Lowassa amuibukia IGP

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Dar es Salaam. Kama ulidhani yameisha, elewa kuwa bado CHADEMA wanalilia mikutano yao iliyozuiliwa kufanyika katika sehemu mbalimbali nchini.

Mara hii, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemwandikia barua Mkuu wa Polisi, Inspekta Jenerali Ernest Mangu akimtupia maswali kadhaa kuhusu agizo la jeshi hilo la kupiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya kisiasa na maandamano ya vyama vya upinzani.

Barua hiyo ya Lowassa imekuja siku chache baada ya jeshi hilo kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya siasa, likisema kuwa taarifa za kiinteljensia zimeonyesha hatari ya kutokea vurugu katika mikutano hiyo, hatua ambayo pia imepingwa na CHADEMA baada ya jeshi hilo kusambaratisha mkutano.

-----------------
UPDATE:

Waraka wa Waziri Mkuu Mstaafu na mjumbe wa Kamati kuu CHADEMA Edward Lowassa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

IGP-MANGU

Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP)

Salaam,

Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huukwako.

Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwana kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa.

Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jeneraliwa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa namaandamano ya vyama vya upinzani.

Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko njeya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema nataifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizolako hilo.

IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanyahivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoakuwa nyuma ya agizo lako hilo.

Wakati nikiwa natafakari kwa mshangao agizo lako hilo, na baadayekurejea nyumbani, nilipigwa na butwaa zaidi niliposikia Jeshi la Polisi tena katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, likiwazuia viongozi wetu wakuuna wa juu kitaifa kufanya mikutano ya hadhara.

Agizo hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwakwa viongozi hao, akiwamo mwenyekiti wetu wa taifa, Freeman Mbowe(MB) huko Mwanza hivi majuzi.

Katika matukio hayo yote, Polisi mnadai kuwa na taarifa zakiintelijensia ambazo zinazonyesha kuwapo kwa uwezekano wa kutokeakwa vurugu kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya siasa.

Madai haya ya polisi ambayo hata wewe binafsi umepata kuyatoa awaliulipoamua kwa sababu mnazojua ninyi wenyewe, kuminya haki zamsingi na za kikatiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimizamajukumu yao ya kisiasa hayana ukweli hata kidogo.

Si hivyo tu, uzoefu wa kihistoria unakinzana na kwenda kinyume kabisana madai hayo, kwani yako matukio mengi ambayo yamethibitishakwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamomaandamano na hata mikutano imekuwa ikifanyika kwa amani.

Iko mifano mingi inayoonyesha kwamba, tumefanya shughulimbalimbali za kisiasa kwa maana ya maandamano na mikutano yahadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata kwa ulinzi wa polisi.

Mifano ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupinganena maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa kwa uhuru wakikatiba wa vyama vya siasa vya upinzani kujumuika bali kwenda mbalizaidi na kutilia shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumoiliyojificha nyuma ya kichaka cha ‘sababu za kiintelejensia’.

Naandika waraka huu kwako nikiamini kwa dhati kabisa kwamba, kilekilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama ilitupilia mbalimaagizo ya namna hii ya polisi kujaribu kuzuia haki ya kikatiba yavyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea hatahapa kwetu pia.

Si hilo tu, naamini wewe IGP ulifuatilia kile kilichotokea Uganda sikuchache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa urais ambako chama kimoja cha siasa kiliitisha mkutano wa hadhara nakikamwapicha Besigye ambaye wao wanaamini ndiye aliyeshinda urais.

Waganda hao ambao wamekuwa wakiiamini kwamba mgombeawanayemuunga mkono ndiye aliyeshinda japo kura zake ziliibwa, waliruhusiwa kuandamana na kukutana kwa uhuru ingawa baadayewalikamatwa.

Ni jambo la kujifunza kwamba, Waganda hawa hawakuzuiwa na‘kuwapo kwa taarifa za kiinteligensia’ licha ya kwamba walishtakiwabaadae.

Tunachojifunza hapa ni mamlaka za dola, kama lilivyo jeshi letu la polisi, kuheshimu na kulinda haki za raia na kuepuka hatari ya vyombovyetu kujipa dhamana ya kuwaamulia wananchi masuala yao kwakisingizio cha taarifa za kiintelijinsia.

Je, kwa maagizo ya namna hii, Inspekta Jenerali Mangu na wenzakopolisi mnatuonaje sisi viongozi wa upinzani?

Je, mnafikiri pamoja na uzoefu wetu katika siasa na uongozi tunawezatukawa mbumbumbu wa kutambua haki zetu au hata kushindwa kujuadhamana kubwa tuliyobeba ya kuwatumikia wananchi na taifa letu?

Je, IGP Mangu na wakuu wenzako wa Jeshi la Polisi mnapotoa maagizoya namna hiyo hamuoni kwamba mnajenga taswira tu kwamba, malengoyenu ni kutafuta jinsi ya kutumia magari ya upupu yaliyoagizwa kwapesa nyingi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana?

Je, mmeshindwa kujifunza kwamba, kama kulikuwa hakuna vurugukabla na baada ya Uchaguzi Mkuu pamoja na kuwapo kwa kila viashiriavilivyochochewa na taasisi za dola, wapinzani hatuna sababu hata mojaya kuwa chanzo cha vurugu za namna hiyo?

IGP Mangu, pengine ni busara nikakukumbusha kwamba, vyama hivihivi vya upinzani chini ya mwavuli wa UKAWA viliwahi kuandamanakwa maelfu kutoka Buguruni yaliko makao makuu ya CUF hadi makaomakuu ya CHADEMA Kinondoni kwa amani na kwa utulivu.

Je, hukumbuki kwamba katika maandamano hayo yaliyohusisha maelfuya wakazi wa Dar es Salaam, hakuna hata sindano ya wananchiiliyopotea wala mtu kukwaruzwa?

Hayo na mengine mengi ndiyo ambayo yamenifanya nitafakari sana nakukosa jibu naposikia polisi mkituzuia kwenda vijijini kuwashukuruwananchi kwa kutuheshimu na kutupiga kura zao

Ni nini hicho kitakachoathiri amani na utulivu? Wanachama wa vyamavipi hao ambao eti watapingana kwa sababu sisi tumeamuakuwashukuru wananchi waliotuunga mkono kwa mamilioni?


IGP Mangu, nakuomba uyatafakari haya na kuliangalia upya agizo lako, ambalo yumkini haliitakii mema nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika


Edward Ngoyai Lowassa
Waziri Mkuu Mstaafu
 
Lowasa ni nani ndani ya CHADEMA mpaka andike waraka ??

Au ndio ule msemo wa kila MTU ni kambale ndani ya CHADEMA??
 
Mara hii, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemwandikia barua Mkuu wa Polisi, Inspekta Jenerali Ernest Mangu akimtupia maswali kadhaa kuhusu agizo la jeshi hilo la kupiga marufuku mikutano yote ya hadhara ya kisiasa na maandamano ya vyama vya upinzani.

Lowasa ni nani kwenye siasa za nchi hii?
Yeye ni mjumbe tu wa kamati kuu ya CHADEMA.Kama ni maswali chama ndicho kingeuliza kupitia mwenyekiti wake.Polisi msipoteze muda hata kusoma hiyo barua ya mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.Ni mtu mdogo mno kumjibu.

Halafu naona kumbukumbu kapoteza!! Chama chake CHADEMA kimefungua kesi kushtaki polisi kuhusu hilo analoulizia au hajui maskini!! Hata tugazeti na taarifa za habari hasikilizi? Na CHADEMA hawajamwambia kuwa wamefungua kesi?

Polisi hawawezi ongelea jambo ambalo liko mahakamani.

Huyu LOWASA hata washauri wazuri hana maskini
 
Where is the letter guddamn, anapaswa kuwa kashikilia fimbo anaswaga ng'ombe sio peni na barua.

Mzee ni mwongo sana kasahau alituambia atafanya nini uchaguzi ukiisha. Hajui sasa hivi kuna isis bongo na mikutano kama hio ndio prime targets zao.
 
Kuna wakati Lowassa anatakiwa kupumzika.. Anatakiwa kuachana na mambo haya ambayo hayampi faida yoyote zaidi ya kuzidi kupoteza thamani yake kiduchu aliyokuwa nayo.

Ina maana hajui kuwa hili suala lipo mahakamani?
ina maana hana washauri katika masuala yake?
yeye kama mjumbe anafanya hivi, ipi kazi ya
MBOWE na DK MASHINJI?

Ni wakati wake wa kuamini kuwa mwisho wake kisiasa umeishia hapo, anatakiwa aangalie biashara zake. Huku awaachie wazee wa KUBADILI GIA
 
CCM Mwanza wako juu ya sheria ndio maana waliachwa waandamane
 
Si mwenyekiti keshafungua kesi na pamoja kuwa imedunda mahakamani wataalam wanarekebisha warudi tena mahakamani. Lowasa anamwandikia IGP kama nani sasa sio katibu wala mwenyekiti au ndio mwenye chama baada ya kununua.
 
Lowasa ni nani kwenye siasa za nchi hii?
Yeye ni mjumbe tu wa kamati kuu ya CHADEMA.Kama ni maswali chama ndicho kingeuliza kupitia mwenyekiti wake.Polisi msipoteze muda hata kusoma hiyo barua ya mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.Ni mtu mdogo mno kumjibu.

Halafu naona kumbukumbu kapoteza!! Chama chake CHADEMA kimefungua kesi kushtaki polisi kuhusu hilo analoulizia au hajui maskini!! Hata tugazeti na taarifa za habari hasikilizi? Na CHADEMA hawajamwambia kuwa wamefungua kesi?

Polisi hawawezi ongelea jambo ambalo liko mahakamani.

Huyu LOWASA hata washauri wazuri hana maskini
NI WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA ,BADO SERIKALI HII INAMTAMBUA KUMUHUDUMIA NA KUMLINDA PIA
GET THAT IN YOUR FILTHY MIND
 
NI WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA ,BADO SERIKALI HII INAMTAMBUA KUMUHUDUMIA NA KUMLINDA PIA
GET THAT IN YOUR FILTHY MIND

Alitakiwa ajue kuwa swala kama liko mahakamani IGP au waziri mkuu yeyote wa zamani awe wa ukweli au kibaka haruhusiwi kuliulizia.Asubiri maamuzi ya mahakama
 
Alitakiwa ajue kuwa swala kama liko mahakamani IGP au waziri mkuu yeyote wa zamani awe wa ukweli au kibaka haruhusiwi kuliulizia.Asubiri maamuzi ya mahakama
VIBAKA WAPO WENGI TU HATA YULE WA BAGAMOYO EXPRESS NI KIBAKA HAHAHAHA...........................
 
Igp kabila gani vile!!!!!???? Na mwigulu je? Naiona Tanzania mpyaa ya vipigo
 
NI WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA ,BADO SERIKALI HII INAMTAMBUA KUMUHUDUMIA NA KUMLINDA PIA
GET THAT IN YOUR FILTHY MIND
Hilo nalo jipu linahitaji kutumbuliwa,itakuwaje mtu aliyejiuzulu kwa kashfa na bado anawamalizia pesa za madawati?
 
Back
Top Bottom