Lowassa amtunishia misuri Kikwete?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,556
29,642
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya mradi wa umeme wa Richmond, Edward Lowassa, sasa anaelezwa kufanya mambo ambayo ni dhahiri yanamchimba Rais wake, Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushindwa kumtetea katika “janga” lililomkuta.

Habari za uhakika zinaeleza kwamba pamoja na mkakati maalumu aliouanzisha yeye na wafuasi wake kujisafisha, Lowassa kwa makusudi kabisa ametajwa kutamka waziwazi kwamba Kikwete hakumsaidia ama alihusika katika kuanguka kwake kisiasa. Kwa mujibu wa habari hizo ambazo tayari zimekwisha kumfikia Kikwete mwenyewe, katika moja ya vikao visivyo rasmi na watu walio karibu naye Lowassa ametamka waziwazi kuhusu ‘kutoswa’ kwake na mtu anayeamini alichangia kwa kiasi kikubwa ‘kumpandisha chati’ .

Katika matamko hayo ambayo anatajwa kuyatoa wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na katika hoteli moja maarufu katikati ya Dar es Salaam, Lowassa anaapa kupambana kwa nguvu zake zote kuhakisha anarejea katika siasa kwa nguvu zote na “hata ikibidi kwa kumshughulikia Kikwete.” Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba hata kampeni za dhahiri na mikakati ya siri ilizoanza kwa nguvu kubwa wiki hii ni sehemu ya mpango huo kamambe ambao unaelezwa kupewa jina la “Agenda 21” ikiwa na malengo kadhaa ya kisiasa.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, “Agenda 21” ina mambo makuu matatu ikiwamo kumsafisha Lowassa na kundi lake “kwa gharama zozote” kazi ambayo tayari imeanza kwa utaratibu maalumu ikiwa ni pamoja na kutumia vyombo vya habari na mikutato ya hadhara kazi ambayo inafanywa kwa gharama kubwa na usimamizi “makini.”

Mpango mwingine unaelezwa ni kuhakikisha Kikwete anaanza “kuchafuliwa” kwa namna tofauti kazi ambayo itaanza wiki hii kwa kutumia kila aina ya mbinu kwa kuanzia na vyombo vya habari na propaganda za kisiasa na hatimaye kutumia Bunge kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule kuchunguza jambo litakalomgusa Rais ama Ikulu.

“Wameandaa mkakati ambao hatimaye itaundwa Kamati ya Bunge ambayo itakayoundwa kwa nguvu ya kundi hilo (la Lowassa) ili lipewe Uenyekiti wa Kamati hiyo lakini wanajipanga jinsi ya kumuingia Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ili waweze kupenyeza wajumbe wao ama wawanunue watakaoingizwa lakini hilo kwa sasa linawaumiza vichwa kutokana na msimamo na historia ya Spika dhidi ya Lowassa na wafuasi wake,” kinaeleza chanzo cha habari ndani ya serikali.

Sehemu ya tatu ambayo nayo inaelezwa kwenda sambamba na ile ya kujisafisha, kundi la Lowassa limepanga kama si kuanza kuwachimba na kuwafuatilia kwa karibu wale wote inaoamini kwamba wamehusika kwa namna moja au nyingine katika kile kilichotokea bungeni wakiwamo wabunge, waandishi wa habari na watu wengine katika jamii.

“Wataanza kwa kujaribu kuwavuta upande wao kwa kutumia mbinu na hata fedha wale wanaoamini kwamba walishiriki kwa namna moja au nyingine katika kuanguka kwa Lowassa na wakishindwa ndipo sasa watabadili mbinu na kuwashughulikia kwa mbinu chafu ili kulipiza kisasi na pia kupunguza nguvu ya ‘adui’,” anaeleza mtoa habari huyo. Inaelezwa kwa uwazi kabisa kwamba hatua zote zinazochukuliwa sasa na Lowassa na wafuasi wake zinalenga kurudisha “hadhi yake kwa haraka sana” ili kuweza kujiandaa kuchukua madaraka ya juu kabisa ya nchi baada ya Kikwete na ikibidi utekelezaji wake uwe hata kabla ya mwaka 2015 ambao ndio Kikwete atakua anamaliza miaka kumi.

“Wanajipanga na wanaweka bayana kwamba kama Kikwete hatamuunga mkono Lowassa basi wataingia katika uchaguzi hata mwaka 2010 kwa namna yoyote ile hata ikibidi kupitia chama kingine badala ya CCM, lakini uamuzi huo ni hatua ya mwisho ikiwa wataona wanakwamishwa katika malengo yao ya baadaye,” anasema mtoa habari huyo ambayo yuko karibu na wanasiasa wote wawili (Kikwete na Lowassa).

Tayari Lowassa amekwishatamka hadharani kupitia Televisheni ya Taifa (TVT) na katika mkutano wa hadhara jimboni kwake Monduli kwamba ameonewa huku akifuatiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na hatiaye Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emanuel Ole Naiko, ambaye ametoa kali kwa kusema kwamba watu wanaotoka Monduli akiwamo yeye wanaonewa.

Karamagi na Ole Naiko walipata nafasi ya kuhojiwa na Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la umeme wa dharura wa Richmond na wote wawili wameonyesha kutoridhishwa na ripoti ya Kamati hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, kupitia CCM, Dk. Harison Mwakyembe. Kwa upande wake, aliyekua Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, yeye hajatoa kauli yoyote hadharani baada ya ile aliyoitoa bungeni kujitetea na hatimaye kujiuzulu baada ya kutajwa kwake kuhusika akiwa Waziri wa Nishati na Madini wakati mradi wa Richmond ukiingizwa nchini.

Wakati yote yakiendelea, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameweka bayana kwamba atatekeleza kwa nguvu zote mapendekezo ya Kamati ya Mwakyembe, na kwamba hatoogopa wala kumuonea haya mtu yeyote, kauli ambayo inaonekana kuwa mwiba kwa wanaothubutu kujitetea ama kujisafisha mbele ya jamii.

Hii Inaonesha ni jinsi gani UROHO wa madaraka unaweza kumtia mtu upofu mpaka akawa haoni hata zile rangi za msingi.
Ifuatilieni hii news kama source inavyoonesha.

Ila kwa taarifa tu, ni kuwa shughuli imeanza na hakuna kulala mpaka wapate wanachokitaka...
 
Hii Inaonesha ni jinsi gani UROHO wa madaraka unaweza kumtia mtu upofu mpaka akawa haoni hata zile rangi za msingi.
Ifuatilieni hii news kama source inavyoonesha.
Ila kwa taarifa tu, ni kuwa shughuli imeanza na hakuna kulala mpaka wapate wanachokitaka...

Huyu Lowasa hajui kuwa anapambana nguvu anayopambana nayo. Naona nifuate alichosema Mkulu FMES, ngoja angalau atumie mapesa yake ambayo ameyakusanya kwa wizi miaka yote hii.
 
Na ole wao Waandishi waliopowa hongo kumsafisha. Ina maana ile sheri ya MoneLoundry inakuwa active kwa wauza unga tu?? nadhani hapa ndio wangechangamkia kuchunguza akaunts za hawa watuhumiwa wa ufisadi kisha na wao tungewapa credit kama PRA.

Ah maskini mmasai wa watu, anakuja na mkuki huku tumejiandaa na AK47 kalashikov
 
Hivi umekosa kichwa kingine cha mada yako? au umeshaathirika na kukopi nakuapaste ....!
 
Niajiuliza kuwa hivi kweli nchi hii ina wenye nchi au wananchi?
Kama huyu white head ataachwa kuendelea kulikashifu Bunge kwa kuikosoa Kamati Teule iliyoteuliwa na kutumwa na Bunge, na kama anaachiwa kutumia vyombo vya serikali kukanusha kuwa kahusiki na Richmond hii inaonesha kuwa kuna mkakati nyuma ya pazia kurudisha darajani.

Nina maswali mengi bila majibu
 
Kwanza huyu Lowassa ana kesi ya kujibu mahakamani, na akipandishwa kizimbani amekwisha halafu analeta jeuri. The fool is fighting a losing battle.
 
Huyu mamvi anafikiri kuwa tupo kwenye the old stone age hivi sasa tupo kwenye kizazi kingine cha dotcom where we dare to talk openly kwanini anafikiri kuwa he is only man deserved to led Tanzanians?Ushauri wa bure kwani asikubali yaishe tu kwa kukaa kimya na kuendelea na maisha ya yake ya kila siku.Another thing ni kwamba what is so special hadi anata kuwa kuwa Rais ikiwa Uwaziri mkuu umemshinda?Akiwa rais si ndio atatupiga mnada?
 
Msamee Lowasa naona hajui kama ameisha toka katika kiti cha uwaziri mkuu.

Asipo angalia atapagawa tu. Tumuombee anaweza kutembea........
 
Kama ni kweli wanajiandaa basi wote inafaa wakanyie debe ,na tatizo hapa ni kwa Muungwana kutaka wawepo karibu na ile kucheka cheka nao ndio itakayomliza asipoangalia na akitahamaki atakuwa amechelewa Waswahili wana msemo unasema udongo upate ungali mbichi na kwa msemo huo hawa baadhi ya mafisadi inafaa wafikishwe mahakamani bila ya kuoneana haya wala yale na wakitahamaki kila mmoja anachezea kifungo cha miaka hamsini kwa kusababisha maafa na shida mbali mbali kwa waTanzania hapo Muungwana na watu wake ndio watakuwa salama lakini kuwaachia wakipeta kwenye mitaa wanaweza kabisa kufanya mambo yenye uamuzi mchafu kama ilivyosenwa katika hiyo dili.
Kwa ushauri wa bure inapotokea kukamatwa au kujulikana kuwa wakuu fulani wamehusika katika ufisadi basi haifai kabisa watu hao kupewa mida ya kujipanga kwani inakuwa ni kama wanapanda mbegu ambayo itatoa mizizi na kukuwa kwa haraka.
Sioni sababu kwa nini serikali haijawapandisha mahakamani hadi leo ,hivi kuna wanalolingojea ,yaani unawapandisha mahakamani halafu unawaweka mahakimu wenye uchungu na nchi yao nisikilizie hakuna tufani wala zamana ,utasikia kesi imekwisha wamehukumiwa kunyongwa kwa kuhujumu uchumi wa Inchi na rufani inatupiliwa mbali ,maana ushahidi kwamba walikwiba ni wa wazi .si tunasikia feza wanailudisha ,hivi mlala hoi angeruhusiwa kurudisha feza ,mambo gani haya wanayafanya serikali hii kwa kweli hayajulikani na ndio kuchezea shilingi chooni ,yaani Muungwana alikuwa afunge kazi nao watu hawa tena kijeuri ukishawasweka jela ,itakuwa wamekwisha na hizo hujuma zao itabidi wapange na maafande wa magereza maana anakwambia katika jiwe hili kuna zahabu chukua nyundo na tindo uitafute ,kinachotakiwa kufanywa ni watu hawa wasikae uraiani zaidi ya miezi sita na huku wanakoanza kufanya ni kujijenga kwa haraka ili kuirudisha imani.Take care !!!
 
..taratibu. una uhakika na hili?

It is so ironic that, something so obvious to everyone in this world it is so oblivious to you. Guess what? Your guy has a case to answer sooner rather than later; in that case, don't set yourself up for surprises.
 
let me ask--how come ur 100% sure that 'ikulu' is free of richmond saga??
But if u know what i mean!!
 
Mimi nabashiri kuwa siku ya Lowassa kupandishwa kizimbani itajulikana atakapoanzisha chama cha siasa au kujiunga na chama kingine kwa lengo la kupambana na JK katika urais wa 2010. Hapo yale yanayofichwa yote yataibuka, na uchaguzi ukishaisha yanarudishwa yalikokuwa!

Yametokea kwa kina Atiku Abubakar (alikuwa mshkaji tena makamu wa Obasanjo, lakini ona alivyomgeuka!), Nawaz Sharif (Pakistan), hata Benazir Bhutto (Mungu apishe mbali lakini janga kama lile) alijulikana kwa ufisadi katika awamu zote mbili alizokaa madarakani lakini bado alikuwa "tishio" katika siasa za upinzani!

Col. Dr Kiiza Besigye (actually ni medical Lab technician) alikuwa rafiki mkubwa wa Museveni wakati wakiwa msituni wakipambana na Obote, na ndiye aliyekuwa daktari wake huko. Lakini alipotaka kupingana nae kwenye urais ziliibuka tuhuma kibao na kesi mahakamani akafunguliwa, mojawapo ikiwa ya ubakaji, kwamba ati walipokuwa msituni Besigye alibaka wapiganaji wa kike na wanawake wengine raia waliokuwa wanawakamata wanapoteka eneo! Lakini makosa hayahaya waliyafanya pamoja na Museveni, ndio iliyokuwa tabia yao porini! Tofauti ni kuwa wakati wa mashtaka mmoja ni rais na mwenzie ni mpinzani, kwa hiyo hakuna aliyeko tayari kuja kutoa ushahidi dhidi ya rais hata kama Besigye angeyasema, na zaidi kikatiba rais ana immunity!

Sasa hivi ingawa yapo mengi anayotuhumiwa Lowasa mintarafu ufisadi, na mengi ukweli wake umeonekana katika matukio ya hivi karibuni yaliyomfanya ajiuzulu, bado dalili zinaonesha hakuna atakayemshitaki bila JK kuridhia. Na akitamani sana kushitakiwa, basi amchokonoe JK kiasi cha kutosha, wakichokana tutayaona tu!
 
Back
Top Bottom