Elections 2015 Lowassa alivyoipaisha CHADEMA katika uchaguzi huu, ni asset na ataendelea kuwa asset

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Dr. Wa mihogo soma hii

LOWASSA ni "Asset au Liability.

-Kabla ya ujio wa Lowassa ndani ya chadema, chadema ilikuwa na majimbo 23 tu na viti maalumu 26 na kuwa na wabunge 49 ktk bunge la 10 la 2010-2015, ujio wa Lowassa umeongeza wabunge kutoka majimbo 23 mwaka 2010 hadi majimbo 35 mwaka 2015 na viti maalumu kutoka 26 hadi 43 na kufanya jumla ya wabunge wa chadema 78 ktk bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chama cha upinzani tangu Tanzania ipate uhuru, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Kabla kuondoka kwa Lowassa ndani ya ccm, ccm ilikuwa na wabunge wa viti maalumu 79 mwaka 2010, sasa ccm itakuwa viti maalumu 62 tu kwa maana hiyo nguvu ya Lowassa imeondoka na viti maalum 17 ambao wote imebidi wapewe chadema, na ndiyo maana sasa chadema itakuwa na viti maalumu 43, which means, chukua viti 26 vya cdm 2010 + viti 17 alivyokuja navyo Lowassa = 43, Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Mwaka 2010-2015, ccm ilikuwa inapokea ruzuku zaidi ya 78% ya ruzuku yote ya vyama vya siasa kutokana na kura za urais alizopata JK, mwaka huu ccm itapokea ruzuku isiyozidi 59% ya ruzuku yote ya vyama ni sawa pungufu ya 20% waliyopoteza ccm, Na kwa mara ya kwanza chama cha upinzani chadema kitapokea 40% ya ruzuku yote ya vya siasa, hii ni kutokana na kura mil 6=39% alizopata Mhe. Lowassa. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"

-Kabla ya ujio wa Lowassa, katika majiji matano (5), Mbeya, Dar, Tanga, Mwanza & Arusha, cdm ilikuwa haiongozi hata jiji moja kati ya hayo kwa mwaka 2010-2015, yote yalikuwa chini ya ccm, Ujio wa Lowassa umeifanya chadema kuongoza majiji 4 (Mbeya, Dar, Arusha & Tanga japo Tanga itakuwa chini ya UKAWA) kutokana na ushindi wa madiwani wake ktk majiji hayo na ccm imebaki na jiji la Mwanza pekee, which means ccm imepoteza majiji 4 kutokana na kuondoka kwa Lowassa. Je Lowasa ni "Asset" au "Liability"


-Mwaka 2010-2015 chadema ilikuwa inaongoza halimashauri 5 nchi nzima mfano: Moshi & Karatu, mwaka 2015 kwa mara ya kwanza chadema itakuwa inaongoza halimashauri 30 Tanzania hii ni kutokana na Ushindi wa madiwani na wabunge ktk halimashauri husika. Je Lowassa ni "Asset" au "Liability"



NB: Kwa mtu wa kawaida na anayefikiria ya leo bila kujua kesho itakuwaje alibeza ujio wa Lowassa ndani ya chadema, lakini kwa anayefikiria leo na kesho na kuangalia kwa jicho la tatu atakuwa amegundua umuhimu wa ujio wa Mhe. EDWARD LOWASSA.

Ahsante...!!!
 
lowassa atabaki katika historia ya taifa kwa kuleta upinzani wa kweli
 
Hakuna zaidi ya lowassa nchi hii....hata CCM wanajua
 
The Don, the King... mzee wa maamuzi Magumu
.EL... ahsante kwa kupiga tafu mabadiliko ya kweli Tz.. . Zenj wameisha ipoteza maana waliweka nguvu sana huku wakikuogopa wewe....
 
Katika jamii utapata heshima kwa kufanya biashara halali yenye kukupatia faida nzuri. Lakini ukifanya biashara haramu kama kuuza bangi au madawa ya kulevya, utapata faida kubwa lakini heshima yako katika jamii itashuka sana. Ni lazima kulinda heshima kuliko kukimbilia mapato ya aibu. Nyerere alilinda heshima yake ndo maana hadi leo fikra zake zinadumu. Hakuwahi kubadili gia angani. Ni liability.
 
Katika jamii utapata heshima kwa kufanya biashara halali yenye kukupatia faida nzuri. Lakini ukifanya biashara haramu kama kuuza bangi au madawa ya kulevya, utapata faida kubwa lakini heshima yako katika jamii itashuka sana. Ni lazima kulinda heshima kuliko kukimbilia mapato ya aibu. Nyerere alilinda heshima yake ndo maana hadi leo fikra zake zinadumu. Hakuwahi kubadili gia angani. Ni liability.

Shkamoo kaka, umemaliza yote
 
Dr. Wa mihogo soma hii

LOWASSA ni "Asset au Liability...?"
LOWASSA ni "Asset au Liability...?"

*Fuatilia utapata jibu...[/QUOTE

Unatoa harufu,
Kwa Pamoja Dr Slaa n Prof Lipumba 2010 walipata 27% n 11% za urais respectively Jumla 38/9%

Mwaka huu Lowassa akiwakilisha vyama vinne kapata 39%

2010 Dr Slaa akitoka Wabunge 5 hadi 24/5,waliongezeka nearly 19, mwaka huu wameongezeka wangapi we pimby

Mnajifanya kuziba pamba maskio, dozi inazidi kuwaingia. Hadi 2020 mtabakiza Wabunge kumi. Maana hata Dar inarudi CCM
 
Watu wengi vichwa na akili zimechoka kama sio kuchoshwa na kubeba mabox hasa huyu anayejiita mwanakiji. Unapomlinganisha slaa na lowasa yako mambo mengi ya kuangalia

Sio kila siku unang'ang'ania jambo hilo tu mnachosha, slaa pamoja na lipumba walifanya sehemu yao na lowasa kafanya yake pia. Kama ni kura kuibwa lowasa atakuwa ameibiwa kimkakati zaidi ya slaa, na watanzania wengi walimchagua hata wewe mwanakijiji unajua, wabunge wa ukawa wameongezeka madiwani wameongezeka halmashauri zimeongezeka umoja wetu kama ukawa umeimarika ingawaje huyo slaa na lipumba walitarajia tusambalatike.

Mnadanganya watu na kuwapotosha kwa Maana mnakaa mijini mnaweza kupata milo angalau 2 nendeni vijijini muone uhalisia wa maisha ya watanzania huko acheni unafiki humu.

Mmeliingiza tingatinga subirini lianze kutingatinga hiyo ndio ccm unaweza kuwa mzuri ukiwa nje ukiingia utaambiwa ya kufanya na chama maana ndio kinashika hatamu. Niliemkubaliga ccm ni marehem sokoine na mwl tu katika utendaji wao walijitahidi kusaidia sana watanzania
 
Eti hata dar inarudi ccm unaongea huku povu linakutoka ikifika 2020 tukiwa hai ccm dar bye bye bye mwaka huu mngebaki na jimbo moja tu kama sio figisu figisu
 
Watu wanachanganya impact ya Lowasa na Ukawa, Muungano wa Ukawa ndio umesaidia wapinzani kupata wabunge wengi, huko nyuma vyama vya upinzani vilikuwa vinagawana kura na kuifanya CCM inashinda kiulaini. Mfano mzuri ni majimbo ya Segerea na Kigamboni
 
Hamjakoma bado... aah well hatuwezi kuwasaidia hadi hivi sasa. Ukweli utaendelea kuwakodolea macho mpaka mtakapoukiri.

Endelea kulamba miguu ya dr. mihogo tu lowassa ataendelea kwa asset kwa ukawa na hata ccm wana lifahamu ilo
 
Back
Top Bottom