Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
JANUARY MAKAMBA mwenyekiti nishati na madini na LYATONGA AMESHINDA LAC.
Duh duh duh!! Haya bwana.
JANUARY MAKAMBA mwenyekiti nishati na madini na LYATONGA AMESHINDA LAC.
Si kila mmoja anayajua ya mjengoni so wekeni na virefu vyake
Kuchaguliwa kwa Edward Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans kuwa mwenyekiti wa the most powerful committee in the National Assembly -- Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ina maana kuu zifuatazo:
1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.
2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.
3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye ayakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.
4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.
5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.
6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa CCM kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa CUF na UDP ambao ni vibaraka wa CCM.
Lowassa, January na Serukamba wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati ya Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana influence shuhuli za Bunge, kanuni, miswada na hoja mbali mbali.
Anne Makinda ndiyo aliyewateuwa kina Lowassa, January, Serukamba kuwa kwenye kamati hizi kwa maelekezo ya Rostam Aziz aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.
Ni dhahiri kuwa mafisadi sasa wameliteka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Hivi kwa nini Watu wazima na akili zao wanakuja humu bodini kuongea damu, kufa, kujitoa mhanga, makaburi n.k
Haya mambo ya kufa kufa yote yanatoka wapi...!!!!
Hivi Mwamvita Makamba wa Vodacom ni ndugu na January au ni majina tu?JANUARY MAKAMBA mwenyekiti nishati na madini na LYATONGA AMESHINDA LAC.
Si kwamba hawajui, matarajio yao ni kwamba kamati hizo zinahitaji akili ya kawaida tu ya kuzijua hasa kama mtu anafuatilia siasa za Tanzania na kwingineko. OkHata hhao waliotuma hawajui virefu vyake.
acha fiksi....Asante Kiranja, ushindi wa Zitto POC ni uthibitisho kuna wana CCM wameamua kuachana na unazi na kuchagua mtu. Jana usiku kucha wamekuwa wakitumiana sms za msisitizo PAC -Cheyo, LAC- Mrema na POC- CUF.
Zingeenda Chadema bila shaka kwa sababu wagombea wangekuwa toka kambi rasmi ya upinzani bungeni. CCm wasingekuwa na namna zaidi ya kupiga kura kuwachagua CDMNingependa kujua hizo posts ndio zingeenda CHADEMA zote kama ile kanuni isingebadilishwa au ndio ingekua hivyo hivyo?