Lowassa ammwagia sifa Mkapa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Lowassa ammwagia sifa Mkapa

Na Haika Kimaro, Mwananchi

Jumanne,Decemba3 2013 saa 9:43 AM
Kwa ufupi

  • Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Masasi mkoani Mtwara katika harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKI) katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi.

Masasi. Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amemmwagia sifa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kuwa ni kiongozi aliyeliongoza taifa kwa uadilifu na umakini.

Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Masasi mkoani Mtwara katika harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKI) katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi,

“Nimefika hapa kwa heshima. Nimefika hapa Masasi kutokana na kwamba wilaya hii imetoa kiongozi, Rais Benjamin Mkapa aliyeliongoza taifa kwa umakini, uadilifu na ushupavu mkubwa.

Lowassa ambaye wakati wa uongozi wa Serikali ya Mkapa alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) kabla ya kupelekwa Wizara ya Maji na Mifugo, alisema lazima Watanzania wampe heshima yake na kumuenzi kutokana na kile alichokifanya kwa Taifa.

Mbali na hayo, Lowassa alisema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote mwenye nia ya dhati ya kupambana kuondoa umaskini katika jamii kwa kuwa yeye ni mdau wa wanaopambana na kuondoa umaskini katika jamii.

“Mtu yoyote anayepambana na kuondoa umaskini katika jamii, kwa kweli mtu huyo niko tayari kushirikiana naye katika harambee za harakati hizo,” alisema Lowassa na kuongeza kuwa wanawake ni jamii inayochukia umaskini.

“Wanawake ni wadau wakubwa katika kupambana na umaskini, na ndiyo maana chama changu cha CCM katika Rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya uwakilishi bungeni na kwamba chama hicho kinawathamini sana kinamama wote nchini.

Aidha, katika harambee hiyo, zaidi ya Sh103 milioni zilipatikana huku marafiki zake wakichangia Sh10 millioni na kuvuka lengo ambalo lilikuwa Sh100 milioni.
 
Fisadi Mkapa aliyehusika na ufisadi wa Rada, EPA, ukwapuzi wa nyumba za Serikali, kufanya biashara akiwa Ikulu, kuuza mashirika ya umma kwa bei ya kutupa ikiwemo National Bank of Commerce, kuiba Kiwira Coal Mining, kuingiza nchi katika mikataba ya uchimbaji wa dhahabu ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania, kuwaingiza makaburu wa Net Group Solutions kuchukua management a TANESCO kwa mtutu wa bunduki leo hii tunaambiwa aliiongoza nchi kwa umakini, uadilifu na ushupavu mkubwa!!!! Fisadi anamsifia fisadi mwenzie ili apigiwe debe 2015!!!!
 
Nadhani lowasa amepotoka kidogo, kwakweli uadilifu haukuwepo!
angesema hiv slogani ya mkapa ya "mtaji wa maskini ni nguvu yake mwenyewe" kuliko ya jakaya ya"maisha bora kwa kila mtanzania" ambayo imeprove failure,
ya mkapa at least alijitwalia baadhi ya makampuni!
 
Mkuu huyu fisadi kapotoka sana na wala si kidogo. Kwanini anaukimbia ukweli wa utendaji wa fisadi Mkapa wakati Watanzania wengi tunaufahamu!? Unafiki kitu kibaya sana.

Twende kazi
 
We jamaa ni mnafiki kiukweli
 
Unaona wanohamisha magoli, mtawajua kwa matendo yao. Leo kishahamisha goli liko nje ya uwanja kabisa.
 
Hakuna popote pale nilipohamisha goli weka uthibitisho wa kuonyesha kwamba siku za nyuma niliandika hivi na hivi karibuni niliandika tofauti na kile nilichoandika siku za nyuma. Kama ushahidi kama huo upo uweke hapa tuujadili badala ya kukurupuka.

Unaona wanohamisha magoli, mtawajua kwa matendo yao. Leo kishahamisha goli liko nje ya uwanja kabisa.
 
Fisadi Mkapa aliyehusika na ufisadi wa Rada, EPA, ukwapuzi wa nyumba za Serikali, kufanya biashara akiwa Ikulu, kuuza mashirika ya umma kwa bei ya kutupa ikiwemo National Bank of Commerce, kuiba Kiwira Coal Mining, kuingiza nchi katika mikataba ya uchimbaji wa dhahabu ambayo haina maslahi kwa Tanzania na Watanzania, kuwaingiza makaburu wa Net Group Solutions kuchukua management a TANESCO kwa mtutu wa bunduki leo hii tunaambiwa aliiongoza nchi kwa umakini, uadilifu na ushupavu mkubwa!!!! Fisadi anamsifia fisadi mwenzie ili apigiwe debe 2015!!!!
Fisadi anamsifia fisadi mwenzie.....

Leo hii jik imefanya kazi.....watu wasafiii.....
 
Hebu tuwekee huu uthibitisho wa huo unafiki wangu mstari kwa mstari kwa nilichokiandika hapo juu badala ya kukurupuka.

Hujitambui wewe mburula unakurupuka kuandika kitu ambacho huna uthibitisho.

We jamaa ni mnafiki kiukweli
 
Hebu tuwekee huu uthibitisho wa huo unafiki wangu mstari kwa mstari kwa nilichokiandika hapo juu badala ya kukurupuka.

Hujitambui wewe mburula unakurupuka kuandika kitu ambacho huna uthibitisho.
Kwahiyo uwa unatetea mabadiliko yapi ndugu??
 
Kwani wewe huko uliko unatetea mabadiliko yapi? Hebu tuwekee mabadiliko ya huko uliko? Usisahau tumeona Lugumi aliyepora 37 billion na kukingiwa na huyu dikteta uchwara. Je, maoni yako kuhusu kukingiwa kifua mwizi na fisadi Lugumi ni yepi!? Na huyo aliyejinadi kwamba kajitoa kafara kupambana na mafisadi hata kuitamka tu Lugumi kashindwa.

Kwahiyo uwa unatetea mabadiliko yapi ndugu??
 
Kwani wewe huko uliko unatetea mabadiliko yapi? Hebu tuwekee mabadiliko ya huko uliko? Usisahau tumeona Lugumi aliyepora 37 billion na kukingiwa na huyu dikteta uchwara. Je, maoni yako kuhusu kukingiwa kifua mwizi na fisadi Lugumi ni yepi!?
Mkuu Mimi kwangu fisadi ni fisadi tu uwa sina unafiki Lowassa, JK,Sumaye ni mafisadi tu na wala alina mjadala!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama una akili timamu na ukazidhikabidhi kwa wanasiasa, matokeo yake ndio haya!

Kama huna akili timamu na ukaendelea kuwa kibendera, hakuna mtu mwenye akili timamu atakushangaa kama anakufahamu huna akili timamu!
 
Hapo tunakubaliana kabisa Lowassa ni fisadi, Mkapa ni fisadi, Sumaye ni fisadi, Magufuli ni fisadi na Kikwete pia ni fisadi. Ingekuwa amri yangu Lowassa na Sumaye wasingepokelewa CHADEMA, lakini huo ubavu sina.

Mkuu Mimi kwangu fisadi ni fisadi tu uwa sina unafiki Lowassa, JK,Sumaye ni mafisadi tu na wala alina mjadala!!
 
jamaa anatamani angekua amejiunga jf mwaka huu. hahaha ngoja tuendelee kufokonyoa nyuzi zake za zamani tuone vichekesho
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom