LOWASSA atajwa sababu ya deni la milioni 1 mbele ya Mkuu wa Mkoa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,413
2,000
Jina la Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa limetajwa na mkazi mmoja wa Mbeya mbele ya Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makala kuwa sababu ya deni la shilingi milioni moja kutokana na mapenzi ya wafuasi wake

Mkazi huyo wa Kata ya Ruanda Nzovwe aliyejitambulisha kwa jina la Amos Mwakyambiki alidai kuwa wafuasi wa Chadema waliharibu paa la nyumba yake walipopanda kwa lengo la kufuatilia mkutano wa Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana na kwamba chama hicho kilimuahidi kumlipa fidia ya shilingi milioni moja lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa

Alimueleza mkuu wa mkoa huo kuwa kutokana na uharibifu huo mkubwa uliofanyika, wapangaji wake waliamua kuhama nyumba yake hivyo kukosa kipato

"Naomba Serikali ya Mkoa inisaidie kuzungumza na Meya (wa Chadema) ili niweze kulipwa stahiki zangu kwani sasa sijui hatma yangu. Kuku niliokuwa nauza kwa ajili ya kupata nauli kwenda ofisi za jiji wamekwisha". Mkazi huyo alikaririwa

Kutokana na madai hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimuagiza Mkuu wa Wilaya kufuatilia suala hilo huku akitahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya nyumba zao wakati wa kampeni

"Lakini na nyie wananchi msikubali nyumba zenu zibadilishwe kuwa viwanja vya siasa"alisema Makala

Akizungumza taarifa hizo, Mkuu wa idara ya Habari ya Chadema, Tumaini Makele, alisema kuwa Chama hicho kinafuatilia kuona ni nani aliyetoa ahadi hiyo kwa Mwananchi huyo na ilikuwa katika mazingira gani ili walifanyie kazi ipasavyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom