Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Pinda awafunika Lowassa Pinda na Ole Sendeka-Makampuni yapitia kwake
MBUNGE wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa pamoja na marafiki zake na kampuni binafsi, wamechangisha Sh milioni 34.5 kwa Kamati ya Maafa ya Mererani ifanye kazi yake ya uokoaji kwa uhakika na kuwa na vifaa vya kisasa.
Lowassa alizitaja kampuni zilizochangia ni MMT Ltd ambayo ilichangia Sh milioni tano, Kampuni ya simu ya Vodacom ilitoa Sh milioni 20, Kampuni ya mafuta ya Oil Com ilitoa Sh milioni mbili, Kampuni ya Utalii ya Muyomba ilitoa Sh milioni mbili na Kampuni ya Caspian ilitoa Sh milioni tatu.
Mbunge huyo ambaye juzi alitembelea mafuriko katika jimbo lake, katika maafa hayo ya Mererani alichangia Sh milioni mbili na kuwataka viongozi wa Kamati ya Maafa kuhakikisha fedha hizo zinazochangwa na kampuni na watu binafsi zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu hadi Februari mwaka huu alipojiuzulu, alisema serikali pekee isiachiwe katika masuala ya fedha kwani ina majukumu mengi ya kitaifa, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuchangia maafa hayo.
Katika kuboresha kamati hiyo, serikali imetoa Sh milioni 49.9 kutoka katika mfuko wake wa maafa kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji miili ya watu waliokumbwa na mafuriko katika machimbo ya madini ya tanzanite yaliyopo Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, alisema fedha hizo zimeshafika mikononi mwake na tayari zimewasilishwa katika akaunti maalumu iliyofunguliwa katika Benki ya NMB tawi la mjini Arusha.
Shekifu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, alisema bajeti kamili ya fedha kwa shughuli za uokoaji miili hiyo ni Sh milioni 128, hivyo amezitaka taasisi, kampuni na watu binafsi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanachangia mfuko huo ili shughuli hizo zifanyike kwa urahisi na haraka.
Alisema fedha ni muhimu katika shughuli hiyo kwani katika bonde lililopitisha maji bajeti yake pekee inahitaji Sh milioni 25 ili kuweka mtaro wa kuzuia maji kutoingia kirahisi katika machimbo hayo ya kitalu B na bila kufanya hivyo maafa yatakuwa yakitokea kila mara.
Mfuko huo kwa sasa una fedha taslimu Sh milioni 27 na hundi Sh milioni mbili na kutokana na msaada kutoka Serikali Kuu, huenda kwa kiasi fulani zoezi la uokoji litafanikiwa. Alizipongeza Benki za NMB na Standard Chartered kwa pamoja kwa kila benki kutoa Sh milioni 10, alisema.