Lowassa akodishiwa ndege maalum na wafadhili wake, Yagharimu mamilioni!

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Wakati watu kama Sitta wakikodi magari maalum kwa ajili ya zoezi la utafutaji wadhamini na watu kama Makongoro wakijikongoja na magari ya marafiki zao; hali imekuwa tofauti kabisa kwa Lowassa kwani yeye amepatiwa ndege maalum kwa ajili ya shughuli hiyo ya kutafuta wadhamini!

Ndege hiyo 'private jet' ambayo Lowassa amepatiwa na wafadhili wake katika safari yake hii ya matumaini imetolewa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha Lowassa anazunguka mikoa yote nchini bara na visiwani kabla ya julai 12 na 13 ili akamilishe zoezi la kuwapata wadhamini 435 nchi nzima ili kufanikisha sharti la chama kwa wagombea nafasi ya urais.

attachment.php

Hii ndio ndege maalum Lowassa anayoitumia kutafutia wadhamini wake kote nchini bara na visiwani.

Pesa tu.
 
Attachments

  • FB_IMG_1433590432272.jpg
    FB_IMG_1433590432272.jpg
    23.5 KB · Views: 17,494
makongoro nyerere anabinuka mabarabarani na magari yake chakavu,ukimpa urais huyu ataanza kujikimu kwanza kimaisha kwa kujenga nyumba,kununua magari.....bora nimchague aliyevuka level hiyo
 
Unajua sifa moja ya mfanyabiashara au mwekezaji pale anapoweka pesa zake sehemu fulani? Sitakwambia mimi, tumia akili yako mwenyewe kujibu hilo.
 
Kumbe mwenzetu unatafuta aliye level nyingine. Naimani hata kwako na maisha yako unatamani mali na vitu,hata mke wako unataka uwe level nyingine.Hata mbinguni mwenyezi akupe sehemu yako tofauti na wengine.use cs (common sense).
 
Unajua sifa moja ya mfanyabiashara au mwekezaji pale anapoweka pesa zake sehemu fulani? Sitakwambia mimi, tumia akili yako mwenyewe kujibu hilo.

kwa hiyo unamaanisha makongoro nyerere anataka kufanya biashara ikulu
 
Huyo Makongoro hela ya mafuta ya gari anachangiwa na wananchi huko vijijini shilingi mia tano mia tano. Hivyo kama ni biashara atakuwa anafanya na hao Watanzania walala hoi wa huko vijijini.
 
akichangiwa lowasa ndio tatizo? mbona unakuwa na standard mbili?
 
HAMY-D hueleweki ,kuna siku unampondea lowassa siku nyingine unamfagilia....sasa umwambie tu akulipe jiunge safari isiyokua na uhakika hiyo
 
Last edited by a moderator:
Ina u-maalum gani?
Ina paramedics, movie theater, extra oxygen tanks, blood bank, resuscitation kits....

😝😝😝

Hivi ilikuwa ni lazima uchangie? Hii ni habari tu, soma upate yanayojiri na uende zako. Maswali mengi ya nini?
 
HAMY-D hueleweki ,kuna siku unampondea lowassa siku nyingine unamfagilia....sasa umwambie tu akulipe jiunge safari isiyokua na uhakika hiyo
anasubiri team lowasa wamtumie private message na kachakula kidogo akae kimya
 
Last edited by a moderator:
Ina u-maalum gani?
Ina paramedics, movie theater, extra oxygen tanks, blood bank, resuscitation kits....

😝😝😝

Ndiyo maana yake yaani full theatre, anatafuta wadhamini akiwa chini ya uangalizi wa madrzz.

Urais wa Pesa, manineer!
 
Nakumbuka mwaka 2008 Obama kwenye kampein zake alikuwa na dege kubwa hivi basi akawa anapanda kwa mbwembwe sana Samadu Hassan wa Star TV akawa anapamba kuwa 'anapanda kisela'. Kinamna fulani alikuwa anajitofautisha na McCain kwamba yeye yuko fit..
 
WanaJF,

Wakati watu kama Sitta wakikodi magari maalum kwa ajili ya zoezi la utafutaji wadhamini na watu kama Makongoro wakijikongoja na magari ya marafiki zao; hali imekuwa tofauti kabisa kwa Lowassa kwani yeye amepatiwa ndege maalum kwa ajili ya shughuli hiyo ya kutafuta wadhamini!

Ndege hiyo 'private jet' ambayo Lowassa amepatiwa na wafadhili wake katika safari yake hii ya matumaini imetolewa mahususi kwa ajili ya kuhakikisha Lowassa anazunguka mikoa yote nchini bara na visiwani kabla ya julai 12 na 13 ili akamilishe zoezi la kuwapata wadhamini 435 nchi nzima ili kufanikisha sharti la chama kwa wagombea nafasi ya urais.

attachment.php

Hii ndio ndege maalum Lowassa anayoitumia kutafutia wadhamini wake kote nchini bara na visiwani.

Pesa tu.
Afya haimruhusu kuzunguka na gari. Jina litabadilika sasa hivi akiendelea kutumia gari.
 
Back
Top Bottom