Mji wa Tunduma jana ulichafuka baada ya Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kulakiwa na umati mkubwa wa wafuasi wa CDM waliokuwa wamejipanga kando kando ya barabara.Wananchi hao walikuwa wakipiga miluzi kwa sauti kubwa na kuonyesha alama ya vidole viwili juu ishara ya chama hicho.
Lowassa alikuwa akienda kwenye harambee ya ya kanisa la EAGT ambapo alichangia sh milioni kumi.
Kutokana na sintofahamu hiyo kulikuwa na ulinzi mkubwa wa polisi ambapo Lowassa alikuwa na msafara mkubwa wa viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi.Kutokana na hali hiyo Lowassa alichelewa kufika kwa wakati kwenye harambee,kwani aliwasili saa 8 mchana badala ya saa 5 asubuhi.
Akizungumza kwa kifupi na waandishi Lowassa alisema alipata majaribu makubwa safarini lakini Mungu alimfikisha salama.Alidai alisaidiwa sana na mkurugenzi mstaafu wa usalama wa Taifa Apson Mwang'onda.
SOURCE:NIPASHE JUMAPILI.