Lowassa amponza Kibanda: Taarifa za awali zahusisha kutekwa na urais 2015

mpotezee huyu.

turudi kwenye mada nimejiuliza mambo mengi sana juu ya hii mada, ina maana basi waliomshambulia Kibanda wanahusishwa na upinzani?? kama ndio kwann iwe hivyo na wala isiwe ni CCM ambao sio wa kambi ya lowassa??

sijasema kama ndivyo ila nina jaribu ku speculate tu
Hapana!! Tafsiri yake ni kwamba anahusishwa Bernard Membe....Membe ndie hasimu mkubwa wa Lowasa 2015.....Membe hata kama hajatamka hadharani, lakini anaamini magazeti ya Habari Corporation yanamchafua....!!
 
...mwisho wa siku mambo yote yatakua hadharani, si mbali sana...whether ni upinzani, serikali au yeyote anayehusika...tuombe uzima tu.
 
sema ndio shida ya kutumia taaluma yake kuganga njaa.hakuwa objective kama KUBENEA.

aiseeeeeeeee...................sasa hivi MEMBE ndugu wa damu wa KIKWETE ndo awe rais wetu kweli?? hata kama ni kurithishana sio hivi. so far nafkiri watanzania tunahitaj sura mpya kabisa kwenye uongozi ujao sura ambazo zitaleta matumaini mapya kwetu. sura ambazo zitabadili hali za maisha ya watanzania ila hizi za bwagamoyo za kuzaliwa na kichwa na nazi hatuzitaki
 
''Katika hatua nyingine, TEF imeunda jopo la waandishi wa habari kwa ajili ya kuchunguza tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Kibanda''

Nadhani aliyetuloga katika huu upuuzi wa kuunda jopo au tume hapa Tz ameshafariki........

 
Nchimbi tangaza,

'Huu siyo ujambazi bali ni ugaidi. Ndani ya CCM kuna magaidi ambao wanatakiwa kusakwa kwa kutumia nguvu zote za ndani na nje ili yaangamizwe'.

Kama CCM wanauana na kutaka kuana wenyewe kwa wenyewe, je, wataweza kuwa na uchungu na wasio wanaCCM? Watanzania wote, chini ya CCM, maisha na usalama wetu vipo mashakani.

Wawaongezee kazi wale FBI.
 
Nimeisikiliza hiyo video kwenye YouTube. Kwa kweli nitashangaa ikiwa Lwakatare bado yuko nje hajaswekwa lubango mpaka sasa. Huyu jamaa ni shushu mstaafu, naona ushushu wake anauendeleza CDM.
 
HHHHHHHIIIIIIIIIIIIIIMMMMMMMMMMMMMMMMMM Hadi uchaguzi sijui watakuwa wangapi,inabidi tusali sana kuepusha balaa linalokuja kwa nchi yetu hatuna ufundi na mambo haya
 
Uoga wangu usije ukawa ni yale mambo ya Said Kubenea, mambo ya kishenzi na wake za watu huku wakidai eti ni maswala ya kisiasa!!

Swali langu ni moja tuu: Hivi katika siasa za Tanzania kweli mwandishi wa habari amekuwa muhimu/tishio kihivyo mbaka waanza kuwa eliminated? Sipati picha hiyo kwa kweli, hata kidogo!!
 
Naona awamu hii ya jk imekuja na uhuru uliopitiliza hadi wa wanaoitwa majambazi kufanya utekaji na kuondoa roho za wale wanaolitakia Taifa mema. Uhuru wao una mipaka
 
..........Maswali Mengi....Risasi hiyo ni silencer ? Mbona Kibanda mwenyewe hajaongelea mambo ya risasi.. pale kwenye tukio kuna ganda la risasi lililookotwa?

Na hili pia aulizwe Wilfred Rwakatare, Kiongozi wa Mipango ya Mauaji
 
Back
Top Bottom