Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Na Mwandishi Wetu
GAZETI la The Sunday Standard la Kenya limemwomba radhi Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, kutokana na habari liliyoandika Oktoba 14 mwaka jana likimhusisha na tuhuma za rushwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu, ilisema katika kumradhi hiyo iliyochapishwa ukurasa wa 27 wa toleo la Januari 13 mwaka huu, gazeti hilo lilisema limegundua kuwa madai hayo hayakuwa na ukweli wowote.
"Gazeti linapenda kumwomba radhi Waziri Mkuu kwa usumbufu wowote aliosababishiwa na madai hayo," lilisema.
Kumradhi hiyo inatokana na barua ya Wakili Eric Ng'maryo wa Moshi, kwa niaba ya Bw. Lowassa, kwa Mhariri wa Gazeti hilo, ikiomba kukanushwa kwa madai hayo bila masharti yoyote na kuombwa radhi Waziri Mkuu.
Nakala ya barua hiyo ya Novemba 5 mwaka jana, ilitumwa pia kwa mwandishi wa habari hiyo, Bw. Ernest Mpakanjira; Mchapaji wa gazeti hilo na Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Standard Group Limited.
"Kama, maombi haya yatapuuzwa, maagizo kutoka kwa mteja wangu yatatekelezwa kwa kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na usumbufu na masuala mengine ya kulipwa fidia...," barua hiyo ya wakili ilisema.
Kumradhi hiyo yenye kichwa "Kumradhi kwa Waziri Mkuu wa Tanzania" ilikiri kuchapisha habari ikiwa na kichwa kisemacho: 'Shinikizo kwa Kikwete kupambana na rushwa' Oktoba mwaka jana, ikiwa na madai mengi kuhusiana na rushwa yakimhusisha Waziri Mkuu Lowassa.
Iliendelea kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete angelazimika kufanya kisichofikirika kwa kumtoa kafara rafiki yake mkubwa, Bw. Lowassa.
Habari hiyo ya The Standard, ilidai kuwa umma ulikuwa ukimwona Waziri Mkuu kama kinara wa rushwa serikalini, ambaye Rais hawezi kumdhibiti licha ya kushinikizwa kusafisha uozo ndani ya Serikali yake.
Kwamba kulikuwa na taarifa za Rais kutaka mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, ambayo yangewaathiri watu wake wa karibu akiwamo Waziri Mkuu, ambao walitazamiwa kuondolewa katika nyadhifa zao.
Pia likadai kuwa Bw. Lowassa katika kutafuta kinga, alimhusisha mtoto wa Rais katika ubadhirifu wa fedha za umma kupitia zabuni tata ya kuliwezesha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kununua jenereta za dharura kutokana na matatizo ya umeme mwaka jana.
Mitambo hiyo aghali lilidai gazeti, ilikuja kubainika kuwa ni mitumba miezi miwili tu baada ya kufungwa na kuzinduliwa na kusababisha nchi kuingia katika kiza na matatizo katika uzalishaji viwandani.
Gazeti liliendelea kudai kuwa hiyo ilisababisha hali mbaya kwa nchi ambayo ilishaanza kubanwa na wafadhili kuwa na uwazi katika matumizi ya fedha za umma.
Hali hiyo iliongezwa nguvu na wapinzani kutangaza majina ya walioitwa 'orodha ya mafisadi' ikimhusisha Bw. Lowassa, Rais Kikwete, mwanawe wa kiume na mkewe, wafanyabiashara na Mbunge, Bw. Rostam Aziz, ambaye alidaiwa kuratibu kampeni za Rais Kikwete mwaka 2005.