Lowassa amkatia Rufaa Kikwete: Hawa gazeti la mwanahalisi vp? Hawana habari mpya?

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
EDWARD Lowassa, mwanasiasa anayetajwa “kujipanga kugombea urais mwaka 2015,” ametinga nchini Nigeria kufanya maombi, MwanaHALISI limeelezwa.
Taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki zilisema, Lowassa aliondoka nchini Ijumaa. Alikutana na Nabii Joshua na kushiriki katika misa ya pamoja iliyofanyika Jumapili iliyopita.
Maombi haya, kwa mujibu wa mmoja wa wabunge wafuasi wake, yanalenga “kukata rufaa kwa nabii, kutafuta utakaso kisiasa, kupata nguvu na ujasiri” kabla ya kuingia katika kinyang’anyiro cha nafasi ya juu ya kisiasa nchini.
Misa ya Nabii ilionyeshwa katika Emmanuel TV ya Nigeria ambayo inaonekana duniani kote. Angalau watu watatu wa jijini Dar es Salaam na mmoja aliyeko Swaziland, wameliambia gazeti hili kuwa wamemwona Lowassa akiwa katika jumba la maombi la Nabii Joshua.
Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambamo Lowassa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kujisafisha na kujitetea ili asiweze kufukuzwa kutoka ndani ya chama chake........Muenedelezo soma website ya Mwanahalisi.

Hana habari mpya au kapewa pesa huyu kubenea?
 
Mwanahalisi linatia kinyaa kwa Habari za kila siku za Lowasa, nikiliona tu lazima nitapike, maana sasa ni too much!!!!!
 
Back
Top Bottom