Lowassa alishabikia mfumo wa elimu ya Misri sasa asemaje????????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa alishabikia mfumo wa elimu ya Misri sasa asemaje?????????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 27, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Wengi tutakuwa tumesahau lakini katika utawala wa Mkapa Lowassa alikuwa Waziri wa maji na katika pita pita zake kule Misri alifahamishwa ya kuwa kwa mwaka Misri inazalisha wakufunzi wa elimu ya Chuo kikuu zaidi ya 750, 000.

  Ndugu yetu Lowassa alistaajabu na aliporudi nchini kitu cha kwanza alichokifanya ni kuitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo aliwasimulia juu ya ufahamu wake huu mpya.......................................Misri inazalisha University graduates zaidi ya 750, 000 wakati sisi tunazalisha 5, 000............................."How can we compete?"...........................Aliuliza Mheshimiwa Lowassa.......................

  Jambo ambalo wenyeji wake kule Misri hawakumfahamisha au walimficha ni kuwa asilimia 98 ya wahitimu hao huwa hawapati ajira wala kuwa na uwezo wa kujiajiri kwa sababu hakuna miundo mbinu au nia ya dhati kutoka kwenye kisima cha watawala kufanya hivyo..................................................


  Alipopata U-PM........Lowassa akaongoza mapinduzi ya elimu na kuweka kando ubora wa elimu ili kutunisha idadi ya wahitimu..................hiyo ni sera ambayo utekelezaji wake ni wanahistoria tu ndiyo ambao wataitendea haki...................kama kweli ilikuwa na manufaa yoyote yale kwa taifa wakati nafasi mbadala zipo tele.......kulikoni kushabikia elimu ya kikoloni...................

  Lowassa alipokwenda Mkwawa na kuzungumzia mass education na waalimu pale kuhoji kama inalipa kutelekeza ubora wa elimu........................Lowassa alichachamaa kuwa hayo ya ubora yatakuja baadaye.........................hakubainisha hiyo baadaye ni lini............................

  Sasa mbali ya ubora wa elimu yetu sasa unathibitisha ni tatizo na kiyama cha kitaifa kama matokeo ya kidato cha nne 2010 yanavyotuthibitishia kwani katika historia yetu hatujawahi kuwa na wanafunzi waliopata sifuri kufikia nusu ya idadi ya watihaniwa wote.........ukiachia mbali viwango vya kufaulu vimeshushwa maradufu ili kubeba wanafunzi wengi na kuwapa nafasi wanasiasa uchwara kuendelea kutughilibu na idadi feki ya kufaulu kwa minajili ya kutupotosha ya kuwa nchi inakwenda mbele wakati inarudi nyuma....................................


  Baya zaidi ni mfumo wa elimu ya Misri na kote kule Afrika ya Kaskazini ambayo tumekuwa mastadi wa kufukuzia kuiga kutokana na mashinikizo yasiyo na hekima wala utashi wowote wa Lowassa.........sasa imejitokeza ya kuwa haina maana yoyote ile kwani kunafaida gani ukawa nayo na huwezi kujiajiri au kuajiriwa?

  Kule Tunisia yule kijana aliyechochea vuguvugu la mabadiliko alikuwa ana elimu ya chuo kikuu na baada ya zaidi ya miaka minne ya kusaga lami alijiajiri kwa kutembeza mkokoteni na kuuza vitu vyake...........huko cheti chake cha digrii kipo mfukoni na kimekunjika-kunjika na kuchakaa vibaya sana..................yaani hana hata mahali pa kukitunza zaidi ya mfuko wa suruali yake...........

  Siku moja polisi wanaogemea utawala uliopo madarakani walimkataza asiendeshe hata huo mkokoteni na kumnyanng'anya na huyo kijana akaona sasa yamemfika akaamua kujichoma na petroli...............................na Afrika ya Kaskazini yote ikarindima kwa vurugu za kutaka mabadiliko ya kimfumo wa jinsi nchi zao zinavyoendeshwa kwa sababu hawanufaiki.............................

  Swali langu kwa Edward Lowassa baada ya kuwa na sera za kuiga mifumo ambayo sasa inaonekana siyo endelevu una lipi la kujitetea baada ya kulitia taifa hili hasara na hizi shule za kata wakati ambako fedha hizo tungelizielekeza kwenye vyuo vya ufundi na kuanzisha benki za wajasiria mali wadogodogo ili waweze kujiajiri baada ya mafunzo mchundo?

  Majibu tafadhali.....yanahitajika kabla ya hayo tunayoyaona Afrika ya Kaskazini hayajahamia hapa kwetu.............Ninaamini hayapo mbali sana......tuna mwaka mmoja au miwili kabla hatujaona machafuko ya vijana kudai uhuru wa kiuchumi..........
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ikumbukwe huyu Lowassa hakuimaliza kazi aliyoianza ya mapinduzi ya elimu kwa muda muafaka, ameishia njiani ilhali ulikuwa ni mpango maalum wa serikali ya awamu ya nne.
  Alipojiuzulu tu...ndipo harakati zote za ufuatiliaji kamilifu ulipoishia, predecessor wake hana habari juu ya muendelezo huo wa ELIMU na badala yake umeingizwa mradi wa KILIMO KWANZA.
  Hakika siwezi kumlaumu Lowassa, bali serikali ingeendeleza kwa kina juu ya ukamilishaji wa mpango huo maalum ambapo qualified teachers ndio ulikuwa mpango unaofuatia...nadhani serikali pia imelifanyia kazi suala la walimu kwa kuanzisha faculty nyingi za education ktk universities ili kwenda sambamba na uboreshaji wa elimu.
  Siku zote mwanzo huwa ni mgumu ktk jambo lolote, UZOEFU UNAONYESHA HIVYO.
  mnyonge mnyongeni ila HAKI YAKE MPENI, huyu bwana hastahili lawama...predecessor ndio aulizwe kulikoni???
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,526
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Crap n nonsense
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Vipi waziri wa elimu kwa sasa ana mpango gani kuziendeleza shule za kata?
   
 5. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  lowasa pamoja na kuwa fisadi kazi kubwa alifanya......... ila serekeli ya jk bado ilikuwa madarakani ilikuwa na uwezo wa kuendeleza pale mwenzao alipoachia,,,,,,,,,,,,,,,,,,, huyu mwenzie kaja na kilimo kwanza majuzi alitabainisha wanaomaliza form 4 wataenda knye kilimo kwa hiyo alijua kabisa matunda ya lowasa nikutoa ziro nyingi zimsaidie knye kilimo kwani ukipata div 1 utaenda form 5 na zoezi lake la kilimo kwanza lisingefanikiwa! wasiwasi wangu huyu nae sakata la dowans linaweza likamtoa akaja mwingine na kauli mbiu may be "maji kwanza" au "afya kwanza" wale wa kilimo kwanza mbegu zikaozea shambani
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  PHP:
  lowasa pamoja na kuwa fisadi kazi kubwa alifanya......... ila serekeli ya jk bado ilikuwa madarakani ilikuwa na uwezo wa kuendeleza pale mwenzao alipoachia,,,,,,,,,,,,,,,,,,, huyu mwenzie kaja na kilimo kwanza majuzi alitabainisha wanaomaliza form 4 wataenda knye kilimo kwa hiyo alijua kabisa matunda ya lowasa nikutoa ziro nyingi zimsaidie knye kilimo kwani ukipata div 1 utaenda form 5 na zoezi lake la kilimo kwanza lisingefanikiwawasiwasi wangu huyu nae sakata la dowans linaweza likamtoa akaja mwingine na kauli mbiu may be "maji kwanza" au "afya kwanza" wale wa kilimo kwanza mbegu zikaozea shambani
  Hiyo elimu haina mashiko na wala siyo endelevu......kwa hiyo hata kamajitihada ilifanyika kwa uzuri kiasa gani...............mwisho wake hautakuwa na mafanikio ila kuliandaa taifa kwa machafuko.....................................

  kwa sababu soko la kujiajiri halijaandaliwa na elimu hii ya mkoloni haiwezi kuwa ni maandalizi ya soko hilo..................................Elimu ya mkoloni ni ya kuwaandaa kwa kuajiriwa ajira ambazo siku nyingi zilikwisha kuota mbawa...................
   
 7. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  mkubwa tatizo hapa ni ubora wa elimu na sio namba ya watahitimu... hilo ndio la msingi duniani kote!!!
   
 8. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,884
  Likes Received: 2,833
  Trophy Points: 280
  Tanzania hii ndugu zangu kila mtu msanii tu! Huyu bwana aliwahi pia kwenda Thailand akaambiwa kuna mvua ya kutengenezwa na binadamu huyoooo mbio kuja TZ kutengeneza mvua sijui aliishia wapi na huo mpango wake? Yaani kila kitu viongozi wetu ni "Duplication" tu hawawezi kuwa Creative eti!! Na huwa wanashangaa hao wakienda nchi za wengine!! Mkwere naye akaenda Botswana akakuta Ng'ombe wa Kilo 1,000 akashangaa wakati kumbe hata hapa kwetu wapo!! Wanakurupukia kila kitu! Ama kweli CCM ni zaidi ya tunavyoijua!! Hapa hatutoki ndugu zangu!!!
   
Loading...