Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,230
- 6,469
Kwa mujibu wa mwanaharakati fulani, ni kwamba hali ya siasa za upinzani kubanwa hivi sasa, ni kidogo sana na hali ingekuwa mbaya sana Kama Lowassa angekuwa Rais kupitia CCM 2015.
Mwanaharakati huyo anadai, Lowassa sio mvumilivu wa siasa za kukosoana na angekuwa Mbabe zaidi hata ya Rais Magufuli. Anadai mbinu anazotumia Magufuli hivi sasa, aliziasisi Lowassa na wafuasi wake wa zamani ambao ni masalia serikalini ndiyo wanaomfundisha Magufuli mbinu hizo.
Nilimuuliza anajuaje Lowassa angekuwa muuaji wa upinzani kuliko Magufuli? Akanijibu kuwa aliwahi kuwa karibu na Lowassa asiyependa ukosoaji na kwa kifupi Angeukwaa Urais wa JMT 2015 kupitia CCM, ni lazima angemaliza kabisa upinzani nchini.
Amedai hata Ushindi wa kishindo na wakati mwingine kupita bila kupingwa na kupelekea uchaguzi kutofanyika Jimboni Monduli, Uligubikwa na usanii mwingi. Anadai wakati mwingine wapinzani wake walihamishwa mbali na Monduli na kupewa Vyeo serikalini au hata kuathibiwa.
Mwanaharakati huyu ananipa mifano ya mwaka 2005, 2010 na serikali za mitaa 2014 jimboni Monduli ambapo Lowassa alicheza rafu nyingi mno.
Kumbe yoote anayoyafanya Magufuli ni kuiga kutoka kwa Lowassa wa CCM hapo zama za kale.