Lowassa akiri Kwamba Wananchi Wanaikimbia CCM

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Waziri Mkuu mstaafu, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ameiomba serikali kutokandamiza haki za msingi za raia na kujali haki za wanyamapori. Hata hivyo, amewataka raia kuheshimu mipaka.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji Bwawani, Mto wa Mbu, wilayani Monduli, Lowassa alisema pamoja na matatizo yaliyoko, ni muhimu haki za raia zikalindwa.

"Hapa Bwawani najua mna matatizo na Bational Park (Hifadhi ya Taifa)...naomba Serikali isifanye haki za wanyamapori kwa kugandamiza haki za msingi za raia," alisema Lowassa.

Aliongeza: "Tunaheshimu sana utalii kwa sababu unatuingizia fedha, lakini tuheshimu haki za msingi za raia..na nyinyi tuheshimu mipaka iliyowekwa."

Eneo hilo limekuwa na mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Manyara inayopakana nayo, suala ambalo ni moja ya kero kubwa kwa wakazi wake.

Akizungumzia wana-CCM waliyojitoa chama hicho, Lowassa alisema: "Anayetupinga, atupinge kwa hoja..Kama kero hazijatatuliwa...siyo unaamua kutoka halafu unataka uhongwe ili urudi."

Aliongeza kuwa ndani ya chama wanagombania utekelezaji wa Ilani na hapo ni haki kwa mwanachama kukasirika iwapo Ilani haitekelezwi, lakini si vinginevyo.

Mapema, akizungumza katika mkutano wa kampeni kwenye kijiji cha Migombani, Kata ya Majengo, Lowassa ambaye anatajwa kutowania tena ubunge na kuelekeza nguvu kwenye urais, alijinasibu kwa mafanikio aliyoyapata katika kipindi chake cha miaka 20 ya ubunge.

"Mwaka 1995 wakati naingia ubunge, mtu ukija hapa Mto wa Mbu lazima ulale, huwezi kutoka Monduli kuja hapa na kurudi...barabara ilikuwa mbaya kabisa," alisema na kuongeza anajivuna kuwa wamemaliza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama.

Alisema serikali ya awamu ya nne imefanya makubwa, ikiwa ni pamoja na usambazaji umeme na maji vijijini.

My take
Huyu fisadi Lowasa anajizonga sana ,hivi kama ilani za CCM zinaonekana ni za uowongo hazitekelezwi hivi mwananchi akikasirika ndio zitatekelezwa ? Mwananchi akasirikike kutamsaidia nini ? Hivi ni kosa ikiwa ilani za ccm zimedumaa na mwananchi anaona kuwa alidanganywa na mwananchi huyo ameng'amua kuwa hizi ilani ni uwongo mkubwa sana utaotumiwa na miccm kila inapokaribia uchaguzi mkuu ,hivi baki huko kufanya nini,abakie ccm kwa faida ya nani ? Kuwaweka wao madarakani au sio ? Kisha iwe kazi yake kukasirika tu ?

Wananchi walio ccm hawakasiriki tena ni kukihama chama hicho cha mafisadi na pakukimbilia wanapo si pengine ila ni UKAWA ,kwani uhuru wa kweli wa Mtanzania upo huko.

Chanzo:IPP Media

Ndugu, Kama huwezi hata kuelewa kilichoandikwa, utaweza vipi kufanya uchambuzi wenye mantiki.

Soma vizuri ili uelewe mantiki ya hoja za Mhe. Lowassa badala ya kuandika kwa kadri unavyodhani.

Watu kama wewe kwenye jamii pevu ni hasara tupu!.
 
Mungu amjalie mmeru Lowassa aimarike afya yake japo amuone rais toka UKAWA mwakani.
 
sisi kina gogo la shamba tulimshauri Luwasa siku nyingi kuamia CHADEMA lakini kwa kuwa ameng`ang`ania ccm urais atausikia tu, kwa mbali
 
Ndugu, Kama huwezi hata kuelewa kilichoandikwa, utaweza vipi kufanya uchambuzi wenye mantiki.

Soma vizuri ili uelewe mantiki ya hoja za Mhe. Lowassa badala ya kuandika kwa kadri unavyodhani.

Watu kama wewe kwenye jamii pevu ni hasara tupu!.
Ndugu , mbona unapanic bila sababu? Hebu tulia sindano ikuingie vizuri
 
My take
Huyu fisadi Lowasa anajizonga sana ,hivi kama ilani za CCM zinaonekana ni za uowongo hazitekelezwi hivi mwananchi akikasirika ndio zitatekelezwa ? Mwananchi akasirikike kutamsaidia nini ? Hivi ni kosa ikiwa ilani za ccm zimedumaa na mwananchi anaona kuwa alidanganywa na mwananchi huyo ameng'amua kuwa hizi ilani ni uwongo mkubwa sana utaotumiwa na miccm kila inapokaribia uchaguzi mkuu ,hivi baki huko kufanya nini,abakie ccm kwa faida ya nani ? Kuwaweka wao madarakani au sio ? Kisha iwe kazi yake kukasirika tu ?

Wananchi walio ccm hawakasiriki tena ni kukihama chama hicho cha mafisadi na pakukimbilia wanapo si pengine ila ni UKAWA ,kwani uhuru wa kweli wa Mtanzania upo huko.

Chanzo:IPP Media
[/SIZE]
[/FONT][/COLOR]

Kosa lako liko kwenye your take,i think you are unnecessarily attack our Next president kimakosa,nadhani kikubwa apewe nchi arekebishe kasoro zote,lakini kumuita FISADI ni kumnyanyapaa kisaikologia mzee wetu,sisi wengine tunayempenda tuko nyuma yake na tumenyanyasika naye,tumefedheheshwa naye na tutafurahi pamoja na yeye,
 
LOWASSA atausikia urais redioni.

Mnachekesha kweli nyie juzi kwenye maadhimisho ya uhuru haujaona mzee wa TEZI DUME amejistukia na ameanza kumvuta karibu akijua mwakani ni mambo mengine?hahahahah mtahangaika lakini ukweli jamaa ndo the next presida
 
anaweza kukumbia mitaa 100 kweli ameongea ukweli wananchi hawana imani na ccm tena sasa ni zamu ya UKAWA
 
My take
Huyu fisadi Lowasa anajizonga sana ,hivi kama ilani za CCM zinaonekana ni za uowongo hazitekelezwi hivi mwananchi akikasirika ndio zitatekelezwa ? Mwananchi akasirikike kutamsaidia nini ? Hivi ni kosa ikiwa ilani za ccm zimedumaa na mwananchi anaona kuwa alidanganywa na mwananchi huyo ameng'amua kuwa hizi ilani ni uwongo mkubwa sana utaotumiwa na miccm kila inapokaribia uchaguzi mkuu ,hivi baki huko kufanya nini,abakie ccm kwa faida ya nani ? Kuwaweka wao madarakani au sio ? Kisha iwe kazi yake kukasirika tu ?

Wananchi walio ccm hawakasiriki tena ni kukihama chama hicho cha mafisadi na pakukimbilia wanapo si pengine ila ni UKAWA ,kwani uhuru wa kweli wa Mtanzania upo huko.

Chanzo:IPP Media
[/SIZE]
[/FONT][/COLOR]
Na wewe fisadi tangu uwadhulumu wale watoto yatima wa marehemu mdogo wako nimekuona wa hovyo Sana!
 
Back
Top Bottom