Lowassa amuumbua Lukuvi, Mbunge wa Monduli asema shamba sio la Lowassa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665

Siku chache baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kulieleza Bunge kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha shamba la Makuyuni Wilayani Monduli mkoani Arusha, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amejitokeza kutoa ufafanuzi unaomsafisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Kalanga alisema kuwa Lowassa hamiliki shamba hilo la Makuyuni kwakuwa tangu Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alipofuta hati ya umiliki wa shamba hilo kutoka kwa raia wa Kigeni aliyemtaja kwa jina la Stein, bado halijamilikishwa rasmi kwa wananchi na ndio ilikuwa hoja yake.

Alisema kuwa maelezo ya Lukuvi hayakuwa na ukweli na kwamba alichanganya kati ya shamba hilo la Mkuyuni na shamba la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kukagawiwa kwa wananchi wa Monduli ambapo Lowassa alisaini hati miliki yake kama muwakilishi wa wananchi wa Wilaya hiyo kwakuwa wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya Ardhi (Tanzania Land Trustee (TLCT).

“Jambo la kushangaza ni pale Waziri alipochanganya shamba hilo na lile la Manyara Ranchi ambalo hati yake ilifutwa tangu mwaka 2000 na kugawiwa kwa wananchi. Hati miliki ya shamba hilo la Manyara Ranchi ilisainiwa na Lowassa ambaye wakati huo alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Land Trustee(TLCT),” alisema

Awali, Waziri Lukuvi alieleza kuwa Shamba hilo la Mkuyuni linapaswa kumilikishwa kwa wananchi lakini nyaraka zinaonesha kuwa hati yake imesainiwa na Lowassa na kwamba Serikali itamnyang’anya na kulirejesha kwa wananchi.

Juzi, Lowassa aliahidi kuwasiliana na Mbunge huyo ili kufuatilia kauli aliyoitoa Waziri Lukuvi dhidi yake kuhusu kujimilikisha shamba hilo ili aweze kutoa ufafanuzi kwani hakuna ardhi anayoimiliki kinyume cha taratibu.
 
Wakianza kufukua makaburi wafu waamka na ıtakuwa hatarı bora waishie hapo
 
WATAMSAFISHA SANA KIPINDI HIKI HAO WALIOMCHAFUA AWALI NA KUMWITA FISADI
 
Tukubali tu kuwa wafanyakazi wengi wa serikali waliokuwa na vyeo vya juu pamoja na wanasiasa wakijimilikisha mashamba makubwa baada ya nchi kuingia kwenye soko huria.

Tumeona migogoro mingi kati ya wananchi na wanasiasa kwa sababu ya matatizo ya kujimilikisha mashamba makubwa.

Siyo muda mrefu tuliona Sumaye wakiambatana na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda kwenda kusuruhisha mgogoro wa shamba lake na wananchi aliodai wamevamia.

Hili ni suala la Lowassa lakini kinashangaza Mbunge ndiye kwa sasa amepewa kazi ya kumsafisha Lowassa.

Nilisema kwenye thread hapa chini ni vizuri Lowassa akawaambia wabunge wa CHADEMA mali zake ili kuepuka kadhia kama hili la kuanza kumsafisha baada ya kumpiga madingo ya kisiasa ( friendly fire).
 
Huyo mbunge alishindwa nini kuomba muongozo kuhusu matamshi ya waziri Lukuvi ili afute kauli yake? Anaacha kufanya hivyo anakuja kuongea na vyombo vya habari kwa suala alilolianzisha mwenyewe bungeni..

Hapa kuna harufu ya dodoki
 
Hii serikali ndipo naposhindwa kuielewa,yaani ukiwa CCM uko salama,ukihama chama basi wanaanza kusaka nyayo zako!Haki itendeke kwa wote
 
Wakati mwingine sielewi kama kiongozi wetu wana akili timamu au wamelogwa (kama uchawi hupo) Waziri mwenye dhamani, unafahamu kuwa kuna shamba linamerikiwa na kiongozi hisivyo halali, badala ya kuchukua hatua zinazostahiki, unaanza kulia lia bungeni sasa sijui unataka sisi wananchi tufanye nini?

Kama shamba ni la serikali, Lowassa akijimilikisha hisivyo halali kwa akili za kawaida kabisa unachotakiwa kufanya ni nini? Mh.Lukuvi????
 
Dalili za kuonyesha kuwa huyu Mzee anasingiziwa mengi zimeanza kujitokea. Mbunge atake Lukuvi aadhibiwe kwa kusema uongo bungeni na kudhihirisha uzembe wa serikali.
Toka wakati wa Mkapa shamba kanyang'anywa Mzungu lakini hadi Leo halijagawiwa kwa wenye Shida ya Ardhi huu si ni ubwege
 
Huyo mbunge alishindwa nini kuomba muongozo kuhusu matamshi ya waziri Lukuvi ili afute kauli yake? Anaacha kufanya hivyo anakuja kuongea na vyombo vya habari kwa suala alilolianzisha mwenyewe bungeni..

Hapa kuna harufu ya dodoki
Sasa kama hakuwa na data kamili ulitaka akurupuke????
 
Nakumbuka sana zile enzi za wahujumu uchumi ambapo watu walikuwa wanatupa maburungutu ya fedha barabarani. Ndicho kilichomtokea Lowasa kwani anajua kuwa alidhulumu shamba hilo
 
Wakati mwingine sielewi kama kiongozi wetu wana akili timamu au wamelogwa (kama uchawi hupo) Waziri mwenye dhamani, unafahamu kuwa kuna shamba linamerikiwa na kiongozi hisivyo halali, badala ya kuchukua hatua zinazostahiki, unaanza kulia lia bungeni sasa sijui unataka sisi wananchi tufanye nini?

Kama shamba ni la serikali, Lowassa akijimilikisha hisivyo halali kwa akili za kawaida kabisa unachotakiwa kufanya ni nini? Mh.Lukuvi????
Lukuvi aliongea hayo Bungeni. Kama anaona kuwa Lukuvi alilidanganya Bunge basi arudi huko huko akaombe mwongozo na amshinikize Lukuvi atoe uthibitisho wa Lowasa kujimilikisha shamba hilo ama atakiwe kufuta kauli coz Hansad zimesharekodi
 
Sasa kama hakuwa na data kamili ulitaka akurupuke????
Bado kanuni zinamruhusu kufanya hivyo ( aombe muongozo au atoe taarifa ili kuweka kumbu kumbu sawa) ...ili tuone majibu ya serikali yatakavyokuwa.

Kuongea na waandishi wa habari ni dekio tu
 
Kulikua na misleading statemnts kadhaa from Lukuvi, including gharama ya kufanya survey... I hope atakua muungwana na kuja kurekebisha baadhi ya kauli alizotoa; he is a gentleman!!
 
Lowasa alikuwa mkurugenzi AICC akafukuzwa kwa tuhuma za ubadhirifu.. Nyerere alikasirika sana akamtimua
 
Back
Top Bottom