Lowassa asafishwa tuhuma za ufisadi Kenya

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Na Mwandishi Wetu

GAZETI la The Sunday Standard la Kenya limemwomba radhi Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, kutokana na habari liliyoandika Oktoba 14 mwaka jana likimhusisha na tuhuma za rushwa.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu, ilisema katika kumradhi hiyo iliyochapishwa ukurasa wa 27 wa toleo la Januari 13 mwaka huu, gazeti hilo lilisema limegundua kuwa madai hayo hayakuwa na ukweli wowote.

"Gazeti linapenda kumwomba radhi Waziri Mkuu kwa usumbufu wowote aliosababishiwa na madai hayo," lilisema.

Kumradhi hiyo inatokana na barua ya Wakili Eric Ng'maryo wa Moshi, kwa niaba ya Bw. Lowassa, kwa Mhariri wa Gazeti hilo, ikiomba kukanushwa kwa madai hayo bila masharti yoyote na kuombwa radhi Waziri Mkuu.

Nakala ya barua hiyo ya Novemba 5 mwaka jana, ilitumwa pia kwa mwandishi wa habari hiyo, Bw. Ernest Mpakanjira; Mchapaji wa gazeti hilo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Standard Group Limited.

"Kama, maombi haya yatapuuzwa, maagizo kutoka kwa mteja wangu yatatekelezwa kwa kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na usumbufu na masuala mengine ya kulipwa fidia...," barua hiyo ya wakili ilisema.

Kumradhi hiyo yenye kichwa "Kumradhi kwa Waziri Mkuu wa Tanzania" ilikiri kuchapisha habari ikiwa na kichwa kisemacho: 'Shinikizo kwa Kikwete kupambana na rushwa' Oktoba mwaka jana, ikiwa na madai mengi kuhusiana na rushwa yakimhusisha Waziri Mkuu Lowassa.

Iliendelea kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete angelazimika kufanya kisichofikirika kwa kumtoa kafara rafiki yake mkubwa, Bw. Lowassa.

Habari hiyo ya The Standard, ilidai kuwa umma ulikuwa ukimwona Waziri Mkuu kama kinara wa rushwa serikalini, ambaye Rais hawezi kumdhibiti licha ya kushinikizwa kusafisha uozo ndani ya Serikali yake.

Kwamba kulikuwa na taarifa za Rais kutaka mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ambayo yangewaathiri watu wake wa karibu akiwamo Waziri Mkuu, ambao walitazamiwa kuondolewa katika nyadhifa zao.

Pia likadai kuwa Bw. Lowassa katika kutafuta kinga, alimhusisha mtoto wa Rais katika ubadhirifu wa fedha za umma kupitia zabuni tata ya kuliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kununua jenereta za dharura kutokana na matatizo ya umeme mwaka jana.

Mitambo hiyo aghali lilidai gazeti, ilikuja kubainika kuwa ni mitumba miezi miwili tu baada ya kufungwa na kuzinduliwa na kusababisha nchi kuingia katika kiza na matatizo katika uzalishaji viwandani.

Gazeti liliendelea kudai kuwa hiyo ilisababisha hali mbaya kwa nchi ambayo ilishaanza kubanwa na wafadhili kuwa na uwazi katika matumizi ya fedha za umma.

Hali hiyo iliongezwa nguvu na wapinzani kutangaza majina ya walioitwa 'orodha ya mafisadi' ikimhusisha Bw. Lowassa, Rais Kikwete, mwanawe wa kiume na mkewe, wafanyabiashara na Mbunge, Bw. Rostam Aziz, ambaye alidaiwa kuratibu kampeni za Rais Kikwete mwaka 2005.
 
Unajua ktk lugha ya kiswahili na matumizi yake kuna tafsiri ya MUONGO kama hivi:-
MUONGO NI YULE ASEMAYE UKWELI WAKATI HAKUHITAJIKA KUUSEMA AMA KUUPELEKA KWA MTU ASIYETAKIWA KUUPATA UKWELI HUO....
 
Kasafishwa sawa...lakini hajatakata!
Roya habari za siku,wewe kama mwanasheria nadhani unajua kuwa swala la kumsafisha mtu siyo genaral bali na specific kwa jambo husika.kwa mtazamo wako kama hajasafishika ni sawa lakini ukumbuke kuwa ni hatua moja kubwa kuelekea ukweli.atasafishwa dhidi ya majungu yote mliompakazia.Lowasa is crean na hajaiba pesa ya umma,ni mjasiliamali na hawezi kuacha kujituma kutafutia pesa kwa njia halali just becouse ya wivu na majungu.KEEP IT UP EDO!!!!!!!!!!!!!!
 
Sio kosa langu asiposafishikika... mi si mwandishi wa habari iliyomchafua. Kama kilichofanyika ni hatua moja kumtakasa, it is ok with me..... mwisho mimi si mwanasheria na wala sitarajii kuwa mwanasheria.
 
Pole sana Roya Roy kwa kuchafuliwa jina . Namtaka sasa Fisadi akuombe msamaha na ajue hapa hatuparamii watu .Lowasa ni msafi ? Wakenya wameamua yaishe lakini Tanzania tunaye mzee wa kasungura na air Uchumi .
 
IAM SORRY ROY BUT ULISEMA KUWA HAJATAKATA.MIMI NADHANI NI MSAFI SIKU ZOTE.
 
Roya habari za siku,wewe kama mwanasheria nadhani unajua kuwa swala la kumsafisha mtu siyo genaral bali na specific kwa jambo husika.kwa mtazamo wako kama hajasafishika ni sawa lakini ukumbuke kuwa ni hatua moja kubwa kuelekea ukweli.atasafishwa dhidi ya majungu yote mliompakazia.Lowasa is crean na hajaiba pesa ya umma,ni mjasiliamali na hawezi kuacha kujituma kutafutia pesa kwa njia halali just becouse ya wivu na majungu.KEEP IT UP EDO!!!!!!!!!!!!!!
Yes he is clean on the thing that doesnt involve Corruption.Edward ni mnyang'anyi na kamwe ufalme wa Mwinguni hauwezi kumpokea hadi atakapoamua kurudisha pesa zetu.

MaMvi Mzeee wa kasungura aliyechota billion 13 mwaka juzi pale Arusha katika kiwanda cha ngozi.Au unataka tumwage mabomu hapa kabla Muda wake haujafika??
 
Gembe kuwa genbe kweli sema usikike na apelekewe taarifa kwamba JF wanajua haya na tunangoja muda . Mpe nyepesi kwanza.
 
IAM SORRY ROY BUT ULISEMA KUWA HAJATAKATA.MIMI NADHANI NI MSAFI SIKU ZOTE.
Unadhani,kumbe hata haumjui vizuri Ndanda kossovo?basi kwa taarifa yako EL ni mchafu,mlafi,fisadi na kwa kumkumbuka Baba wa taifa,Mwalimu Nyerere(RIP) alishwahi kuhoji pesa ya Lowassa,sasa kama wewe Fisadi mtoto ambaye haujui historia ya El kwanini usituulize wazee kama sie tulioko hapa mjini muda mrefu.?

Maisha yamekuwa magumu baada ya watu kama hawa kuaminiwa na chama huku mzee wa kifimbo aliwakataa

Mzee ES embu baalezee
 
NYERERE ALIKUWA NI MSHAMBA TU NA NAKUMBUKA ALIHOJI KWA SABABU YA NYUMBA ILIOKUWA YA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI.HILE NYUMBA NIN YA KAWAIDA SANA LABDA KAMA UNA NJAA ZAKO NDIO UTAONA DEAL.USHAHIDI WAKO WA NYERERE NI MDOGO SANA KUTULETEA HAPA,NYERERE HAKUWA NI MUNGU WA TANZANIA NAE ANA MAKOSA MENGI SANA,PENGINE BORA YA EL
 
Yes he is clean on the thing that doesnt involve Corruption.Edward ni mnyang'anyi na kamwe ufalme wa Mwinguni hauwezi kumpokea hadi atakapoamua kurudisha pesa zetu.

MaMvi Mzeee wa kasungura aliyechota billion 13 mwaka juzi pale Arusha katika kiwanda cha ngozi.Au unataka tumwage mabomu hapa kabla Muda wake haujafika??
UNAPASWA KUWA MTUNZI WA HADITHI NA STORY ZAKO ZA KUFIKILIKA.KESI ZA KUBUNI NA TAMTHIRIA ZA KUSADIKIKA.WEWE KAMA NI UKWELI HUU UZUSHI WAKO BASI MUNGU AMSAMEHE MH EDO MAKOSA YAKE NA ANITWISHE MIMI BADALA YAKE.
 
NYERERE ALIKUWA NI MSHAMBA TU NA NAKUMBUKA ALIHOJI KWA SABABU YA NYUMBA ILIOKUWA YA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI.HILE NYUMBA NIN YA KAWAIDA SANA LABDA KAMA UNA NJAA ZAKO NDIO UTAONA DEAL.USHAHIDI WAKO WA NYERERE NI MDOGO SANA KUTULETEA HAPA,NYERERE HAKUWA NI MUNGU WA TANZANIA NAE ANA MAKOSA MENGI SANA,PENGINE BORA YA EL
Mmmmh! FM uko serious mkuu katika bandiko hili?
 
Back
Top Bottom