Lowassa alihukumiwa na bunge kuwa ni fisadi

haya mtoto wa kiroho wa nabii flora peter umesikika ila ni vizuri zaid kama ungesema bunge lilimshutumu kuwa fisadi maana bunge halihusiki kutoa hukumu labda kule kwenye bunge lenu mbezi beach

Huyo nabii flora peter ndio nani ni hawara yako au mkeo mi mbona simjui
 
Mwandishi wa makala ifuatayo ni kigogo wa Ikulu ya serikali ya CCM kwa sasa. Je hizi FACTS alizoandika kuhusu utendaji wa Magufuli zilibadilika? na kama hazikubadilika, kwa nini tumuamini Magufuli mgombea wa CCM ambaye ana utata kwa mujibu wa watu wa Ikulu ya CCM hiyo hiyo?

Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...
Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo' katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

"Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi," vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

"Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili," chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa,
Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

"Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
Hebu angalia upuuzi uliomo humo kila akifika sehemu anaandika jina limehifadhiwa,jina limehifadhiwa mtu akitaka kusema uongo ukimwululiza nani kakwambia akisema jina limehifadhiwa jua ni uongo
 
Lowasa alituletea majenereta ya richmond ambayo ya ubungo yanafua umeme hadi dakika hii, bila maamuzi magumu ya lowasa hata huu umeme wa mgao tunaoupata sasaivi tanzania ingekuwa gizani tangu 2007. Watanzania tumeshaamua kumpa lowasa kura zetu. Lowasa hoyeeeeeeeeeeee
 
Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo

Lowassa ajawai kua msafi wala hafai kuwa ata rais
 
Tundu lissu naye ni mwanasheria wa kumnukuu? Huwa anajiita mwanasheria mahiri.Alimshambulia Lowasa sana kuwa yeye ni fisadi akamtaja kwa jina.Baadaye kageuka anasema kuwa Lowasa si fisadi kwa kuwa hajawahi kupelekwa mahakamani.Alipokuwa akisema Lowasa fisadi hadi bungeni alikuwa sio mwanasheria? Kama alikuwa ni mwanasheria aliwezaje kumsema mtu ni fisadi bungeni na kwenye mikutano ya hadhara wakati yeye kama mwanasheria anajua hakutakiwa kumsema Lowasa kwa kuwa Lowasa alikuwa hajapelekwa mahakamani bado.

Katika wanasheria koko tundu Lissu ni mmoja wao.Na asivyo na haya hata kusimama tu aseme hadharani kuwa Mzee Lowasa samahani CHADEMA na sisi wabunge wanasheria tulikusema wewe lowasa fisadi wakati ulikuwa hujapelekwa mahakamani tusamehe tulikosea kaufyata kimya.

Tundu LISSU TAPELI WA KISIASA NA KISHERIA.USIMNUKUU KABISA TUNDU LISSU UNANIPA KICHEFU CHEFU

Tundu lissu hafai yule me nlkua namkubal sana saiv namuona mjinga tu!!!
 
Kuna wanao dai kuwa Lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,Serikali na mahakama.Bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.Serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.Chama cha Mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

CHADEMA wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya Lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.CHADEMA wana dharau kubwa kwa bunge.Wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha CCM kuwa ni FISADI.

CHADEMA kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.Kusema Lowassa hakuhukumiwa ni uongo

Hawajui kama mahakama n mhimili kama ulivyo bunge
ukihukumiwa na bunge na bunge inakuwa imetosha

lakin kama mnataka tena mahakama ya magufuli inakuja
 
Tundu lissu naye ni mwanasheria wa kumnukuu? Huwa anajiita mwanasheria mahiri.Alimshambulia Lowasa sana kuwa yeye ni fisadi akamtaja kwa jina.Baadaye kageuka anasema kuwa Lowasa si fisadi kwa kuwa hajawahi kupelekwa mahakamani.Alipokuwa akisema Lowasa fisadi hadi bungeni alikuwa sio mwanasheria? Kama alikuwa ni mwanasheria aliwezaje kumsema mtu ni fisadi bungeni na kwenye mikutano ya hadhara wakati yeye kama mwanasheria anajua hakutakiwa kumsema Lowasa kwa kuwa Lowasa alikuwa hajapelekwa mahakamani bado.

Katika wanasheria koko tundu Lissu ni mmoja wao.Na asivyo na haya hata kusimama tu aseme hadharani kuwa Mzee Lowasa samahani CHADEMA na sisi wabunge wanasheria tulikusema wewe lowasa fisadi wakati ulikuwa hujapelekwa mahakamani tusamehe tulikosea kaufyata kimya.

Tundu LISSU TAPELI WA KISIASA NA KISHERIA.USIMNUKUU KABISA TUNDU LISSU UNANIPA KICHEFU CHEFU

Mchangiaji utakua una utapia mlo kichwan au ubongo wako una matatizo ya kujilazimisha. Sote ni mashahidi jinsi Speaker mama Makinda alivyokuwa anajivunia uwepo wa Lissu katika kuweka sawa mambo mengi ya Kisheria Bungeni. Hata kama una ushabiki wa Kimbumbumbu, ueledi ukuongoze kidogo na ujitahidi kuwa fair kwa umahiri au ujuzi wa mwenzio hata kama una chuki nae!
 
Aisee ww mujamaa una akili sana. Kuna manyumbu ya ukawa hayajitambui humu.lowasa ni fisadi na kama ulivosema kashaadhibiwa na bunge, kashaadhibiwa na serikali kwa kkubali aachie ngazi, kashaadhibiwa na ccm kwa kukatwa na matumaini yake ya kilaghai. Na bado anasubiria adhabu ya mahakama sasa akan*yee debe zegerea. Tumkatae lowasa oct 25 hafai na ni fisadi na hilo linadhibitishwa na viongozi wote wa chadema hakuna ambae hajawahi kumwita lowasa ni fisadi!

kuna wanao dai kuwa lowassa ni msafi hakuna mahakama iliyowahi mhukumu kwa ufisadi.

Nchi ina mihimili mitatu ambayo ni bunge,serikali na mahakama.bunge lilishamhukumu kuwa ni fisadi mbele ya bunge lote.serikali ikampiga chini kuondoka uwaziri mkuu.chama cha mapinduzi kikaona kiungane na maamuzi ya bunge kikakata jina lake.

Chadema wasiojali maamuzi ya bunge ambalo hata wao walikuwemo hukumu ya lowassa ilipotolewa wakampa agombee uraisi.chadema wana dharau kubwa kwa bunge.wakiongea utafikiri wao hawakuwemo bungeni wanavyomtetea kwa nguvu.

Kuweka rekodi sawa ieleweke kuwa lowasa alihukumiwa na bunge na chama chake cha ccm kuwa ni fisadi.

Chadema kikaamua kumchukua fisadi aliyehukumiwa na bunge na chama chake.kusema lowassa hakuhukumiwa ni uongo
 
Back
Top Bottom