Lowassa alihukumiwa na bunge kuwa ni fisadi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo
 
Bunge lilimwona kuwa ni kibaka kupitia ripoti ya Richmond ya tume iliyoundwa na bunge kisheria.Na likatoa pendekezo kwa serilkali kuwa mtoeni huyo kibaka mwenye mikono mirefu.Serikali ikamwambia timua haraka achia ngazi waziri mkuu kibaka akaachia ngazi.Kule kumtoa uwaziri mkuu ilikuwa hukumu aliyopewa na bunge na serikali.

Kuhukumiwa si lazima ufungwe waweza fukuzwa kazi,simamishwa au lazimishwa kujiuzulu.

Wewe unaota jela tu na faini? UKAWA ndio taabu yenu mna uwezo mdogo mno wa kufikiri

Kwa nini hajafungwa au kwanini hakuna kesi mahakamani.
 
Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo

Katika hiyo mihimili mitatu, muhimili wenye uwezo wa kutoa hukumu ni MAHAKAMA PEKEE
 
EL aliwajibika ili kuiokoa serikali ya JK isianguke maana JK alihusika moja kwa moja na kashfa hiyo. Kwa busara ya EL akaamua kuwajibika badala ya serikali nzima. Huu ni uamuzi mgumu sana na wa kijasiri. Hakuna mahali popote Bunge limepitisha azimio la kumfukuza waziri mkuu wa wakati huo EL kwa kashfa ya Richmond.

Chadema na EL wameshasema mhusika mkuu wa Richmond ni JK, rejea speech ya Tindu Lisu
 
Huyu jamaa ameenda shule lakini Ana usomi hafifu asijue kazi za mihimili ya nchi
 
Chadema na EL wameshasema mhusika mkuu wa Richmond ni JK, rejea speech ya Tindu Lisu

Tundu lissu naye ni mwanasheria wa kumnukuu? Huwa anajiita mwanasheria mahiri.Alimshambulia Lowasa sana kuwa yeye ni fisadi akamtaja kwa jina.Baadaye kageuka anasema kuwa Lowasa si fisadi kwa kuwa hajawahi kupelekwa mahakamani.Alipokuwa akisema Lowasa fisadi hadi bungeni alikuwa sio mwanasheria? Kama alikuwa ni mwanasheria aliwezaje kumsema mtu ni fisadi bungeni na kwenye mikutano ya hadhara wakati yeye kama mwanasheria anajua hakutakiwa kumsema Lowasa kwa kuwa Lowasa alikuwa hajapelekwa mahakamani bado.

Katika wanasheria koko tundu Lissu ni mmoja wao.Na asivyo na haya hata kusimama tu aseme hadharani kuwa Mzee Lowasa samahani CHADEMA na sisi wabunge wanasheria tulikusema wewe lowasa fisadi wakati ulikuwa hujapelekwa mahakamani tusamehe tulikosea kaufyata kimya.

Tundu LISSU TAPELI WA KISIASA NA KISHERIA.USIMNUKUU KABISA TUNDU LISSU UNANIPA KICHEFU CHEFU
 
we pepeta wee ila leba huwezi kwenda maana utacharazwa bakora kwa tabia zako chafu
 
Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo

YEHODAYA, are realyl serious? Siamini kama maneno haya umeyatoa ukiwa uko fresh otherwise nakuona kama uko kwenye stress ya kiwango cha juu hadi unaona ni bora utoweke hapa duniani ili usishuhudie yanayojili. Hivi ni kweli umesahau mchakato mzima wa Richmond basi hata hitimisho la riport ya Mwakyembe nayo hukumbuki - pole sana. Kwa kifupi tu nikwambie kwa mujibu wa katiba yatu ya sasa ambayo si nzuri sana kwa wananchi, kati ya mihimili mitatu uliyoitaja ni MAHAKAMA pekee yenye uwezo wa kutoa hukumu. Au ulitaka serikali yote ipigwe chini? Lakini pia mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, vipi baada ya EL kujiondoa Ikulu, ndy ulikuwa mwisho wa ufisadi au ndy mfumo wa kulindana hivyo tunyamaze kana kwamba hakuna madudu mabaya ya kifisadi yaliyofanywa baada ya EL. YAANI HATA SAKATA LA TEGETA ESCROW HILI LA JUZI MNADIRIKI KUTUSAHARISHA HIVI HIVI TU! Tena kwa mzalendo wa kweli ni no no no no no and a big NO!
 
YAKO NI MADHARA YA KUWA NA AKILI ISIYOKUWA NA AKILI!! Bunge lilimuhukumu EL kwa kosa gani?! katika Bunge la ngapi na kikao cha ngapi!? hata kama ni kashfa ya Richmond; wewe uliwahi kuisoma ripoti ya Harrison Mwakyembe; ukaielewa? inasemaje? ilikuwa na kurasa ngapi, nini kilifuata baada ya hapo?! Unayajua maazimio ya Bunge kuhusu kashfa hiyo? yalikuwa mangapi? yanasemaje?je mangapi yaliwahi kutekelezwa?! je unajua mjadala wa Bunge kuhusu kashfa hiyo ulifungwa vipi? na nani? na kwa nini? Je unazifahamu ripoti za TAKUKURU na Mkaguzi mkuu wa serikali zilisema nini kuhusu kashfa hiyo?! Mbwiga wa Mbwiguke we?!

Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo
 
Mbunge wa bariadi mh Andrew chenge mmoja kati ya wapigaji hodari ndani ya serikali...kila kashfa kahusika na bado ni kada namba zote wa ccm...bado hamjawashawishi wanamabadikiko...kwa sera ya ufisadi
 
mabadilikooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Mwandishi wa makala ifuatayo ni kigogo wa Ikulu ya serikali ya CCM kwa sasa. Je hizi FACTS alizoandika kuhusu utendaji wa Magufuli zilibadilika? na kama hazikubadilika, kwa nini tumuamini Magufuli mgombea wa CCM ambaye ana utata kwa mujibu wa watu wa Ikulu ya CCM hiyo hiyo?

Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...
Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa,
Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
 
Back
Top Bottom