Lowassa amtaka Gavana wa Benki Kuu kueleza kwanini mfumuko wa bei haushuki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa amtaka Gavana wa Benki Kuu kueleza kwanini mfumuko wa bei haushuki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magesi, Aug 27, 2012.

 1. M

  Magesi JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Mh. EDWARD LOWASSA amemtaka Gavana wa Benki kuu kuelezea umma ni kwanini mfumuko wa bei haushuki.

  Je alipokuwa serikalini alikuwa halioni hili? Au yeye sio sehemu ya chama kinachotawala na kupeleka mawazo yake kwenye vikao vya chama?

  SOURCE: ITV DK 45
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Huyu naye kachoka vibaya! Mbona hata mtoto wa darasa la pili anajua sababu! Mfumuko haushuki kwa sababu CCM inatawala - hakuna maelezo mengine; wala wasitake kumtafuta mchawi bure wakati mchawi ni chama chao.
   
 3. K

  Kiswigo Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetoka kuangalia highlights za mahojiano ya Lowassa katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, na sasa naweza kuthibitisha hofu yangu juu ya uwezo wa mwanasiasa huyu anayewania kushika hatamu za uongozi wa nchi hii. Amemtaka Gavana wa Benki Kuu atoe maelezo kwa nini mfumuko wa bei haujashuka mpaka sasa na kwake yeye, sababu ya mfumuko huo ni dolarization ya uchumi wetu. Akijenga hoja yake, alitoa mifano ya nchi za Kenya, Uganda, Misri na Afrika ya Kusini ambako unapoingia ni lazima usajili kiasi cha fedha za kigeni ulichoingia nacho.

  Binafsi nimesikitishwa sana na ukosefu huu wa ufahamu wa mwanasiasa huyu mkongwe. Mfumuko wa bei, ambao ulifikia asilimia 24 umekuwa ukishuka kila mwezi, na takwimu za mwezi uliopita, zilizotoka mwanzoni mwa mwezi huu, mfumuko umeshuka hadi asilimia 15 na unaendelea kushuka. Takwimu hizi peke yake zinamuumbua huyu bwana. Vile vile, mfumuko wa bei hausababishwi na dolarization maana ingekuwa hivyo, mfumuko huu, ambao unachangiwa hasa na bidhaa za chakula zinazozalishwa nchini zisingeathiriwa na matumizi ya dola kama anavyodai yeye. Pili si sahihi kwamba nchi zote hizo alizozitaja zina utaratibu huo wa kusajili fedha za kigeni unazoingia nazo na mifano ya haraka hapa ni Kenya na Uganda ambao exchange control imekuwa fully liberalized.

  Mimi namshauri huyu bwana aache kukurupuka kwa nia tu ya kusikika na kujiweka relevant kisiasa. Ni vizuri akawa na washauri na kuziangalia takwimu zake vizuri. Najua anasukumwa kuongea kwa sababu mahasimu wake nao wameongea na yeye angependa kusikika. Hili tumeliona katika suala la mgogoro wa ziwa Nyasa ambapo mkubwa huyu alitangaza vita.

  Jipange mzee!
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mbona Lowassa analojibu sema hataki kukufikiri. Hivi kwa ufisadi huu na uholela anategemea nini? Hivi kwa pengo walilosababisha kwenye ufisadi wao na jamaa yake alitegemea nini? Hivi kwa ukubwa usio na sababu wa serikali yao Lowassa alitegemea nini? Hivi kwa uzembe huu na matumizi mabaya ya mali na fedha za umma unaofanywa na utawala huu alitegemea nini?Lowassa alitegemea nini kutoka kwenye utawala ulioko kwenye outpilot huku kila kitu kikifanyika kishikaji? Nadhani jibu analo Lowassa sema hataki kukubali kuwa alilo nalo ni jibu sahihi.
   
 5. T

  Tiote Senior Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakwambia mpaka 2015, nchi hii itashuhudia vituko kutoka kwa wanasiasa wakurupukaji wa aina ya huyu bwana. Nami nimemuona huku akiwa kauficha mkono wake wa kushoto ambao unadaiwa kupooza.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nitoke vip!
   
 7. n

  ndutu Member

  #7
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnamuonea baba wa watu kutaka awe na utaalam kama mchumi wakati mwenzenu kajisomea usanii. Sasa hapo takwimu zinaingiaje? Ingekuwa maigizo mngemlaumu. Mwacheni apumzike mzee wa watu!
   
 8. w

  watenda Member

  #8
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ananikumbusha Jaramogi Oginga Odinga wa Kenya ambaye aliomba aachwe atawale Kenya angalau kwa saa moja tu ili aingie kwenye kumbukumbu kwama amewahi kuwa rais wa nchi. Mnaonaje huyu bwana akaachiwa hata kwa mwezi mmoja ili naye apandishe CV yake? Ni wazo tu.
   
 9. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Amesahau bado tunalipa deni la Richmond kufidia hela aliyoweka Uswis
   
 10. C

  CHOMA Senior Member

  #10
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mwacheni Mzee wa watu anajieleza anachokielewa.Huyu ni mtu wa Media.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Muoneeni huruma mwenzenu. Hajui atoke vipi maana kila analokamata linakataa na sasa anaweweseka. Amegundua hata kuwahujumu washindani wake hakutamsaidia sana maana hiyo haimpi yeye kukubalika. Sasa kaanza kutoa amri kwa kitu ambacho hana utaalam nacho!
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu ahsante kwa kutukumbusha. Anasahau kwamba yeye ndo katufikisha hapa?
   
 13. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,497
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  katika kujenga hoja yake ange cite mabingwa wa uchumi kama reference ili kukonvice hadhira kwa sababu yeye si mchumi na hajafanya utafiti wowote
   
 14. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  dolarization contributes 61.7 pct kwenye mfumuko wa bei..mupende musipende LOWASA ndo rais wa 2015,au dr.slaa...ila kumpa membe nchi hii bora ****** aendele miaka 10 tena,membe over our dead body hawezi kuwa rais mtu mwenyewe anaongea kama kalishwa andazi,ana low iq,ni low undstandng.,kwa hli mwenyez mungu tuepushe na hili janga tuko chini ya magoti yako mola tunakuomba sana muumba wetu.amina.
   
 15. G

  George Smiley JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kuna ubaya Gavana wa benki kuu kuelezea hali ya uchumi na mambo ya mifumuko ya bei?
  In fact huyu jamaa alitakiwa kila mwezi atoe taarifa kwa umma kuelezea hali ya uchumi na hii mifumuko ya bei.
  unless you have other ideas
   
 16. N

  Nipe tano Senior Member

  #16
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TeteteteeEee
   
 17. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona majibu anayo mwenyewe EL jamani? Jibu ni sababu yeye kaficha budget ya tz ya Mwaka mzima UAE Sijui SWS alafu anamtoa kafara gavana?? Tajaneni tuu pole pole
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mwacheni aendelee na kubwabwaja huyo!!!!!
   
 19. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Umelonga vizuri sana mkuu sasa pitia mtaa wa UFIPA kachukua chako kwa kazi nzuri za leo
   
 20. b

  banyimwa Senior Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa nani ana IQ ndogo hapa kama siyo wewe ambaye umehamisha mada na ujinga aliouonyesha huyo mungu wako? Mimi nafikiri haya ndiyo mambo yanayochangia kuzorota kwa afya ya Lowassa. Obsession yake katika kumshambulia Membe bila mafanikio imemuweka katika hamaniko linalomuumiza sana hata kuathiri afya na uwezo wake wa kufikiri. Wewe unasema atakuwa Rais 2015 wakati walio karibu naye wanalia kwamba afya ilivyozorota, hata huko 2015 ni mbali!
   
Loading...