Lowassa akabidhi Madawati 500 kwa shule Ukonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa akabidhi Madawati 500 kwa shule Ukonga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by S2dak_Jr, Sep 12, 2012.

 1. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanabodi,

  Kuna taarifa kuwa Barrick Gold wametoa madawati 500 yenye thamani ya Tsh.15,000,000 kwa shule ya Jimbo la Ukonga.

  Habari zinadai kuwa EL ndiye aliyekabidhi madawati hayo kwa Makongoro Mahanga (MP), Mbunge wa Jimbo la Ukonga.

  Akiongea kwenye hafla hiyo, EL amesema amesikitishwa na matokeo ya kufeli masomo ya Sayansi kwa mitihani iliyofanyika mwaka jana.

  Source: Clouds Fm News saa 2:00 asubuhi leo.

  Swali:

  i) African Barrick Gold wasingeweza hao wenyewe kukabidhi madawati hayo bila ya kumualika EL?

  ii) Kuna nini kati ya EL na Mahanga? Au ndio exposure ya presidential races za 2015?

  Naomba kuwasilisha
   
 2. u

  upendom Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akifanya jema maneno akifanya baya maneno,acha *****!
   
 3. S2dak_Jr

  S2dak_Jr Senior Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Acha up****, rejea nilichouliza. Halafu madawati hayajatoka mfukoni mwa EL.

  Jema lipi amefanya EL? Kutuibia akishirikiana na African Barrick ili return kwetu iwe madawati!

  Tumia kichwa kufikiri na si kufuga nywele.
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  alichoki kuna ka wimbo kake ka zamani sana aliimba wanachuki binafsi achana nao
   
 5. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumatano, Septemba 12, 2012 05:23 Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, jana alikabidhi sehemu ya madawati 500 kwa shule za msingi zilizoko Kata ya Kipawa jijini Dar es Salaam. Lowassa alikabidhi madawati hayo yaliyotengenezwa kwa ufadhiri wa Kampuni ya Kuchimba Dhahabu ya African Barrick, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Msingi Minazi Mirefu, Wilaya Ilala, Dar es Salaam. Wakati wa hafla hiyo, Lowassa pia alitoa vyeti kwa Kampuni ya Barrick kwa kufanikisha utengenezaji wa madawati hayo na cheti kingine kwa Shirika la Lions Club of Dar es Salaam Mzizima ambalo limeweka maji safi na salama katika kata hiyo. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Lowassa aliwapongeza viongozi wa Barrick na Lions Club kwa kusema kuwa misaada waliyotoa inaonyesha ni kwa jinsi gani wanavyojali maisha ya Watanzania. Pamoja na shukrani hizo, alisema kuna haja taasisi hizo kuendelea kuisaidia jamii kwa vile misaada yao ni muhimu. Kuhusu Barrick, alisema kampuni hiyo ina kila sababu ya kubadilisha mtazamo wake kwa kuelekeza misaada katika sekta ya elimu badala ya utaratibu wa kampuni hiyo wa kuisadia jamii inayozunguka migodi ya dhahabu ya kampuni hiyo. “Nawapongeza sana Barrick na Lions Club Mzizima kwa msaada wenu huu kwa sababu mnaonyesha ni kwa jinsi gani mlivyo karibu na wananchi. “Lakini, nyinyi Barrick nawaomba msaidie zaidi sekta ya elimu kwa sababu kuna matatizo mengi yanayohitaji msaada wenu na mfano halisi ni jinsi matokeo ya kidato cha nne yalivyokuwa mabaya mwaka jana,” alisema Lowassa. Naye Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (CCM), alisema Barrick na Lions Club Mzizima, walitoa misaada hiyo kama sehemu ya utekelezaji wa mradi ulioanzishwa Machi mwaka huu katika Kata ya Kipawa uitwao Elimu Bora kwa Mazingira Bora. Kwa mujibu wa Dk. Mahanga, uwepo wa mradi huo katika kata hiyo kimekuwa ni kichocheo cha mradi kama huo katika kata zingine nchini. Awali, Makamu wa Rais wa Klabu ya Lions Dar es Salaam Mzizima, Mustafa Kudrat, alisema klabu yake iliamua kuisaidia kata hiyo baada ya kuombwa na Diwani wa Kata ya Kipawa, Bona Kalua. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Barrick, Emmanuel ole Naiko, alisema kampuni yake imekuwa ikitenga Dola za Marekani milioni 10 kila mwaka ili kusaidia shughuli za maendeleo katika maeneo yanayozunguka migodi ya Barrick. Pamoja na hayo, alisema madawati 500 yaliyotengenezwa kwa ajili ya shule tano za Kata ya Kipawa, yaligharimu Dola za Marekani 10,000. Toa Maoni yako kwa habari hii
   
 6. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,166
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Former Prime Minister, Edward Lowassa addressing Kipawa residents and other people appeared in hand over of 500 desks to Minazi Mirefu Primary School in Dar es Salaam


  Lowassa said helping Tanzanian children to get education can help them to resolve their own challenges in future such as unemployment challenge."If we help our children to get education they will have good opportunity of resolving unemployment challenge in future.

  "
  Speaking today at Minazi Mirefu Primary School in Dar es Salaam, Edward Lowassa who is also Monduli Province MP congratulated African Barrick Gold Mine for handing over to Minazi Mirefu Primary School 500 desks in their efforts of improving education sector in Tanzania."This is the way of improving education so other stakeholders should also join hands the government."

  The event of handing over desks was also observed by Deputy Minister for Labour and Employment and Segerea MP, Dr Makongoro Mahanga, Governmental Relations Director of African Barrick Gold Mine, Mr Emmanuel Ole Naiko, Kipawa Ward Counselor, Boma Kaluwa and other officials.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Huyu naye kapten wa nini??
  Netball??

  Huyu hata meli ikipinduka, yeye anag'ang'ana kuoga na suti yake.
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  He should not applaud all Africans because he is not among of them given that he is but a very big let down. He should talk about his role and that of Jakaya in Richmond scam that left our country in morass socially. Whenever I see his photo I feel like vomiting.
   
 9. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,694
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lowassa ni janga la kitaifa
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wivu utawauwa watanzania ..mtu akiwa na hela tayari fisadi,,,,,mtakufa na vijiba vya roho
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Yaya Toure acha kutumiwa kama nepi. Acha Lowassa ajisemee. Tunajua kuna mafisadi-fisi wanotumiwa na mafisadi papa kuwatetea kila mahali including JF. Ingawa ni wajibu na kibarua chako kumtetea huyu proved fisadi, tumia lau akili badala ya kuwashambulia watanzania wote. Kwani wewe unayemshabikia na kumtumikia huyu fisadi wako si mtanzania? Hitimisho la jumla ni ushahidi wa ujuha na umbumbumbu katika mambo. Ahitaji kusoma misahafu kama Mahabhurata wala Korani wala Biblia kujua kuwa Lowassa ni fisadi. Jitahidi mtafute lau utetezi unaoingia akilini badala ya kulaani na kutuhumu watanzania wote. Kwa walioathirika na ufisadi wa Lowassa hata ungetumia bahari nzima ya Hindi kumsafisha hatatakata kamwe.
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kuna uongozi ama kitu kinatafutwa nyuma ya huu msaada!
   
 13. k

  kwitega Senior Member

  #13
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ni fisadi hata hayati Mwalimu Nyerere alimkataa. Gamba lake lilishakuwa sugu hata akimwagiwa tindikali ni kazi bure!
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,481
  Trophy Points: 280
  Kuna wenzetu wa imani fulani wanamjua Mungu Mwana aliyejitoa kubeba dhambi za ilimwengu na ni kwa kuteswa kwake sisi tuliponywa!.

  Vivyo hiyo kuna Mtanzania mmoja mwenye uwezo wa hali juu sana alijitolea kubeba ziko la Richmond ambalo kiukweli limemtesa sana, ila naye pia ni vivyo hivyo, kwa kuteswa kwake, kuna watu wameponywa!.

  Urais wa 2015 mtashuhudia jinsi " Jiwe walilolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni"!.

  Na kwa wale wote wasio amini, amini nawaambieni, "lisilowezekana kwa binadamu, kwa Mungu linawezekana!".

  2015 ni CCM tena!, 2015 ni Yeye!.
   
 15. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pasco hizo zako ni ndoto za Alinacha. Tambikia sali hata funga hata uwe uchi hakuna mtanzania mpumbavu wa kuchagua fisadi aje kuiba zaidi. Kikwete ametosha. Hatuhitaji tena kizazi cha laana cha mafisadi wapenda sifa na kuiba bila kufanya lolote. Heri kutokuwa na rais kuliko kuwa na Lowassa kama rais. Hata hivyo si vibaya kuota kwa vile mwisho wa CCM ni 2015. Wewe, CCM na Lowassa wako mnajua hivyo. Hata kama mtamleta Lowassa kama kafara ya Richmond, bado atakuwa na maswali ya kujibu ni kwanini yeye na Kikwete walihujumu taifa.
   
 16. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Alinacha the dreamer.
   
 17. t

  tenende JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kidhungu!
   
 18. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kwani hapo EL kafanya nini cha maana??? shukrani kwa barrick kwa kutoa madawati 500 na sio hawa mafisadi *****!!!
   
 19. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mkuu Pasco kwa hiyo alibeba zigo la richmond kuwaficha mafisadi??? na wewe kabisa unakubali alifanya la maana!! sisi tunawataka mafisad wafichuliwe afu yeye anabeba zigo kuwaficha...ina make sense kweli!!!! sasa kama anaficha mafisad akiwa mbunge akiwa rais itakuaje??? huu ni mgando wa mawazo na ndoto za mchana......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Geezzle

  Geezzle JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Iv we pimbi ume2mwa na Lowasa?!ushachelewa.Is ss n kwa ufukara we2 km nchi,n wa kugawa madin km zawad then 2ngoje kuchongewa MADAWATI?!waza km una kchwa tmam we ****!
   
Loading...