Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Niko mbali, ila mida hii nimetafuta wire wa JF na nimeupata.. Lowasa kapigiwa simu kali.. kaambiwa kama ana mpango wa kujivua gamba basi atafute nchi ya kuishi kama anapenda maisha yake.. sijui kinachoendelea huko nchini.. ila nimewajuza tu..
 
Twasubiri kwa hamu....ila asiwe na jazba wakaanza kuumbuana na rafiki yake!!
 
Anaeleza uhusiano wake na CCM na kuwa yeye ni kada wa chama kwa muda mrefu hivyo hawezi kukihujumu chama. Kama kuna tatizo wanajadili kwenye kikao na hawezi kumhujumu Rais
 
Hataki kuulizwa maswali nje ya atakayoyazungumza???? Mh sielewi elewi hapa ni kukimbia maswali magumu au sarakasi za kujivua gamba? Wacha tumsikilize anazungumza nini
 
Wenye radio hapa arusha tune 105.7fm jamaa anaongea hapa sijui ni radio gani ila frequency ni hiyo
 
Anaendelea kusema kuwa hajakutana na JK barabarani hivyo watu waache kumchonganisha na viongozi wa chama. Na anakanusha kuwa ana mpango wa kugombea urais. Anawaita wazushi wote kuwa ni wanafiki.
 
Saa nne na dk 40 bado hajaanza funguka huyo mzee.....mtibuano zaidi kwa Magamba unazidi
 
Tunasubiri mtuhabarishe maamuzi magumu atakayo fikia.
Sidhani kama atajivua gamba........ hilo haliwezi tokea
 
Anakanusha kuhusika na maandamano ya vijana Arusha. Ansema ni uongo wa kutupwa na umbeya. Ana-quote gazeti moja, sijui gazeti gani
 
Ndio maana anasita sita kuongea....inawezekana kweli maana anaweweseka sasa nini aseme nini aache maana najua leo angefyatuka!!
 
Gamba limeng'ang'ania hakika. Huyu babu hawezi kujivua gamba. Shukurani. Tafadhali tuupdate. Tuko mashambani tunajenga taifa.
 
Lowassa ni miongoni mwa viongozi wenye kauli zisizoaminika katika jamii. Kwa mfano mdogo tu hapa, huyu ndugu alijipangia mwenyewe na akatafuta kututangazia kwamba leo hii ANALO LA MOYONI KUHUSU UFISADI WA DOWANS na kwamba angetuambia Wa-Tanzania wenzake kama na yeye kesharejesha chenchi Benki Kuu sawa na Manji au laa; ona sasa amepitiliza karibia na dakika 60 nzima!!!

Bure kabisa, hamn kitu hapa!!

nne na nusu si tiyari.. Lete updates
 
Natoa TAMKO:Ni uzembe mpaka leo JF haina live audio flaws. kitu gani kigumu.. tuambie tuchangie.. habari hii tungeipata live humu jamvini.. Mods ongezeni kufikiri bwana!!
 
Back
Top Bottom