Lowassa akanusha kuanzisha mtandao akaunti ya Escrow

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,162
2,000

Edward Lowassa

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amelaani kikundi cha watu kilichoanzisha ukurasa wa mtandao wa Twitter kwa kutumia jina lake unaohusu suala la Akaunti ya Escrow.

Katika taarifa yake jana, Lowassa alisema kikundi hicho kimefungua mtandao huo kwa anuani ya Lowassa edwardlowasa.
"Toka bunge limeanza mjadala wa kadhia ya Escrow account, kuna mtu au kikundi kwa sababu wanazozijua wao wenyewe wameanzisha akaunti ya mtandao wa twitter kwa jina la Edward Ngoyai Lowassa," alisema katika taarifa yake.

Alisema kwa kutumia ukurasa huo, mtu huyo amekuwa akiandika masuala kadhaa kuhusiana na suala hilo la escrow account na kile kinachoendelea bungeni, ikionekana kama ni kauli ya Lowassa.

"Tunawaomba wananchi kupuuza yote yanayoandikwa katika ukurasa huo. Watanzania tuachane na tabia ya matumizi ya mitandao ya kijamii kupotosha umma, tutumie mitandao hiyo kwa kuhamasisha maendeleo, amani, umoja na mshikamano kwa taifa letu," ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Last edited by a moderator:

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,389
2,000
Kwani walitegemea asemeje? hatuwezi kukubali nchi ikaendeshwa kwa visasi,yeye alishachafuka sasa leo anataka awachafue ili apande chati na akikaa pale si atafanyiwa naye visasi ili ashindwe tena sasa hiyo ni nchi ama kijiwe cha visasi? ndo maana nasema ccm mnatakiwa mtuachie nchi yetu na tutakuwa tayari kutumia njia yoyote ilimradi mwakani mnatuachia ardhi yetu,mmekuwa wakoloni weusi and we must fight you violently
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom