Lowassa asimikwa kiongozi wa kimila wa wamasai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa asimikwa kiongozi wa kimila wa wamasai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Huduma, Sep 1, 2008.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Sep 1, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yetu, mwenzetu Bwana Lowassa ametawazwa rami kuwa kiongozi wa kimila wa jamaa zetu Wamasai.

  Kusimikwa huko kutampa nafasi ya kufanya ziara Arusha, Arumeru, Monduli, Morogoro, Usangu na kadhalika ili kujitambulisha rasmi.

  Shirika la Taifa la Habari Tanzania [TBC] lilitumia takriban dakika 2 na nusu nzima kutangaza habari hizi.

  Tunategemea pia na wabunge wa Kihaya, Kichagga, Kipemba, Kimakonde, Kiluguru, Kimeru, Kipare, Kigogo, Kikiha, Kinyamwezi, Kisukuma, Kinyakyusa, Kihehe, Kingoni na kadhalika watakaochaguliwa kuwa viongozi wa kimila wa makabila yao nao watapewa fursa sawa na mwenzetu Lowassa mara muda wao wa kusimikwa utakapowadia!

  WAKATI huo huo Bwana Mkubwa Yusufu Makamba anasema kwamba CCM hailei wala haiwafugi MAFISADI. Swali ambalo Watanzania wengi wamejiuliza pamoja na ngonjera za kufuata mkondo wa sheria ni kuwa vipi kama polisi ni wa CCM, Mahakama ni za CCM, TAKUKURU ni ya CCM na TBC ni ya CCM na kadhalika na kadhalika huo mkondo wa sheria utatoka wapi.

  Wanachokiomba wao ni kwamba Kamanda Mkuu wa Polisi ateuliwe na Bunge, Jaji Mkuu ateuliwe na Bunge, TBC iwe shirika h uru la habari linaloendeshwa kwa ruzuku ya serikali na kiongozi wake kuchaguliwa na Bunge na sio rais na mambo kama hayo ndio tutajua kweli CCM haiwafugi wala kuwalea MAFISADI!
   
 2. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..hii haitakuwa mara ya kwanza!

  ..kampeni zinapamba moto!

  ..kwasababu ya umuhimu wa habari yenyewe!

  ..ukiiga tembo kunya utachanika msamba.

  ..huu ni wakati wa ajabu katika historia ya tanganyika!

  ..tunasubiri ya firauni sasa, ya musa tushayazoea!
   
 3. c

  chikira Member

  #3
  Sep 1, 2008
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuishi kwingi ni kuona mengi.Ndio mana nasema, watanzania tumekwisha.Hivi hawa hawaelewi kwamba kufanya hivyo ni kujitambulisha na ufisadi wake.Haya ni maajabu ya Musa!
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  njaa kali hiyo, hakuna cha kusimikwa wala chochote, lowasa ameendelea kutumia zile pesa alizopata kwenye richmond kujijenga kimila na kisiasa, hatutamruhusu akanayage usangu labda huko morogoro watamruhusu kwa kuwa huwa wanaabudu sana vya kupewa, ndo maana wanawabunge maponjoli hadi leo
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Haya mambo ya "kusimikana" mmh mie simo......
   
 6. M

  Mbunge Senior Member

  #6
  Sep 1, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BAADA ya miaka takriban hamsini ya ubabaishaji wa ksiasa, je, huu si wakati wa Watanzania kurejeshewa uchifu na umangi.

  Faida za viongozi wa Kikabila kama Adam Lusekelo anavyotuelezea kuhusu uchifu wake huko Unyakyusa ni kuwa karibu na wananchi.

  Chifu Adam Lusekeleo pia analea watu wa kabila lake hususan katika masuala ya maendeleo ya jamii na kiuchumi.

  Mila mbalimbali zilizowekwa toka enzi za mababu zinapotumika wanawake, watoto, wazee, walemavu, maalbino na kadhalika wanalindwa na haki zao kuangaliwa.

  Matatizo ya maeneo, majimbo, kaya, ukoo na familia yanakuwa na watu wa kuyaangalia tofauti na hivi sasa ambapo hata kesi za kuku zinapelekwa mahakamani.

  Uchifu utaleta ushindani katika masomo na hivyo kila eneo likijitahidi kuwasomesha watoto wao na hivyo kuchochea maendeleo ya elimu nchini.

  Suala la huduma litaendelezwa na kuwafikia wananchi kwa ukaribu tofauti na hivi sasa. Aidha fedha za tiba hazitaliwa na ununuzi wa magari ya kifahari na unywaji wa peteroli na dizeli bali zitatumika kununua vifaa vinavyohitajika mahospitalini.

  Madaktari na manesi kadhalika hawatakuwa na roho mbaya na wala rushwa kama ilivyo sasa.

  Polisi wa chifu watakuwa ni watu walio karibu na sio mamluki wa fedha na wakubwa kiasi ambacho hupindishwa sheria mwenye hatia akawa ndio mwenye haki.

  Mahakama za chifu zitakuwa wazi na hazitaruhusiwa kufanya vituko vya mahakama za wanasiasa.

  Wawalishi wa machifu watakuwa ni koo za kabila husika na hawa watawatetea kwa dhati watu hao na sio kutafuta maslahi binafsi.

  Kwa kuwa viongozi wa kisiasa wameshindwa kazi na sasa wameingia kwenye mashindano ya ufisadi na kushindana kwa kuwa na magari, ndege, majumba na milki nyingine za kifahari; kwa kuwa viongozi wa dini wanapigania fedha za sadaka na ruzuku toka serikalini badala ya kuendeleza dini zao; kwa kuwa wabunge wanapigania maslahi binafsi na ya jamaa zao; na kwa kuwa wasomi wetu wamekuwa kasuku wa kukariri na kuimba ya wengine badala ya kuja na ufumbuzi wa matatizo yetu ya maendeleo n inatoa wito wa herufi kubwa SASA TURUDISHIENI MACHIFU NA MANGI WETU. Na hongera Lowassa kwa kutawazwa Chifu wa Umasaini-Limbuginna!!!!
   
 7. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #7
  Sep 2, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Na hasa afie kwingine lakini siyo Usangu Haki ya Mungu! Naanza kupiga kampeni ili asipokelewe akienda! Fisadi huyu asije ambukiza kizazi chetu! Aende hukohuko Arumeru na arusha wanakomuabudu!
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba tuanze petition kumfanya Lowassa awe Rais au mgombea wa Urais kupitia CCM 2010!

  It is about time we allow him to be the president and prove everyone wrong!
   
 9. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kuna kijana mmoja kule kijijini kwetu,alienda kujisaidia haja kubwa porini.(si mnakumbuka mambo ya huko kwetu majita).Basi kama kawaida akachuma majani ili kujisafisha baada ya shughuli yake hiyo.Huyo bwana alikuwa hakwenda mbali na njia toka pale alipochuchumaa.Mara ghafla mtumeee!! ile yuko katikati ya shughuli akamwona mama mkwe wake anakuja.Guess what??? Jamaa ilibidi ajifiche usoni kwa kutumia yale majani aliyokuwa amechuma ili ajichambie akidhani kuwa mama mkwe hatomuona.
  Anyaway sina uhakika kama jamaa alifanikiwa kujificha na mama mkwe wake hakumjua sura au ndo ile kuonyesha jinsi mishipa ya aibu ilivyokatika.

  Kaazi kwelikweli
   
 10. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Haiwezi kumsaidia sana, lakuvunda halina ubani. Mavi matupu!
   
 11. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duuh aisee huyu Lowasa sasa jamani cheo alichobakiza ni Urais tu...!

  Vyeo vyote vya kisiasa vya Ardhi ya Tanzania amevikalia au aliwahi kuvipitia...!

  Sasa ameamua kutoka kikabila...!

  Huyu mtu analake jambo, hapo bado, kwa vile kaoa singida, utasikia wiki ijayo kateuliwa kuwa Mkuu wa kabila la kinyaturu...! (kwa mashemeji)

  Kwa vile mwanae kaolewa na Mchaga utasikia mwezi ujao kateuliwa kuwa mkuu wa kabila la wachaga...! (kwa wakwe)

  Kimya kimya...! 2010 RAIS LOWASA kupitia Chama Cha Makabila (CCM)
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yale yaleeee go on....
   
 13. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..you will be surprised!
   
Loading...