Lowassa amfunika Pinda: Makampuni yapitia kwake

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2007
Messages
310
Points
195

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Joined Dec 23, 2007
310 195
Pinda awafunika Lowassa Pinda na Ole Sendeka-Makampuni yapitia kwake

MBUNGE wa Monduli mkoani Arusha, Edward Lowassa pamoja na marafiki zake na kampuni binafsi, wamechangisha Sh milioni 34.5 kwa Kamati ya Maafa ya Mererani ifanye kazi yake ya uokoaji kwa uhakika na kuwa na vifaa vya kisasa.

Lowassa alizitaja kampuni zilizochangia ni MMT Ltd ambayo ilichangia Sh milioni tano, Kampuni ya simu ya Vodacom ilitoa Sh milioni 20, Kampuni ya mafuta ya Oil Com ilitoa Sh milioni mbili, Kampuni ya Utalii ya Muyomba ilitoa Sh milioni mbili na Kampuni ya Caspian ilitoa Sh milioni tatu.


Mbunge huyo ambaye juzi alitembelea mafuriko katika jimbo lake, katika maafa hayo ya Mererani alichangia Sh milioni mbili na kuwataka viongozi wa Kamati ya Maafa kuhakikisha fedha hizo zinazochangwa na kampuni na watu binafsi zinafanya kazi iliyokusudiwa.


Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu hadi Februari mwaka huu alipojiuzulu, alisema serikali pekee isiachiwe katika masuala ya fedha kwani ina majukumu mengi ya kitaifa, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuchangia maafa hayo.


Katika kuboresha kamati hiyo, serikali imetoa Sh milioni 49.9 kutoka katika mfuko wake wa maafa kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji miili ya watu waliokumbwa na mafuriko katika machimbo ya madini ya tanzanite yaliyopo Mererani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekifu, alisema fedha hizo zimeshafika mikononi mwake na tayari zimewasilishwa katika akaunti maalumu iliyofunguliwa katika Benki ya NMB tawi la mjini Arusha.


Shekifu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, alisema bajeti kamili ya fedha kwa shughuli za uokoaji miili hiyo ni Sh milioni 128, hivyo amezitaka taasisi, kampuni na watu binafsi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanachangia mfuko huo ili shughuli hizo zifanyike kwa urahisi na haraka.


Alisema fedha ni muhimu katika shughuli hiyo kwani katika bonde lililopitisha maji bajeti yake pekee inahitaji Sh milioni 25 ili kuweka mtaro wa kuzuia maji kutoingia kirahisi katika machimbo hayo ya kitalu B na bila kufanya hivyo maafa yatakuwa yakitokea kila mara.


Mfuko huo kwa sasa una fedha taslimu Sh milioni 27 na hundi Sh milioni mbili na kutokana na msaada kutoka Serikali Kuu, huenda kwa kiasi fulani zoezi la uokoji litafanikiwa. Alizipongeza Benki za NMB na Standard Chartered kwa pamoja kwa kila benki kutoa Sh milioni 10, alisema.
 

RR

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2007
Messages
6,845
Points
1,500

RR

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2007
6,845 1,500
Sorry for the asking ..... how is the headline related to the story, I couldnt find Pinda in the story. And what is the source for this?
 

Power to the People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2007
Messages
1,201
Points
1,500

Power to the People

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2007
1,201 1,500
Mbunge huyo ambaye juzi alitembelea mafuriko katika jimbo lake, katika maafa hayo ya Mererani alichangia Sh milioni mbili na kuwataka viongozi wa Kamati ya Maafa kuhakikisha fedha hizo zinazochangwa na kampuni na watu binafsi zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Kama hii habari ni ya kweli, Do these people think before they speak! ni mapesa kiasi gani hayakuwafikia walengwa wakati ulipopewa dhamana ya kutetea na kusimamia maslahi ya wananchi? leo hii umetoa vimilioni viwili unangangania ziwafikie walengwa. please kama mtu hana kitu cha kusema ni heri anyamaze tu.

Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu hadi Februari mwaka huu alipojiuzulu, alisema serikali pekee isiachiwe katika masuala ya fedha kwani ina majukumu mengi ya kitaifa, hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuchangia maafa hayo.
hapa umekosea kidogo ulitakiwa useme serikali ina majukumu mengi yasiyo na umuhimu wa kitaifa Kama vile kuilipa richmond.
 

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,561
Points
1,195

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,561 1,195
Paparazi muwazi your cridibilty is getting worse as day goes on, hueleweki kaka umetumwa nini? Nani kamfunika mwenzake? PINDA yeye kachangisha KIASI gain?
 

DMussa

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2007
Messages
1,314
Points
1,225

DMussa

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2007
1,314 1,225
Headline = UDAKU
Main Story = Looks like ok though i don't find Pinda in it!!
Amazing spin!
Duh!!!?
 

IsayaMwita

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2008
Messages
1,124
Points
1,195

IsayaMwita

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2008
1,124 1,195
Mambo mperampera, unaposhindwa kujieleza ukafahamika unachokisema hapo ndipo tunasema wewe huwezi kumsafisha Lowasa na mafisadi wenzake, wewe kama hauna story ongelea hata majanga ya mvua hapa Tanzania.
 

Forum statistics

Threads 1,367,466
Members 521,746
Posts 33,399,059
Top