aliagiza kuwa ili kuzifanya mamlaka kuwa endelevu ni lazima kutilia mkazo ukusanyaji madeni yake yatokanayo na huduma za maji safi na maji taka.

Akizungumzia hali ya maji nchini, Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi waishio mijini ni milioni nane ambapo zaidi ya asilimia 70 wanaishi katika maeneo yasiyopimwa.

Aidha, alisema madeni ya mamlaka yamepungua kutoka Sh bilioni 5.091 hadi Sh. bilioni 3.02 na wastani wa saa za kutoa huduma umeongezeka kutoka saa 16 hadi saa 18.

Mkutano huo wa siku tatu, unawashirikisha washiriki 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi, wakiwemo wataalam kutoka Benki ya Dunia, DAWASA, DAWASCO na EWURA.

Wakati huo huo, mwandishi wetu Apolinary Kweka anaripoti kuwa, Waziri Mkuu, ameikataa taarifa ya maendeleo ya Wilaya ya Kigoma Mjini kwa maelezo kuwa, imepitwa na wakati.

Bw. Lowassa alifanya hivyo kwa kumkatisha Mkuu huyo wa wilaya, Bw. John Mongella kuendelea kuisoma taarifa hiyo.

Aidha, aliwatuhumu watendaji wa mkoa akiwemo Ofisa Tawala Bw. Martin Mgongolwa kwa kushindwa kumsaidia Mkuu huyo mpya wa Wilaya.

Alifikia hatua ya kuikataa taarifa hiyo wakati akimsomea kipengele kinachohusu zao la mchikichi.

Huku akionyesha kukasirishwa na taarifa hiyo, Bw. Lowassa alisema taarifa hiyo imepitwa na wakati kwa maelezo kuwa, haiendani na waliochokubaliana huko Ngurdoto kuhusu kuweka mipango madhubuti ya kuboresha kilimo nchini.

`Hakuna taarifa kwani imepitwa na wakati kwa kuwa haiendani na makubalino ya Ngurdoto,” alisema Waziri Mkuu.

Mapema, akianza kusoma taarifa hiyo, Bw. Mongella alisema wilaya yake inayo wataalamu wawili wa zao la kahawa akiwemo mwenye ngazi ya Shahada.

Alisema huyo mbali na mwenye shahada anahudumia maeneo yanayolima kahawa.

Alisema mtaalamu huyo yupo peke yake huku akiwa hana zana wala vitendea ukiwemo usafiri.

Alieleza matatizo mengine yanayowakabili wakulima kuwa ni pamoja na ukosefu wa pembejeo na uwezi mdogo wa wakulima kuzalisha zaidi zao hilo.

Alisema wilaya inayo mpanga wa kusambaza miche bora pamoja kujenga kiwanda cha kukobolea kahawa.

Alisema hivi sasa wanazalisha tani 614 kwa mwaka.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu, amechangia jumla ya Sh. milioni nne kwa ajili ya vikundi viwili vya SACCOS katika kata ya Gungu.

Vikundi hivyo vya SACCOS ni Kino chenye wanachama 60 na Nyakageni chenye wanachama 106.

Aliahidi mchango huo kwa vikundi vya Nyakageni na Kino mara baada ya kukagua vikundi vya ukaushaji wa dagaa vilivyoko eneo la Kibirizi mjini hapa.

Waziri Lowassa pia alikabidhi mikopo kwa wawakilishi 10 wa vikundi hivyo mikopo yenye thamani ya Sh. 100,000 SACCOS.

Pia, Bw Lowassa aliagiza daraja la Kibirizi kujengwa mara moja kuanzia wiki ijayo ili kuwaondolea wananchi usumbufu.

Alitoa agizo hilo baada ya wananchi kutoa kero zao kuhusu daraja hilo ambalo baada ya kukatika halijajengwa.Daraja hilo litagharimu Sh. milioni 115.

Mapema akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara, Waziri wa Miundo mbinu Bw. Basil Mramba aliwatangazia wananchi hao kuwa serikali inayo mpango wa kujenga barabara ya Mwanga hadi Ujiji kwa kiwango cha lami.

Alisema kazi hiyo itafanyika mwaka ujao.Alisema hivi sasa serikali inakarabati uwanja wa ndege wa Kigoma ili ndege kubwa ziweze kutua.

Kadhalika, alisema kuwa itakabarabati na kujenga kwa kiwango cha lami
Bw.Lowassa katika ziara yake anatumia mtindo wa kutoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali au kueleza kero zao.

Alifanya ziara pia katika wilayani Kasulu ambako alipokea taarifa ya utendaji wa wilaya hiyo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Waziri Mkuu Bw.Lowassa anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Kigoma Mjini.

* SOURCE: Nipashe

HIVI HUYU SI ALIKUWA WAZIRI WA MAJI JUZIJUZI TU?AU WAKATI HUO ASINGEWEZA KUIFANYIA KAZI ORODHA KAMA HII ANAYOOMBA?AU TUSEME WAZIRI MWENYE DHAMANA YA MAJI AKIOMBA ORODHA HIYO HATOPEWA,KWANINI HAJAOMBA,KAMA HAJAOMBA ANAFANYA NINI MADARAKANI?
HAPA KUNA UWEZEKANO UFUATAO:
1.HUYU MMASAI ANAINGILIA MADARAKA YA WAZIRI HUSIKA (IT DOESN'T NEED A PRIME MINISTER KUWAKUMBUSHA WADAIWA SUGU WA MAJI KULIPA MADENI YAO)
2.WAZIRI HUSIKA NI MZEMBE HADI INAMLAZIMU WAZIRI MKUU AINGILIE JUKUMU LA KAWAIDA LA WAZIRI HUYO.
3.MAMLAKA HUSIKA HAZINA NGUVU KISHERIA KUWALAZIMISHA WADAIWA SUGU KULIPA MADENI
4.WAZIRI MKUU ANAINGILIA "UTARATIBU" WALIOJIWEKEA MAMLAKA ZA MAJI WA KUDAI BILI PALE TU WANAPOJISKIA WAO...BY THE WAY,SIO HIZO BILLS NDIO ZINAWALIPA MISHAHARA.SO,KAMA HAZILIPWI NA ZINAWAATHIRI MBONA HAWACHUKUI HATUA (WAHENGA WALISEMA MWENYE NJAA HALAZIMISHWI KULA)
5.UBABAISHAJI,MORE UBABAISHAJI,AND EVEN MORE UBABAISHAJI.Except,TAFITI THEN JADILI is likely,as usual,to defend LOWASSA.
 
mazingaombwe...viinimacho...na mazingaombwe zaidi!!! halafu miezi michache ijayo.. Rais Kikwete atasema "Nileteeni orodha ya wadaiwa sugu" na gurudumu la mazingaombwe litaendelea kuzunguka!
 
Nimefuatilia erikali hii most of the time ni Raisi na waziri wake mkuu ndio wanaovuma. Mawaziri wao wanafanya nini? au ndio kutafuta cheap populalarity? kampeni zilishapita kitambo na sasa ni muda wa kufanya kazi. By the way what is the use of having a big cabinet?
 
hapo ndipo huyo JK na PM wake wanapochemsha

kwani hao jamaa wa kuzuia RUSHWA kazi yao ni nini au ndio wanataka kungangania kuwa kwenye headlines?
 
Lowassa ni mtu wa pupa, hajatulia kimawazo na kimaamuzi. mfano mdogo suala la mvua ya kutengeneza kule Thailanda.

kwasababu ya pupa, akashindwa kujiuliza swali dogo: kwanini mvua za kutengeneza hazijatumika katika mataifa yanayokabiliwa na ukame wa mara kwa mara kuliko sisi watanzania?

kwasababu ya pupa, akashindwa kuuliza ni nini athari za kemikali za mvua ya kutengeneza katika viumbe[wanyama, wadudu, mimea] pamoja na udongo wa eneo itakaponyesha.

kwasababu ya pupa, Lowassa amewakaribisha watailand kuja kutufanya guinea pigs wa utafiti wao.
 
Serikali hii usanii mtupu.....Lakini wasanii hawako huko juu tu. Wengine tunao mitaani na wataibuka muda si mrefu kumtetea mheshimiwa Lowasa. Ama kweli ni ujuha mtupu.
 
Hii ni serkali yakina Mr. Misifa,wana uchu mkubwa wa kuandikwa magezetini kila kukicha! Mpaka sasa hawajaipa nchi muelekeo wowote zaidi ya kugusa masuala madogo madogo kuendelea kuvuna sifa.

Kukitokea matatizo ya kiutendaji utasikia nileteeni mimi, nipeni orodha!! Badalu ya kurekebisha mambo? kuwajibisha wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao mtu anadai nileteeni orodha? Ataziomba ngapi? za Wizara ngapi? Hata kocha mchezeji hayuko hivyo! Hii serekali ni show game tupu!
 
Lowassa ni mtu wa pupa, hajatulia kimawazo na kimaamuzi. mfano mdogo suala la mvua ya kutengeneza kule Thailanda.

kwasababu ya pupa, akashindwa kujiuliza swali dogo: kwanini mvua za kutengeneza hazijatumika katika mataifa yanayokabiliwa na ukame wa mara kwa mara kuliko sisi watanzania?

kwasababu ya pupa, akashindwa kuuliza ni nini athari za kemikali za mvua ya kutengeneza katika viumbe[wanyama, wadudu, mimea] pamoja na udongo wa eneo itakaponyesha.

kwasababu ya pupa, Lowassa amewakaribisha watailand kuja kutufanya guinea pigs wa utafiti wao.

Hilo la pupa hukukosea kabisaa
 
Siwaelewi waTZ mh lowasa alikuwa anatekeleza wajibu wake sasa mnampinga nini nyie ndio wachawi wa nchi hii na mh lowasa angeendelea na uwaziri mpaka Leo tungekuwa mbali sana
 
Siwaelewi waTZ mh lowasa alikuwa anatekeleza wajibu wake sasa mnampinga nini nyie ndio wachawi wa nchi hii na mh lowasa angeendelea na uwaziri mpaka Leo tungekuwa mbali sana

Wazembe walimuogopa sana huyu mtu!!
 
Back
Top Bottom