Ukosefu wa ajira kwa Vijana: Lowassa atabiri vita Tanzania...

Lowasa is very intelligent politically.

Now anataka kutumia mtaji wa vijana. Kama mwanasiasa anataka tuamni kuwa yuko very concened na "vijana".

VIpi Kuhusu wazee amabao walitumikia serikali na makampuni binafsi na pension zao wanazopata sasa wanaishi maisha ya ajabu. Au sababu wazee hawana uwezo wa kurusha mawe.

Labda walio karibu yake wamuulize hilo bomu la ajira kwa vijana limeanza hasa kutengenzwa mwaka gani?
"Mtupa ganda la ndizi husahau lakini anayelikanyaga hasau".
Ikiwa Lowasa amesahau alivyochangia kuiuza nchi, kuifisidi na kuifakirisha, wananchi hatusahau. Mwacheni aimbe, ruhsa!
 
Mimi tatizo langu ni hawa wansiasa wanajifanya wako concerned na vijana lakini wakifika mjengoni tofauti

Mimi ila siku nauliza
kwa nini mbunge(mwanasiasa ) anamzidi kimapato watu wenye majukmu makubwa zaidi kieneo na kumuhimu kama

  • Afisa kilimo wa mkoa, na hata wilaya
  • Afisa Mifugo wa mkoa au wilaya
  • Mganga mkuu (afya) wa wilay au mkoa
  • Afisa Elimu wa Mkoa au wilaya
  • Mhandisi wa Mkoa au wilaya
  • Afisa Maji wa mkoa au wilaya
  • Afisa Nyuki
  • Afisa Teknohama wa mkoa au wilaya( kama wapo)
Hivi kuna mbunge anaweza kumuhoji kwa ukali afisa elimu kuhusu mambo ya elimu duni wilayani au mkoani kwake au inabidi afyate mkia sababu anajua kila kitu ni siasa na hana cha kuhoji.? Kwa nini hatusikii wabunge/ mawaziri wakitaka watu wenye majuumu makubwa zaidi yao wapate mishahara zaidi yao? Kwa nini kijanaiwe vigumu kuwa afisa elimu wa kasulu lakini iwe rahisi kuwa mbunge.
Wanasiasa wajifunze hata huko maju wanapokwenda waulize mapato ya watendaji na wanasiasa yakoje.

Baadaye anakuja mtu kama samuel siita Mkoa wa tabora una mbao na misitu na vijana mafundi Lakini ofisi ya mbunge ambayo haitumii hata kwa siku 30 samani(furniture) zake zote zimetoka dar na dar wamezitoa china. Sasa mwansiasa kama huyu atasema anafikria ajira za vijana !!!!!!!!

Lowasa, CCM , JK , mhhhh kazi tunayo mana hata wapinzani nao hawajipanga linapkuja suala la maslahi ya taifa.
 
Asante......its True.....lakn hiyo ya kungátuka ni kama ndoto.Sio utamaduni wa kiafrika...Mara nyingi huwa wanasubiri damu imwagike kwanza.Tuombe Mungu atunusuru WaTZ waendelee kuwa wapole

Mungu ametupatia wanadamu utashi, sasa kama hatutaki kutumia utashi wetu ni kweli tutafika pa baya na tukisha fika tusimlilie Mungu. kwanza Mungu anayo mengi ya kufanya na alisha tufanyia mengi , sisi tumefanya nini japo kwaajili yetu?
tazama Tanzania ya leo, mbunge anakwenda kwenye kesi yake mahakamani wananchi wanamfuata nyuma, kwa nini hili linatokea? ni mbunge wao amewaita? la- hasha . hii ni kwa sababu vijana wenye nguvu hawana kazi za kuwafanya wasiwe na muda wa kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge wao. Tazama kule mbeya wafanya biashara ndogo wamebishana na polisi , hata polisi mikoa jirani wakaja kusaidia , na hatimaye askari jeshi, kwanini viijana wanafanya haya , ni kwa sababu hawana kazi, hawana security. vyuo vikuu imekuwa kawaida kwa wanavyuo kugoma na kuandamana- wanafahamu maisha yalivyo magumu kwa kijana wa leo wa kitanzania

kama tungelikuwa na sera nzuri za kusimamia njia za uchumi vizuri , hawa vijana wasingepata muda wa kushinda mahakamani pale mbunge wao akienda kwenye kesi zake , au wasingepigana na polisi. ni kweli chumi nyingi duniani zimeyumba, tunafahamu mambo ya cuts huko ulaya hususani ugiriki, italia na hata uingereza, hayo ni lazima yatatuathiri, kwani nasi uchumi wetu ni tegemezi.

nilitarajia wakati huu wakuu wetu wa nchi watangaze kujifunga mkanda, wananchi waambiwe ukweli, wajue tupo ktk kipindi kigumu ki maisha. watu wajibane wapunguze matumizi. chaajabu serikali yetu haitaki hata kuzungumzia hili. wakati tunaona hata tusio wachumi jinsi shilingi inavyo yumba, mfumuko wa bei na hata uhaba wa bidhaa muhimu kama mafuta na nishati kwa ujumla. serikali iliyo makini inachofahamu yenyewe ni kuwa kama wananchi wameandamana, basi wametumwa na wanasiasa, inafahamu ukweli lakini inakwepa kuuzungumza kwa wananchi wake. lakini kukwepa kuzungumza matatizo tuliyo nayo ni kutengeneza mwanzo wa mwisho.

sasa leo kila anae kemea ovu anaambiwa anataka uraisi, au kila anayedai haki anaambiwa katumwa na wanasiasa. ivi hii serikali isiyojua wajibu wake , ipo kwaajili ya nani? ndiyo hapo watu wanafikia kusema serikali ijiuzulu, kuleta hali ya matumaini na kuepusha huu ninao uita mwanzo wa mwisho.
 
Lowasa amekuwa serikalini tangu mwanzoni mwa miaka ya 90 amesha fanya nini kuepusha hilo la ajira za vijana ? zaidi yakufisadi Richmond na mikataba feki hata ya mvua za kutengeneza Ashindwe na alegee
 
Hao wanaojali ajira za vijana
  • Hata mashsati na vipeperushi vya uchaguzi utakuta vinatengenezwa china tena bila aibu wala kificho. Na hawaoni Tatizo.........
  • Hata CDM sijui magwanda yao japo seti chache ni kiwanda gani/ mwanamitin gani wa Tanzania anayategeneza.....
Hivi wanasiasa wanajua wachina wenyewe wangekuwa watu wa kusema bidhaa zao hazina quality basi wangejikuta wanakuwa mateja wa bidhaa za wenzao mpaka kesho.
 
Kwa kweli kuna watu humu likitajwa jina la Lowassa huripuka kama moto wa Petroli. Badala ya kuchangia kwa fikra pevu wao hutanguliza ushabiki mbele na Jaziba pamoja na Munkari. Lowassa ni mwanasiasa mwenye mikakati kuliko wengi wetu tunavyofikiri. Alipokuwa waziri wa Ardhi kwa kauli yake watu tulivamia pale kwenye bustani ya Mnazi mmoja na kung'oa mabati yaliyokuwa yamewekwa kama uzio kwa ajili ya kufanyika kwa ujenzi wa ghorofa kwenye bustani ile.

Kama si juhudi za Lowassa inawezekana kabisa ile bustani leo hii isingekuwepo. Lowassa ni mchapakazi lakini ana dosari nyingi sana zinazoondoa sifa za yeye kuwa kiongozi mkuu wa taifa hili. Lakini sote kwa bayana au kwa chini chini tunakubali kwamba Lowassa ni mwanamkakati aliyebobea kwenye siasa za Tanzania.

Mwaka 1995 sisi tuliokuwepo tunajua ni yeye ndiye aliyemtanguliza Kikwete baada ya kujua kwamba yeye na Nyerere "haziivi" kwa hiyo haitakuwa rahisi kwake kukubaliwa kugombea nafasi ya Urais. Kawaulize kina Sukwa Said Sukwa na Mwenzie John Guninita ushawishi wa Lowassa ulivyowafanya wavue mashati ya Kijani baada ya Kikwete kushindwa na Mkapa.

Naona badala ya kuongea kwa hisia basi sote kwa pamoja tuwe na mkakati wa kumzuia Lowassa kwani "mbabe" pekee tuliyekuwa tunamtegemea na aliyekuwa na uwezo wa kumwambia Lowassa "hatuchagui Kiongozi kwa uzuri wa sura yake" ameshatangulia mbele ya haki!!
 
Wana JF, Ngoja niwakumbushe kitu kimoja. Katika imani ya Kikristo, na kwa kufuata maandiko matakatifu ya Biblia, Mwenyezi Mungu amejiwekea utaratibu ambao ni mgumu sana kwa sisi binadamu wa kawaida kuukubali na kuupokea, nao ni huu. Kusamehe na kusamehewa. Biblia inasema, kwa mkosaji yeyote, hata ukiwa na dhambi kubwa kiasi gani, au umetenda maovu makubwa kiasi gani, ukiungama kwa Mungu kwa kweli na dhati, unapata msamaha palepale. Lakini kwa Binadamu kusamehe binadamu mwenzake ni ngumu mno. Sasa basi, Kama EL ameungama madhambi yake basi atakuwa amepata msamaha wa Mungu, basi na atoke waziwazi na kweupe na kuwaomba radhi Watanzania kwa yale anayohusishwa nayo na hapo wapo watakao msamehe na wapo watakao kuwa na roho ngumu kusamehe, lakini kwake atakuwa ametua mzigo. Kazi kwa EL na kwetu wenyewe kutekeleza hilo. Natoa Hoja.
 
Lowasa is very intelligent politically.

Now anataka kutumia mtaji wa vijana. Kama mwanasiasa anataka tuamni kuwa yuko very concened na "vijana".

VIpi Kuhusu wazee amabao walitumikia serikali na makampuni binafsi na pension zao wanazopata sasa wanaishi maisha ya ajabu. Au sababu wazee hawana uwezo wa kurusha mawe.

Labda walio karibu yake wamuulize hilo bomu la ajira kwa vijana limeanza hasa kutengenzwa mwaka gani?

mzee una akili nyingi sana,hii yako nimeipenda sana sana,huyu jamaa ni mjanja mjanja,huwa anasoma alama za nyakati na kujichanganya,si unakumbuka yale maandamano ya waarabu wa egypt,tunisia n.k.nae alijichanganya akadai ni haki yao na kuseama eti viongozi wa afrika waache kulimbikizia mali!!!!!!watu tukajiuliza hivi hili la kujilimbikizia mali analitamka lowassa au labda tunaota pengine ni mzimu wa marehemu sokoine???lakini mzee wangu yule akawa serious pale kwenye kioo cha taifa tbc tv ametoa macho anasisitiza kauli yake hiyo!!!lowassa mjanja sana sijui hata ile "ajali" ya kisiasa ilimpata pata vipi na ujanja wake wote huu wa kucheza sarakasi za kisiasa!
 
Wana JF, Ngoja niwakumbushe kitu kimoja. Katika imani ya Kikristo, na kwa kufuata maandiko matakatifu ya Biblia, Mwenyezi Mungu amejiwekea utaratibu ambao ni mgumu sana kwa sisi binadamu wa kawaida kuukubali na kuupokea, nao ni huu. Kusamehe na kusamehewa. Biblia inasema, kwa mkosaji yeyote, hata ukiwa na dhambi kubwa kiasi gani, au umetenda maovu makubwa kiasi gani, ukiungama kwa Mungu kwa kweli na dhati, unapata msamaha palepale. Lakini kwa Binadamu kusamehe binadamu mwenzake ni ngumu mno. Sasa basi, Kama EL ameungama madhambi yake basi atakuwa amepata msamaha wa Mungu, basi na atoke waziwazi na kweupe na kuwaomba radhi Watanzania kwa yale anayohusishwa nayo na hapo wapo watakao msamehe na wapo watakao kuwa na roho ngumu kusamehe, lakini kwake atakuwa ametua mzigo. Kazi kwa EL na kwetu wenyewe kutekeleza hilo. Natoa Hoja.

Hapa unajaribu kumpigia mbuzi gitaa..we mtu mpaka leo yeye haamini kama aliwahi kufanya makosa yeyote zaidi ya kulia lia kwamba issue ilikua ni uwaziri mkuu "wake" na hata akirudishwa leo madarakani atarudia madudu yale yale,sasa unataka aungame kitu gani,mtu kakaa chini lakini bado anaamini kwamba amesimama utamsaidia vipi ili ainuke!mwacheni aendelee kuamini kasimama wakati wote tunamuona amekaa chini au amachuchumaa!
 
Kwa kweli kuna watu humu likitajwa jina la Lowassa huripuka kama moto wa Petroli. Badala ya kuchangia kwa fikra pevu wao hutanguliza ushabiki mbele na Jaziba pamoja na Munkari. Lowassa ni mwanasiasa mwenye mikakati kuliko wengi wetu tunavyofikiri. Alipokuwa waziri wa Ardhi kwa kauli yake watu tulivamia pale kwenye bustani ya Mnazi mmoja na kung'oa mabati yaliyokuwa yamewekwa kama uzio kwa ajili ya kufanyika kwa ujenzi wa ghorofa kwenye bustani ile.

Kama si juhudi za Lowassa inawezekana kabisa ile bustani leo hii isingekuwepo. Lowassa ni mchapakazi lakini ana dosari nyingi sana zinazoondoa sifa za yeye kuwa kiongozi mkuu wa taifa hili. Lakini sote kwa bayana au kwa chini chini tunakubali kwamba Lowassa ni mwanamkakati aliyebobea kwenye siasa za Tanzania.

Mwaka 1995 sisi tuliokuwepo tunajua ni yeye ndiye aliyemtanguliza Kikwete baada ya kujua kwamba yeye na Nyerere "haziivi" kwa hiyo haitakuwa rahisi kwake kukubaliwa kugombea nafasi ya Urais. Kawaulize kina Sukwa Said Sukwa na Mwenzie John Guninita ushawishi wa Lowassa ulivyowafanya wavue mashati ya Kijani baada ya Kikwete kushindwa na Mkapa.

Naona badala ya kuongea kwa hisia basi sote kwa pamoja tuwe na mkakati wa kumzuia Lowassa kwani "mbabe" pekee tuliyekuwa tunamtegemea na aliyekuwa na uwezo wa kumwambia Lowassa "hatuchagui Kiongozi kwa uzuri wa sura yake" ameshatangulia mbele ya haki!!

Lowassa kweli ni mtendaji mashuhuri,mi nadhani kwa utendaji wake huo uliotukuka lowassa anagefaa awe waziri,tena sio waziri mkuu,waziri wa wizara yeyote korofi,ataiweza sana,tukimpeleka ikulu tutaukosa utendaji wake!
 
Hata hili swala la katiba linaweza kuleta vurugu na hata vita. Ndugu zangu TISS mshaurini mjomba vizuri
 
Askofu Makungu alisema, vitendo vya kulalamika lalamika ama kwa kuilalamikia Serikali, ofisa, kiongozi au mtu fulani huo ni sawa na ufedhuli mtupu, na kwamba Watanzania waache kusonta vidole watu, ili taifa liweze kupata taranta kutoka kwa Mungu.

Hata hivyo, alisema ujio wa Lowassa katika harambee hiyo ni mzuri sana, na alisema kwa vile kanisa hilo limejengwa kwa tofali moja moja, basi na waumini wa kanisa hilo watakuwa tofali moja moja kwa Lowassa.

This is not right!!

Yaani nchi yetu imefilisika namna hii mpaka watu kawa Lowassa anaanza kuonekana anafaa mbele ya macho ya kanisa katoliki na waamini wake?

Waamini watakua tofali moja moja kwa Lowassa ili iweje?!
 
Lowassa kweli ni mtendaji mashuhuri,mi nadhani kwa utendaji wake huo uliotukuka lowassa anagefaa awe waziri,tena sio waziri mkuu,waziri wa wizara yeyote korofi,ataiweza sana,tukimpeleka ikulu tutaukosa utendaji wake!

Alishawahi kuwa waziri katika wizara zaidi ya 3; alifanya nini huku mpaka useme ni mtendaji mashuhuri?
 
Hadi Lowassa atakapoanza kukizungumzia CCM hapo tutaanza kuelewana. So far kuzungumzia "serikal" ni kujaribu kuchezeshea mchezo wa 'doli doli.. shilingi ya Nyerere katikati ina mwenge...'
 
Kwa kweli kuna watu humu likitajwa jina la Lowassa huripuka kama moto wa Petroli. Badala ya kuchangia kwa fikra pevu wao hutanguliza ushabiki mbele na Jaziba pamoja na Munkari. Lowassa ni mwanasiasa mwenye mikakati kuliko wengi wetu tunavyofikiri. Alipokuwa waziri wa Ardhi kwa kauli yake watu tulivamia pale kwenye bustani ya Mnazi mmoja na kung'oa mabati yaliyokuwa yamewekwa kama uzio kwa ajili ya kufanyika kwa ujenzi wa ghorofa kwenye bustani ile.

Kama si juhudi za Lowassa inawezekana kabisa ile bustani leo hii isingekuwepo. Lowassa ni mchapakazi lakini ana dosari nyingi sana zinazoondoa sifa za yeye kuwa kiongozi mkuu wa taifa hili. Lakini sote kwa bayana au kwa chini chini tunakubali kwamba Lowassa ni mwanamkakati aliyebobea kwenye siasa za Tanzania.

Huo uchapakazi wake umeinufaisha vipi Tanzania?

Hili suala la uchapakazi wa Lowassa sasa ni just a constructed reality!!!!
 
WanaJF,

katika hili la Lowasa nasikitishwa sana na viongozi wa dini kuendelea kumsafisha kwa nguvu zao zote bila ya Mtu huyu kutueleza ushiriki wake ktk mambo haya ya ufisadi anayohusishwa nayo.....viongozi wa dini tulikuwa naoo mpaka hivi majuzi kuupinga ufisadi pamoja na mafisadi lakini leo naona wananchi tunaongea lugha tofauti na viongozi hawa wa dini.

Kuna kipindi mafisadi walihusishwa na kuingilia uchaguzi wa kiongozi mkuu wa KKKT pale bagamoyo,na Askofu Malasusa alilalamika hadharani kuwa watu wasio wakiristo wanataka kutuchagulia viongozi and its good walishindwa kutimiza malengo yao.....

siku za hivi karibuni tumeona Lowasa akiongozana na Mkuu wa BAKWATA wakielekea kigamboni ambako inasemekana ametoa ufadhili katika shule ya Waislam....baadaye tukaona ndugu huyu akiwa na Askofu Mokiwa kule Anglikana kwenye maharambee ya kujenga majengo kwa ajili ya kanisa(be reminded kanisa siyo jengo ni watu waliomwamini Mungu)....leo tena ameonekana Mwanza kwenye harambee tena za ujenzi wa kanisa.
Viongozi wa dini wanapoteza ushawishi wao katika jamii kwa kasi sana...ushawishi walio nao ulijengwa kwa muda mrefu sana ila wao wanataka kuugaragaza kwa muda mfupi sana, hawawezi kutuambia ufisadi ni mbaya ila peas za mafisadi ni nzuri na zinafaa kujengea majengo ya makanisa!!!!!

Mipango ya Lowasa kushiriki au kuongoza harambee hizi yanaratibiwa na wafuasi wake ambao wamo makanisani pia na kinachonisikitisha zaidi ni Upofu wa viongozi wa dini kuruhusu ruhusu tu kila mtu kuchangia ujenzi wa jengo la kanisa. RC nilikuwa nawaamini sana kuhusu kipengele hiki,niliwahi kuambiwa kuwa huko nyuma ilikuwa hairuhusiwi mtu mmoja kutoa pesa za kujengea kanisa ili kuacha mwanya kwa watu wengi kushiriki ujenzi wa jengo la kanisa na hata ukitoa pesa hiyo walihahakisha wanaigawa sehemu ndogo iingie kwenye ujenzui na nyingine iingie kwenye kusaidia wenye uhitaji...lakini leo wamenaswa pia kwenye mtego wa Mafisadi.!!!

Tunaambiwa akina Bashe walikuwepo kwenye kuratibu ziara ya Mwanza ,watu ambao siyo waRC wanawezaje kuwa na uchungu wa kujenga jengo la kanisa???

Kuhusu utendaji wake , i mean Ndugu Lowasa ni sawa na mimi naona sehemu ya wajibu wake tu, watu wanao kaza misuli kumsifia as if alifanya something extra ordinary ni wanafiki na watumishi wa matumbo yao na actually matumbo ndo yanatumika kufikiri kwa ajili yao. Lowasa anaonekana alikuwa mtendaji kwa kuwa analinganishwa na Failures wenzie ndani ya sisieMu na si vinginevyo, hata mikataba mnayosema alivunja nachelea kusema inawezekana alivunja kwa interest binafsi na sio taifa....mbona tunakumbuka aliyoyafanya Masaki/Oysterbay! alipobomoa construction ya wawekezaji ili yeye afanye biashara.

yapo mengi yanayosikitisha kuhusu huyu bwana Mkubwa, leo anabebwa directly na watu kama Rostam mtu ambaye tunajuta kuwa naye kama Mtanzania and yet kuna wavivu wa kufikiri wanamuona kama anaweza kuwachagulia Rais bora.....Rostam anajitapa kupitia media kuwa ameitajirisha Igunga kumbe ndo wilaya iliyo na watu wengi wasio jua kusoma na kuandika, barabara za kuunganisha kata hakuna ...je vijiji? watu wanakunywa maji machafu dunia nzima halafu watu wachache wanaofaidi ufisadi wake wanamtetea eti ni Mkombozi....Watu mnao tetea ufisadi na mafisadi ili mpate kuishi, kuishi kwenu kuko mashakani mpaka mtakapo jua kujitegemea kwa kufanya kazi halali na kuwa huru vichwani mwenu.

Mungu iepushe nchi hii na balaa la watu wenye uchu wa fedha kama hawa!!!!

Amen.
 
EL amesema hayo mwanza alipokua mgeni rasmi kuchangia kanisa katoliki, kukosekana kwa ajira kwa vijana ni bomu linalotarajia kulipuka wakati wowote hivyo kusababisha vita nchini. Kuna vijana 2.5m wasio na ajira! ========== UPDATED: Na mwandishi wa FikraPevu.com Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (MB), amesema kwamba, amani iliyopo hapa nchini ipo mashakani kutoweka, kutokana na wimbi kubwa la vijana kutokuwa na ajira maalumu, hivyo Serikali inapaswa kuweka mikakati madhubuti ya kuzalisha ajira nyingi kwa vijana. Amesema, kati ya nguvu kazi ya taifa inayokadiriwa kufikia milioni 25 kwa sasa, kati yake milioni 17.5 ni vijana ambao kimsingi wanakabiliwa na ukosefu wa ajira maalumu, jambo ambalo Serikali inapaswa kulipatia ufumbuzi haraka sana ili kulinda amani ya nchi isiyumbe au kutoweka kabisa. Lowassa, aliyasema hayo leo Jijini Mwanza, wakati alipokuwa akizungumza kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa Katoliki, Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu la Mwanza. Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa alisema, hali hiyo inachangiwa na uchumi duni wa nchi ikiwa ni pamoja na sera mbovu za elimu zisizozingatia uhitaji wa soko la ajira na vijana wengi kutotaka kuchukuwa masomo ya sayansi na hisabati ambayo yana fursa kubwa ya kupata ajira. Kiongozi huyo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyokusanya sh. milioni 200 na kuvuka lengo la sh. milioni 120, alisema kwa sasa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hapa Tanzania limefikia zaidi ya asilimia 30, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 21 wa tatizo hilo linalozikumba nchi zote za Bara la Afrika. "Siku zote nimekuwa nikisema nchi yetu inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana. Hali hii isipopatiwa ufumbuzi na Serikali, amani ya nchi yetu inaweza kuyumba. "Kati ya vijana 850,000 wanaoingia kwenye soko la ajira baada ya kumaliza masomo yao ya msingi, sekondari na vyuo, ni asilimia tano tu ndiyo wanapata ajira katika sekta rasmi isiyo ya kilimo. Na hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu", alisema Lowassa ambaye alichangia sh. milioni 11 katika harambee hiyo. Kwa mujibu wa Lowassa ambaye alionekana kushangiliwa kila wakati pale jina lake linapotajwa, vitendo vya rushwa vinavyoonekana kuota mizizi katika sehemu za utoaji ajira rasmi Serikalini na kwenye taasisi za umma, ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo kama hayo. Sababu nyingine alizozitaja Lowassa zinazochangia kukosekana kwa ajira kwa vijana nchini ni pamoja na sera mbovu za ajhira na mitaala ya elimu isiyokidhi mahitaji ya soko la ajira Bara la Afrika na duniani kwa ujumla. "Kutozingatia mabadiliko ya kiuchumi, kibiashjara, kisiasa, kijamii na kiteknolojia nchini, Afrika Mashariki, Afrika na dunia nzima ndiyo inayozalisha yote haya mabaya", alisema Lowassa ambaye alionekana kuwa kivutio kikubwa kwenye harambee hiyo. Awali, Makamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Askofu Richard Makungu aliwaonya watu wanaowanyooshea vidole wenzao, na kusema vitendo hivyo si vizuri hata kidogo, kwani watu hao wakichunguzwa nao wana mabaya yao, na wala hata choo majumbani mwao hawana kabisa. Askofu Makungu alisema, vitendo vya kulalamika lalamika ama kwa kuilalamikia Serikali, ofisa, kiongozi au mtu fulani huo ni sawa na ufedhuli mtupu, na kwamba Watanzania waache kusonta vidole watu, ili taifa liweze kupata taranta kutoka kwa Mungu. Hata hivyo, alisema ujio wa Lowassa katika harambee hiyo ni mzuri sana, na alisema kwa vile kanisa hiolo limejengwa kwa tofali moja moja, basi na waumini wa kanisa hilo watakuwa tofali moja moja kwa Lowassa.

kaka makamu wa askofu sio askofu..... richard makungu ni padri na ndo makamu wa askofu (kwa lugha ya kigeni wanamwita Vicar General) yeye sio askofu naona umeamua kumtabiria......usije ukachanganya na askofu msaidizi kana ilivyo bukoba na Dar es Salaam
 
Muhimu ameanzisha mjandala wenye umuhimu mkubwa kwa taifa letu badala ya kukakalia kujadili mijadala ya kipuuzi kama ushoga na kujivua gamba!
 
Back
Top Bottom