Lowassa angeshinda uchaguzi 2015 sera yake ya ELIMU, ELIMU, ELIMU ingeimarisha vipi uchumi wa Mtanzania mmoja mmoja?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,605
9,074
Tangu uchaguzi wa mwaka 2015 upite huu ni mwaka wa 6 sasa, wagombea wa nafasi ya urais walikuwa ni JP. Magufuli na E.Lowassa,

Swali langu je kama ingetokea Lowasa akashinda uchaguzi sera yake kuu ilikuwa ni kutoa elimu bure kwa wote mpaka chuo kikuu (ELIMU, ELIMU, ELIMU), kwa elimu yetu hii hii inayotolewa vyuoni je hii sera ingeweza vipi kuimarisha uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?
 
Tangu uchaguzi wa mwaka 2015 upite huu ni mwaka wa 6 sasa, wagombea wa nafasi ya uraisi walikuwa ni JP.Magufuli na E.Lowasa,

Unapofanya comparizon, tumia equal comparators. Elimu na uchumi, wapi na wapi?. Swali lako lingekuwa valid kama ungecompare elimu bure ya JPM ya darasa la kwanza mpaka form 4, imekuza vipi na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja wa Tanzania?. Baada ya kuonyesha faida hizo ndipo sasa tungelinganisha na Elimu Elimu Elimu ya EL ya elimu bure toka chekechea hadi Chuo Kikuu?.

Mimi ni supporter wa ile Elimu elimu elimu.
P
 
umenikumbusha mwaka ule Mbowe kagombea urais. Baada ya mwaka mmoja wa uchaguzi Dada yangu mmoja akaniuliza huyu Mbowe wenu alikuja hapa na helkopta akatuahidi vitu vizuri, mbona mpaka sasa hajatimiza?
 
Tangu uchaguzi wa mwaka 2015 upite huu ni mwaka wa 6 sasa, wagombea wa nafasi ya uraisi walikuwa ni JP.Magufuli na E.Lowasa,

Swali langu je kama ingetokea Lowasa akashinda uchaguzi sera yake kuu ilikuwa ni kutoa elimu bure kwa wote mpaka chuo kikuu (ELIMU, ELIMU, ELIMU), kwa elimu yetu hii hii inayotolewa vyuoni je hii sera ingeweza vipi kuimarisha uchumi wa mtanzania mmoja mmoja?

Bila ushabiki wa kisiasa, tuangalie umuhimu wa elimu tu. Kama unataka kujua umuhimu wa elimu kwenye kuimarisha uchumi kawaulize China na Japan
 
Unapofanya comparizon, tumia equal comparators. Elimu na uchumi, wapi na wapi?.
Natumaini umelielewa vizuri swali langu hebu nisaidie kuliweka vizuri,

Lengo langu tujadili kwa manufaa ya baadae as long as hatuna cha kupoteza sababu hakushinda uraisi, lengo langu ni kuuliza ila sio kumbeza E. Lowasa.
 
Bila ushabiki wa kisiasa, tuangalie umuhimu wa elimu tu. Kama unataka kujua umuhimu wa elimu kwenye kuimarisha uchumi kawaulize China na Japan
China ya nini mkuu wakati tupo bongo, na elimu yetu ndio hii hii nimeuliza swali lengo langu sio kumbeza mtu
 
Unapofanya comparizon, tumia equal comparators. Elimu na uchumi, wapi na wapi?. Swali lako lingekuwa valid kama ungecompare elimu bure ya JPM ya darasa la kwanza mpaka form 4, imekuza vipi na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja wa Tanzania?. Baada ya kuonyesha faida hizo ndipo sasa tungelinganisha na Elimu Elimu Elimu ya EL ya elimu bure toka chekechea hadi Chuo Kikuu?.

Mimi ni supporter wa ile Elimu elimu elimu.
P
Unaonaje mkuu ukiuanzisha upya huu mjadala mkuu tuwaombe Mods waufute siku ukipata muda uuweke vizuri ili ueleweke vizuri mi naona unamanufaa tutajifunza kitu
 
Sioni uchumi popote bila elimu, elimu ndo ufunguo wa maisha!

Nilikuwa namkubali sana huyu mwamba kwa sera yake ya elimu! Ukitaka maendeleo ya sehemu yoyote wekeza kwanza elimu, baada ya hapo utaona nn kitatokea!!

Kama unataka kuelewa vizuri chukua mfano mdogo kuanzia ngazi ya familia!!

Chukua familia ambayo baba, mama na watoto wamepata elimu na kuelimika vyema! Then compare na familia ngingine ambayo baba mama na watoto hawajapata elimu kabisa!

Then wapime katika vigezo vya maisha ya kawaida tu, nani anaisha maisha mazuri!

Then ukipata jibu, chukulia kama mtaa mzima, kijiji, wilaya, mkoa na taifa litaelimika, nchi itakuwa katika level gani ya maendeleo!

ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU
 
Education is an investment in human Capital.
Mkulima msomi/mwenye elimu na asiye na elimu utaona tofauti ktk uzalishaji wao wa mazao, kamwe hauwezi kulingana.
Msomi lazima atazalisha mazao kwa wingi na na yenye ubora na hivyo kuletea tija ktk uchumi wake na kwa taifa kwa ujumla.
ufanisi ktk utendaji wa kazi yoyote ile ni tija katika uchumi.

Faida ya Elimu Bure iliyo anza kutolewa na Serikali kuanzia mwaka 2015 (Msingi hadi kidato cha 4) Faida/tija yake ktk uchumi huwezi kuipima ndani ya miaka 6 labda baada ya miaka 20 ijayo.
kumbuka mfumo wa Elimu yetu unachukua muda mrefu sana(7+4+2+4=17)
 
Back
Top Bottom