Lowassa amjibu Kinana huko Pemba!

Huyu amiri jeshi mkuu mwoga atakuwa wa kwanza duniani, ukisema huogopi kwa maana nyingine unaweza ogopa pia.
 
Soma kwanza uelewe alichoeleza mkuu, soma soma soma kwanza kabla ya maoni yako! Labda kama utahitaji ufafanuzi juu ya maelezo yake

nimeelewa kama mleta uzi alivyoleta kuwa kama sheria hazikufuatwa atamwachia huru, sasa kama sheria hazijafuatwa si mahakama itawachia huru na kama watapewa hukumu isiostahili siwatakata rufaa! Tatizo liko wapi hadi rais aamuru waachiwe huru?
 
Suala la sheikh farid wa uamsho liko mahakamani anaposema atamwachia hapo anaingilia uhuru wa mahakama. Kuna tatizo gani sheria kuchukua mkondo wake?

Inamaana akiwa rais hakuna haja ya kuwa na mhimili wa mahakama na ofisi ya DPP? Kwani mashauri atakuwa anaamua sebuleni kwake! Utakuwa utawala wa hovyo sana.

Wakuu Salaam!

Napenda kunukuu neno kwa neno kadri nilivyosikia Mzee Lowassa akielekeza maneno yake kwa Mzee Kinana.

"Kuna mtu mmoja mwenye mamlaka kwenye Chama, tena Muislam, akaandika barua kwenye gazeti moja nchini MAREKANI, gazeti maarufu kidogo." Akasema 'LOWASSA ANAPENDA MAGAIDI NA ATAENDELEZA MAGAIDI, na AKICHAGULIWA kuwa RAIS ATALETA UGAIDI NCHINI'.

Lowassa anaendelea...Sasa nataka nirudie majibu yangu kwake na kwa waTanzania...nilisema 'NITAZINGATIA SHERIA KUCHUNGUZA KAMA WALE MA - SHEIKH WAMEONEWA na KAMA TARATIBU ZA KISHERIA ZILIFUATWA na KAMA HAZIJAFUATWA NITAWATOA NJE mara MOJA , sasa NAMRUHUSU HUYO ANAETAKA KUSHTAKI DUNIANI AKASHTAKI KOKOTE, angojee TU NIWE RAIS.

Anaendelea Lowassa...Nchi hii ina AMANI kwa sababu TUNAHESHIMIANA hakuna watu wenye HATIMILIKI wa nchi hii kwamba wanachosema wao ni sawa. Mimi nimesema jamani nitachunguza upungufu wa sheria na nitachukua hatua wala SIOGOPI NG'O. kamaliza

MY TAKE:wiki kazaa zilizopita Mzee KINANA aliandika article katika blog ya The HILL tukasoma, Mzee LOWASSA nae kasoma kisha akakaa kimya lakini jana akiwa Pemba hayo ndio majibu yake! Aksante.

Kwa faida yako wewe unaechangia bila kusoma
 
hamjitambui, anatumia kutokumfaham kwenu na udhaifu wetu kuwatumia kama daraja la kutimiza yake. Kashakwambia akishinda yy atashugurika na mama lishe na bodaboda je na ww mama lishe au bodaboda? Huyu mtu tapeli hana maono ya kulifikisha taifa hili ktk maendeleo endelevu, akataliwe kwa njia yoyote ile
Pamoja na madhaifu yake, ndugu yangu hayo makundi ni hatari kwa usalama wa nchi na utawala wowote. Ni mabomu yaliyotegwa na yanaweza kulipuka muda wowote. Hakuna mgombea wa urais anayeyakashifu au kuyaweka pembeni. Nafikiri kikubwa unachoweza kumsifia Lowassa ni uwezo aake wa kuvumilia na kukaa kimya bila kuropoka anapochokozwa au kutukanwa. Binafdi siwezi.
 
hapo kweli ameongea kama raisi kura yangu kwako Inshallah nikifika hiyo tarehe 25
 
mzee edo kura yangu na kura za familia yangu umezipata zote kwa hekima ulizoonyesha, ukiwa na mzazi ambaye anakurupuka ni shida sasa je president akiwa mtu wa kukurupuka ni nihatari zaidi, pia nataka Edo akachunguze pia na mkataba wa gas ya ntwara
 
Kila nikimuwazia Lowassa sipati jibu,zaidi natamani kila mtu awe kama mimi.
Yaani tumchague ashinde kwa kishindo...naiona Tanzania mpya chini ya Lowassa.

Acha akili za mavi hizo, ww ni kijana kweli watz au ni mkimbizi, wewe umeona jipya gani kwa huyo mzee, ambalo unaweza kusimlia wenzio, yani kwa ujinga ulionao unaona Lowasa mpole sana co, au umemjua jana baada ya kuingia chadema? tena inaonekana bado una tongotongo nyingi sana usoni kwako na pia inawezekana ndo itakuwa mara ya kwanza ww kupiga kura, funga domo lako hilo!
 
huyu mzee jamani..au ndo katumwa na Mungu kuja kutuokoa watanzania..

alaf tizama wale wote wanaomtukana wanatangulia mbele za haki

wewe wangapi umewatukana na bado hujatangulia...acheni hizo tuache Mungu afanye kazi yake!!!
 
huyu mzee jamani..au ndo katumwa na Mungu kuja kutuokoa watanzania..

alaf tizama wale wote wanaomtukana wanatangulia mbele za haki

Ni kweli kabisa ndugu; Watu wanasema Lowasa ni fisadi mara mgonjwa, lakini wanashindwa kuelewa kuwa wakati mwingine Mungu hutumia watu waovu, dhaifu kuleta neema. Angalia wana wa Israel wakati wanaingia nchi ya ahadi, Rahabu ambaye alikuwa kahaba sana ndiye aliwaficha wapelelezi na kuwawezesha kufanya upelelezi na hatimaye wakaingia Kaanan. Paulo ambae ameandika vitabu vingi vya nyaraka hapo mwanzo aliitwa Sauli na ndiye alikuwa kiongozi wa mauaji ya Wakristo na vitabu vyake kuanzia Warumi hadi Waebrania tunavitumia. Inawezekana na mpango wa Mungu kumtumia fisadi kuleta neema kwa Tz.
 
Huyu mzee Lowasa binafsi kuna vitu vingi vya kujifunza toka kwake kiukweili....Mwenyezi Mungu amjalie afya njema na kumpigania zaidi.
 
Anajisumbua waislam hakuwatetea mashekhe yuko ccm waislam tunajua nini tutafanya hata aseme atatujengea chuo kikuu cha waislam hatukupi ng'o
 
jangwani alisema atawatoa tu.... jana kabadilika ili apate kura za waislam wengi ambao kitakwimu wapo huko zanzibar... baada ya hao waislam kutokuwa na imani nae pale alipoomba kura kwa kigezo cha udini na ulutheri pale tabora
 
Back
Top Bottom